BAADA ya kutoka Chuo cha Ualimu Butimba(Butimba TTC) wiki chache zilizopita, Jana shughuli nzima ya Jointmass ilihamia Chuo Kikuu cha Bugando ambapo Wanafunzi toka Matawi yote ya Tafes Mwanza walikutana pale.
|
With his Presence |
Vikundi mbalimbali vya Uimbaji vya Praise and Worship vilihudumu, pamoja na waimbaji binafsi pia walipata nafasi ya kuhudumu.
|
Sema na Moyo wako.................... (Ruth Lyanga) |
Moja ya Vitu vilivyopewa nafasi kwa Siku ya Jana, ni "TAFES AWARENESS", Mada iliyowakilishwa na Tafes Staff(Former Reginal Coordinator) Dada Upendo Mwangoka. Kati ya Mengi aliyoyazungumza, pia alieleza historia ya Tafes na Kazi zake pia.
|
Dada Upendo Mwangoka |
Kwa Upande wa Chakula cha Kiroho, Neno lilifundishwa na Mwl. Gilbert Ezekiel likiwa na Kichwa cha Somo kisemacho; "Nguvu iliyoko katika Ufahamu" na tukapitia Mistari ifuatayo; Yoh 8:31-32, Yoh 1:11, Mithali 8:9 na Waefeso 3:20.
|
Mwl. Gilbert Ezekiel |
|
Wanafunzi wakifuatilia somo kwa Makini |
Kusifu na Kuabudu pia kulipewa nafasi ya kutosha sana ili kushusha Uwepo wa Mungu mahali pale.
|
Tafes Praise Team |
Upande wa pili mambo yakawa hivi.........
|
Pipooooooooooooooo................!!! |
|
Mpaka chini, Mpaka chini..................!(Ester Denisy) |
|
Sephone Sospeter(Kwenye Keyboard) na Mutu ya watu Felix Mshama(Kwenye Guitar) |
Maombi pia yalikuwepo wa watu mbalimbali waliokuwa na Uhitaji.
|
Baadhi ya watu waliofanyiwa Maombi |
Mungu na akupe Neema ya kutambua Nguvu iliyoko katika Ufahamu.