Mkuu wa kanisa la Anglikana duniani, Rowan Williams |
KANISA la Anglikana nchini Uingereza limetupilia mbali uwezekano wa kuwaapisha wanawake kuwa makasisi huku kiongozi wa kanisa hilo akionesha wazi kusikitishwa na hatua hiyo.
Uamuzi huo umechukuliwa baada ya kupiga kura katika uchaguzi
uliofanyika juzi nchini Uingereza na kushuhudia makasisi waliopiga kura
wakiupinga muswada huo kwa asilimia 76.7 ya kura.
Uamuzi huo huenda ukaleta madhara makubwa katika kanisa hilo ambapo kulikuwa na matumaini makubwa ya kuboresha na kufanya marekebisho katika taasisi za kanisa hilo la Anglikana.
Kiongozi wa kanisa hilo duniani, Rowan Williams ambaye anamaliza muhula wake Desemba ijayo, amebainisha masikitiko yake kuona muswada huo unashindwa kupasishwa baada ya kupambana kwa muda wa miaka 10.