Sanamu Mpya ya Papa Yohane |
Katika kile kinachooonekana kuwa ni
marekebesisho ya makosa yao, Roma wamezindua upya sanamu ya Papa Yohane
(John) Paul tarehe 19 Novemba, baada ya ile ya awali kushambuliwa na
kuharibiwa na watu kwa madai ya kuwa haifanani katu na baba huyo
mtakatifu, bali kama dikteta Benitto Mussolini.
Msanii ambaye amefanya kazi ya kuirekebisha, Oliviero Rainaldi amesema
kwamba ameridhishwa na matokeo ya alichokifanya, kwani ndicho alichokuwa
nacho kwenye mawazo yake.
Hapo awali baada ya kuzinduliwa mnamo 2011 mwezi Mei, mkosoaji kutoka
Vatican alisema kwamba sanamu hiyo inaonekana kama vile bomu ndo
limetua, na si Papa wetu mpendwa kama inavyotakiwa.
Sanamu kushoto ikiwa imeharibiwa, na kulia ikiwa baada ya marekebisho |
Sandro Barbagallo anaendelea kusema kuwa baada sanamu hiyo kukosewa, na
kwamba ni watu wachache walioweza kumtambua kama Papa, basi ilibidi
haraka iwezekanavyo meya wa jiji la Rome akutane na wasanii wataalamu wa
uchongaji, maofisa utamaduni na wanazuoni ili kuweza kuokoa jahazi. Na
hapo ndipo michoro ya Rainaldi ilipopitiwa upya na kufanyiwa kazi
ipasavyo, jambo ambalo sasa limefanikiwa, kwani Papa amewekewa tabasamu,
na pia anaonekana kuwa na shingo tofauti na hapo awali ambapo kichwa
chake kilifananishwa na tufe (mpira wa bowling).
Hata hivyo katika uzinduzi huo wa mara ya pili, wananchi siku zote
hawakosi ya kusema, na mjenzi wa barabara mwenye umri wa miaka 54
akafunguka.
"Sasa hivi inapendeza, naona wamefanya kazi nzuri, sio kama ilivyokuwa
mwanzoni, naona wamerekebisha uso, sasa nona tabasamu na pia shingo ipo.
Kazi ni nzuri".
Lakini msafiri mmoja akasema aliyefahamika kama Alberto Donella amekuwa tofauti na wenzake, yeye akisema.
"Sio yeye, sio yeye kabisa, alikuwa mwenye furaha - sio kitu kama hiki"
Alberto alisema alipokuwa akipita kando ya hilo sanamu na kuongeza,
"Kwangu mimi hiki naona kama ni jokofu tu".
- Gospel Kitaa -