PAROKO wa Kanisa Katoliki Parokia ya Isimani, wilayani Iringa Angelo
Burgeo (60) na msaidizi wake Herman Myalla (36) wamenusurika kufa baada
ya kuvamiwa na majambazi waliokuwa na silaha za moto, mapanga na nondo.
Paroko Angelo Burgeo |
Mbali na kupigwa risasi katika ubavu wake wa kushoto na kujeruhiwa
vibaya katika tukio hilo lililotokea majira ya 4.45 usiku wa kuamkia jana, Padri Burgeo alijeruhiwa vibaya nyuma ya kichwa chake baada ya
kupigwa na nondo.
Akizungumza na wanahabari katika hospitali ya mkoa wa Iringa ambako
viongozi wamelazwa kwa ajili ya matibabu, Kaimu Mganga Mfawidhi wa
Hospitali hiyo, Dk Faustine Gwanchele alisema Padri Myalla amejeruhiwa
vibaya kichwani baada ya kupigwa kwa panga na nondo.
Msaidizi wa Paroko, Bw. Herman Myalla |
"Walifikishwa majira ya saa sita usiku wa kuamkia jana, na wakaanza
kupatiwa matibabu wanayoendelea nayo mpaka sasa," alisema na kuongeza
kwamba Padri Bergeo alianza kufanyiwa upasuaji jana ili kuondoa vipande
vya risasi vilivyopo ndani ya mwili wake.
Tukio hilo limetokea ikiwa siku moja tu baada ya mlinzi wa Kanisa Katoliki Kihesa Iringa Mjini, Bathelomeo Nzigilwa (64) kujeruhiwa vibaya na majambazi waliovunja kanisa hilo na kufanikiwa kuiba mali mbalimbali zikiwemo fedha taslimu zaidi ya Sh 500,000.

Dk Gwanchelle alisema hali ya Nzigilwa ni mbaya kwasababu majambazi
waliomjeruhi walimvunja mfupa wa sehemu ya nyuma ya kichwa chake.