Kuanzia kushoto ni Felix Mshama, Noel Mlabwa, na Barnabas Shija
|
KWA wahudhuriaji wa Event nyingi sana za Injili za Jijini Mwanza, hizi sura pamoja na majina yatakuwa sio mageni kwao. Hawa ni Vijana toka Jijini Mwanza ikiwa ni Mazao ya Tanzania Fellowship of Evangelical Students(TAFES) katika Chuo Kikuu cha Mt. Agustino cha Jijini Mwanza.
Safari yao
ya Uimbaji ilianzia mbali kidogo, kila mmoja akiwa na historia yake, lakini
kukutana kwao TAFES Saut, kuna tengeneza historia nyingine ya vijana hawa
katika kumtumikia Mungu, na safari hii ni katika wimbo wao mpya wa "U
Mwema".
Wakiwa
katika studio za Makaya records za Jijini Mwanza, vijana hawa wanapata Idea ya
kufanya wimbo kwa kutumia Acoustic Guitar, chombo kilichopigwa na Felix Mshama
toka Mwanzo wa wimbo mpaka mwisho.
Tofauti na
Utengenezaji wa Video tuliouzoea kwamba inaanza audio halafu ndo inafuata
video, utengenezaji wa video hii ilianza Video kisha Audio ndo ikafuata kwa
kutengenezwa katika Studio za Makaya Records.
Video
Producer wa Wimbo huu akiwa ni Wynjones Kinye toka Kinye Media ndo
aliyehakikisha Video hii ina ubora wa kutosha huku rangi ya video hii ikiwa ni
ya tofauti na rangi za kawaida tulizozizoea kuziona kwenye video nyingine.
WASIFU
WAO
Barnabas Shija
|
- Aliwahi kuwa Praise leader wa Tafes mkoa wa Mwanza(2010/2011).
- Ni mmoja wa waimbaji waliofanya Back up katika Event ya Jehovah Yu Hai tour katika Mkoa wa Mwanza.
- Alishawahi kurekodi audio albam ambayo hakuitoa kutokana na Sababu za Ubora wa Kazi.
- Kwasasa anahudumu katika Praise Team ya Kanisa la FPCT la kurasini Jijini Dar es salaam.
- Graphic Designer (Banners na Posters)
- Kitaaluma ni mhitimu wa BA. Mass Communication (2012), SAUT-Mwanza.
Felix Mshama
|
- Mpiga Gitaa aina ya Acoustic na Bass.
- Aliwahi kuwa Mwalimu wa kwaya ya Caanan Anglican ya mkoani Dodoma akiwa na umri wa Miaka 18.
- Kitaaluma ni Mwanasheria (LLB, Saut-Mwanza, 2012)
Noel Mlabwa
|
- Mwimbaji wa Gospel Band ya Kingdom worshipers ya jijini Mwanza.
- Mpiga Drums mwenye mapenzi sana na mahadhi ya kikongo.
- Mwanasheria mwanafunzi Mwaka wa 4, Saut-Mwanza.
Wasiliana Nao, Kwa Namba zifuatazo;
0717 642263
0716 093245
0719 995061
Sasa itazame Video hiyo iliyopewa jina la "U Mwema"