Muonekano wa Nje wa Kanisa Katoliki Porokia ya Kihesa |
WATU wasiofahamika usiku wa kuamkia Jana
wamevamia Kanisa Katoliki Parokia ya Kihesa Jimbo la Iringa, Mkoani Iringa na kuiba
baadhi ya mali huku mlinzi wa Kanisa hilo Bathlomeo Nzigilwa akijeruhiwa
vibaya na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa.
“Mimi nilifika hapa kanisani saa 11:40 alfajiri, na nilipofungua mlango wa kanisa kwa ajili ya misa nilishangaa mlango ukiwa wazi na kumuona mlinzi amekaa kwenye kiti huku kichwa chake kikiwa kimeinamishwa chini na kufunikwa kofia, nilijua amelala kumbe alikuwa ameumizwa na hajitambui," Alisema Sista Mgata.
Amesema alipomsogelea mlinzi huyo aliona
damu inatiririka chini na mwili wake ukiwa umelowa kwa damu na hapo
ndipo alipokwenda kugonga nyumba ya padre kutoa taarifa.
Pamoja na kuvunjwa kwa Kanisa hilo ofisi ya parokia nayo ilivunjwa huku vitabu, na kumbukumbu mbalimbali zikiwa zimechanwa na kuwa mavazi ya ibada na vifaa mbalimbali vya ibada vimeharibiwa vibaya, Taberenakulo ndogo nayo ikiharibiwa, msalaba kuvunjwa pamoja na Hostia Takatifu zikimwagwa kila mahali.
Kwa upande wake Katekista Agustino Luhama
mhudumu wa ofisi ya Parokia alisema hela anazozikumbuka kwa
harakaharaka ambazo zimechukuliwa na wavamizi hao ni zaidi ya shilingi
laki tano.
Akizungumzia tukio hilo Sista Lucy Grace
Mgata amesema aligungua kuwa kunauvamizi majira ya alfajiri alipofika
kanisani hapo kwa ajili ya ibada ya Misa za kila siku zinazoanza saa
12:00 asubuhi.
“Mimi nilifika hapa kanisani saa 11:40 alfajiri, na nilipofungua mlango wa kanisa kwa ajili ya misa nilishangaa mlango ukiwa wazi na kumuona mlinzi amekaa kwenye kiti huku kichwa chake kikiwa kimeinamishwa chini na kufunikwa kofia, nilijua amelala kumbe alikuwa ameumizwa na hajitambui," Alisema Sista Mgata.
Ndani ya Ofisi baada ya Uharibifu |
Pamoja na kuvunjwa kwa Kanisa hilo ofisi ya parokia nayo ilivunjwa huku vitabu, na kumbukumbu mbalimbali zikiwa zimechanwa na kuwa mavazi ya ibada na vifaa mbalimbali vya ibada vimeharibiwa vibaya, Taberenakulo ndogo nayo ikiharibiwa, msalaba kuvunjwa pamoja na Hostia Takatifu zikimwagwa kila mahali.
Damu zilizovuja baada ya mlinzi kupigwa |
Sista Mgata amesema hela za watumishi wa
Artare walizokuwa wakichangishana pamoja na fedha za chama cha kitume
cha utume wa Fatima zimechukuliwa japo bado hazijajulikana ni kiasi
gani.
“Pia wamechukua hela ambazo watumishi wa
artare walikuwa wakichangishana kwa ajili ya matumizi ya umoja wao, na
fedha za chama cha kitume cha utume wa Fatima nazo wamechukua ingawa
sijajuwa ilikuwa ni kiasi gani mpaka wao wenyewe waje waeleze kulikuwa
na shilingi ngapi," Alisema sista Mgata.
Muuguzi mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa Rustica Tung'ombe akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya mlinzi aliyeumizwa na kufukishwa hospitalini hapo leo |
“Hela ninazozikumbuka kwa harakaharaka
ambazo zimechukuliwa ni zaidi ya shilingi laki tano lakini zingine
sijapata idadi kwa sababu nilikuwa sijazijumlisha na zingine nilizipokea
jana kutoka kwa waamini mbalimbali” alisema Kat. Luhama.
Padre Aloyce Mdemu ambaye pia ni Makamu
wa Askofu wa jimbo hilo alisema bado ni mapema kujua thamani ya
uharibifu uliofanyika kwa kuwa bado wanaendelea na uchunguzi wa vifaa
vingine na maeneo mengine ambayo huenda hayajagundulika.
Mlinzi aliyejeruhiwa akiwa hospitali |
“Ni kweli tukio hili limetokea na
kutushtua sana hata kuumizwa nuzura kuuawa mlinzi wetu lakini bado ni
pame sana kujua thamani ya uharibifu wa vitu vyote vilivyoharibiwa kwa
sababu tunaendelea na uchunguzi wa vitu vingine na maeneo mengine ambayo
huenda nayo yameharibiwa na hayajajulikana. Tutakapokuwa tumekamilisha,
taarifa zitatolewa” alisema Pd. Mdemu.
Hata hivyo Muuguzi mfawidhi wa hospitali
ya Mkoa wa Iringa Rustica Tung’ombe alikiri kumpokea majeruhi ambaye ni
mlinzi wa kanisa hilo na kusema kuwa hali yake ni mbaya japo kuwa
anaendelea kupatiwa matibabu.
“Tumempokea majeruhi Bathlomeo Nzigilwa
mlinzi wa Kanisa ambaye ni mkazi wa kwa Semtema akiwa na hali mbaya, na
bado hajapata ufahamu, ila anaendelea na matibabu,” alisema Tung’ombe.