Advertise Here

Sunday, March 17, 2013

Holly Gospel Search mkoani Iringa yaanza rasmi.

Bi. Kazi Nyolo, Muandaaji wa shindano hilo akisisitiza Jambo kwa Washiriki
HATIMAYE ule mtanange wa kusaka vipaji vya Waimbaji wa Muziki wa injili toka Mkoani Iringa yaani Iringa Holly Gospel Star Search umeanza rasmi Jana katika ukumbi wa Tucta katika manispaa ya Iringa huku kila mshiriki akionesha hamu ya kuwa mshindi. 

Wakizungumza na mtandao huu baadhi ya washiriki wamesema kuwa kwa sasa wameanza kutambua nini wanachokifanya  kutokana na ushindani kuendelea kuwa mkubwa zaidi.
Mwamvita Bernard, ambaye ni Mmoja wa washiriki wa shindano hilo akiwa mbele ya Jopo la Majaji
 Kwa upande wa mwandaaji wa mashindano hayo Bi. Kazi Nyolo amesema kuwa washiriki lazima wahakikishe kuwa wanakuwa makini kwani siku zilizobaki ni chache sana.
  
- Denis Nyali (GNM Iringa) -

Papa Francis akataa vitu vya kifahari.

Papa Francis I
Siku chache baada ya kuchaguliwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amewashangaza wengi mengi kwa kukataa kuvaa viatu vya kifahari na msimamo wake kuwekwa wazi kuwa hatavumilia makasisi watakaotenda uovu.

Tayari, Papa Francis ameelezwa kuwa kiongozi asiyetaka makuu, mhafidhina na mtu ambaye hataweza kubadili mengi katika kanisa hilo lenye waumini bilioni 1.2 duniani.

Katika siku mbili za uongozi wake, Papa Francis amelithibitisha hilo kwa kutokea hadharani akiwa amevaa viatu rahisi, vyeusi na kuachana na vyekundu vya kifahari vilivyopendelewa na mtangulizi wake, Benedict VXI.

Katika uongozi wake, siku zote Papa Benedict, alivaa viatu vyekundu vilivyotengenezwa kwa mkono, jambo ambalo Papa Francis anaonekana kuachana nalo.

Watu walio karibu naye Papa Francis, wanaeleza kuwa kabla ya kuondoka Buenos Aires, Argentina kwenda Rome, Kardinali Jorge Mario Bergoglio, kama alivyojulikana awali, alivaa viatu rahisi vya rangi nyeusi, na kuwafanya marafiki zake, wakiwamo mapadri kutaka kumnunulia viatu vingine vipya.

“Siku ile aliyoondoka mjini Buenos Aires kuelekea Rome kwa ajili ya mkutano wa uchaguzi wa Papa (conclave), marafiki zake walimpa zawadi ya viatu. Yeye, siku zote amekuwa akitokea hadharani akiwa amevaa nguo rahisi, viatu vya kawaida,” walieleza mapadri hao kutoka Amerika Kusini walipozungumza na Kituo cha Redio Vatican. 

Mbele ya Makardinali 106 
Juzi Ijumaa alipokutana na makardinali 106, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 76, licha ya kuonyesha uso wa furaha na kuwatania aliwaonya makardinali hao kuhusu wajibu wao kama viongozi wa kanisa maeneo mbalimbali duniani akiwataka kutosahau kuwa hawarudi kwenye ujana.

Katika ukumbi wa Sala Clementina, ulioko Vatican Papa Francis pia aliwataka makardinali hao wakiwamo waliomchagua kuwategemea zaidi vijana aliosema ndio nguzo kuu muhimu ya ustawi wa Kanisa Katoliki, huku aliwashauri makardinali kusaka njia sahihi ya kueneza Ukristo pande zote za uso wa dunia katika karne ya 21.

Aidha, alimsifu mtangulizi wake, Papa Benedict kwa uamuzi wa kijasiri wa kustaafu, akieleza kuwa ni uamuzi wa busara, wenye kuonyesha ukomavu na kuwataka wasichoke kuiga matendo mema.

- Mwananchi -

Saturday, March 16, 2013

Mfahamu kiundani Jessica Honore na The Jessica's Music.

Jessica Honore
Jessica Honore ambaye ni Mtoto wa 6 na wa mwisho kuzaliwa katika familia ya kitumishi amerithi kipaji cha uimbaji toka kwa wazazi wake, kaka pamoja na dada zake. Watoto wa familia yao wengi wamekuwa ni waimbaj na wapiga vyombo vya Muziki.

Jessica alianza uimbaji akiwa na umri wa miaka 6. Alikua akiimba kwaya ya watoto Kijitonyama Pentecoste, na baadae Mwananyamala Pentecoste. Huko ndiko alikokukuzia huduma iliyokua ndani yake. Mnamo Mwaka 2005 akiwa darasa la 7 Jeesica akasikia habari za mashindano ya Uimbaji(Gospel Star Search).
Jessica akiwa na baadhi ya Washiriki wa Gosprl Star Search ya Mwaka 2005
Jessica anasema "Wakati huo sikuwa katika mazingira ya kuniruhusu kushiriki shindano hilo, ila kwa msukumo uliokuwa ndani yangu juu ya uimbaji na kwa ruhusa na ushirikiano wa Mama yangu, niliweza kwenda katika usahili na kushiriki shindano hilo. Baada ya mchakato mrefu sana, ulio jumusha washiriki toka mikoa mingine ya tanzania kama mitatu hivi, ndipo nikafanikiwa kuibuka mshindi."

"Hapo ndipo nilipoanza safari rasmi ya uimbaji. Nilifanikiwa kupata gari na kusomeshwa elimu ya sekondari mpaka kidato cha 4 kupitia Ushindi ule chini ja usimamizi wa Walezi Ruge Mutahaba na Michael Nkya. Pia Mwaka huo huo wa 2005 nikafanikiwa kutoa track yangu ya kwanza iliyojulikana kama "Mungu Yupo" na ikafanya vyema katika vyombo mbalimbali vya habari, ingawa bado sikuwa tayari kuingia deep kwenye maswala ya Muziki kwani nilikuwa bado ni Mwanafunzi na nilikua chini ya uongozi ambao haukuhitaji kunipeleka puta, maana waliona nahitaji kukua kiuimbaji, kielimu na kiakili." Aliongeza Jessica.
Jessica akiwa Studio
Baadaye akafanikiwa kutoa nyimbo nyingi sana akiwa bado anasoma, chini ya usimamizi wa Mlezi wake Rugemalila. Baadhi ya Nyimbo hizo ni kama Sitaogopa, Mtumikie, Sifuni, Sitahofu na nyingine nyingi ila hakutengeneza album. Mnamo Mwaka 2010 baada ya kumaliza shule Jessica alifanikiwa kutengeneza album ya Tenzi za Rohoni, ila kwa sababu mbalimbali haikuweza kutoka.

Baada ya kumaliza kidato cha 4, Jessica alitamani sana kwenda shule ya Uandishi wa Habari(School of Journalisim) ila haikuwezekana kwa kipindi hicho na ndipo akaanza rasmi kazi ya Muziki. Wakati huo alianza kwa kufanya Matangazo mbalimbali na Jingles pia hasa za Clouds Fm, na zikapendwa sana na watu. Pia alifanya Matangazo ya Kampuni za simu kama Vodacom na Zantel.
Jessica akiwa katika Utengenezaji wa Video yake ya Napokea
Jessica anasema " Pia nimekuwa nikiitwa kwenye hafla mbalimbali kuhudumu kama Harusi, Misiba na Sherehe mbalimbali huku nikitumia Keyboard pamoja na Mpigaj aitwae Isaya, na kwahiyo niliweza endesha Maisha yangu vyema. Nilipendelea pia maswala ya Modeling na Designing na Wakati mwingine nimekuwa nikichora designs za nguo kwa mitindo mbalimbali."

Jessica alianza jitegemea mwaka 2010, na Mwaka 2011 Emmanuel Mabisa alimfuata na kumshirikisha swala la Glorious Celebration. Jessica anasema, "Sikusita maana nilikuwa napenda sana kushirikiana na waimbaji wengine ila ilikuwa ni kwa makubaliano ya kua nitapotaka anza rasmi simamia maono yangu nitatoka Glorious Celebration na kuanza simamia kitu kilicho ndani yangu. Pia mwaka huo huo nikapata nafasi katika kanisa la Word Alive Center kwa kufundisha Praise Team na kuanza kusali pale baada ya kua Christ Embassy kwa miaka mitatu.
Jessica akiwa na Glorious Celebration
Mwaka jana(yaani 2012) Mwezi wa 5 au wa 6 alianza chukua hatua ya Maono yake huku akiendelea shughurikia album yake aliyokua ameitelekeza kwa muda mrefu. Jessica anasema ilikua ni changamoto maana alikuja gundua kuwa alikua akua kiuimbaji hivyo ikabidi aanze kuziimba upya Nyimbo za kwenye Album hiyo. Jessica anaendelea kusema kuwa amekuwa na maono ya muda mredu ya kua na team maalum ya kuhudumu nayo mahali mbalimbali kwa kufanya Live Music, kuwa na shule ya Muziki, pamoja na eneo ambalo watu wanaweza kuwa wakilitumia katika Kusifu na Kuabudu yaani Cathedral of Worship.
Jessica katika pozi
"Pia napenda kuwa na studio kubwa ya muziki na kwa kutambua hilo nikaanza kwa kujitoa kufundisha watu ambao wamekua wakihitaj msaada wangu. Mwaka jana mwishoni nilifanikiwa kuanzisha Team yangu kwa kupata mabinti walio kua na vipaji ila walihitaji uzoefu na mafunzo ya ziada ili kukua na kuimba vizuri. Hivyo nikawafundisha na pia nikawashirikisha baadhi ya wapigaji wa vyombo akiwemo kaka yangu wa kufuatana John na akakubali na kunisaidia kusimamisha maono yangu."

Mwaka jana mwishoni nikaanza kuhudumu na mabinti zangu na wakaka wawili niliowafundisha mwenyewe. Baada ya kuona tumefanya vizuri katika tamasha la Holy Bass Guitor lililofanyika pale DPC mwaka jana, nikaamua kuwa serious zaidi na kujikita kufanya huduma ikue. Kweli huduna ikaanza kukua, watu wa kufanya back up wakaanza ongezeka pamoja na wapiga vyombo maana wakati huo bado nilikua sijapata wapigaji maalum wa kuwa nao katika huduma. Ndipo nikawa na msukumo wa kufanya huduma hii kwa ukamilifu zaidi."
Jessica(aliyekaa) akiwa na baadhi ya waimbaji wake
"Baadaye nikapata msukumo wa kuandaa tamasha la uzinduzi wa album yangu ya kwanza ili kuelezea maono yangu na kutambulisha team yangu nitakayokuwa nikihudumu nayo kwa jina la THE JESSICA MUSIC. Na kwa mwaka huu nikaanza mikakati mingi kwa msaada wa Pastor mmoja toka Nchini Zambia Pastor John Mumba aliyeguswa na huduma yangu na kuamua kunisaidia kupanua ufahamu wangu kufikia ndoto zangu, na akawa bega kwa bega pamoja na Mume wangu mtarajiwa Boniphace Magupa mpaka kufikia hapa."
Jessica akiwa na Mume wake Mtarajiwa Boniphace Magupa
Kwa sasa The Jessica Music ina member wasiopungua 10 ikiwa ni waimbaji na wapiga vyombo. jessica anasema "Namshukuru Mungu kwa kuwa nao mana ni Baraka katika Maisha yangu na kwangu ni ushuhuda mkuu wa Mungu alikonitoa". Sasa The Jessica Music inaelekea katika tamasha la ZIMA UKIMYA NA JESSICA HONORE, Tamasha litakalofanyika pale City Christian Centre - Upanga Machi 24, Mwaka huu kuanzia Saa 9 Alasiri - Saa 1 Usiku. Kiingilio katika tamasha hilo kitakuwa ni Tshs. 15,000. USIKOSEEE!

Hii ni Video ya Wimbo wa Jessica Honore unaojulikana kama Napokea

Ruth Lyanga, Mwimbaji anayefuata Nyayo za kaka yake Lyanga George.

Ruth Lyanga George
Jina lake Kamili ni Ruth Lyanga George. Alizaliwa Mwezi Novemba 1986 huko Musoma Mkoani Mara. Ni Mtoto wa 4 kuzaliwa kati ya Watoto wanne wa Mr. George Manase Lyanga, na Mama alikuwa anaitwa Neema Manase (Alifariki Mwaka 2004). Kwa upande wa Kabila, Ruth ni Mnyiramba toka Singida.

Elimu yake ya Msingi aliipata kwenye shule ya Msingi Kapolo iliyopo Ifakara, Morogoro (1994-2000), Elimu ya Sekondari aliipata Kwenye shule ya Sekondari Kilombero (2001-2004), Elimu ya Kidato cha 5 na 6 aliipata kwenye Shule ya Sekondari Bahari Beach (2007-2009). Na kwasasa Ruth anasomea Shahada ya Mahusiano ya Umma na Masoko (Ba. Public Relation and Marketing) mwaka wa 2 katika Chuo Kikuu cha Mt. Augustino, campus ya Mwanza.
Ruth Lyanga akiimba katika Tukio la Uzinduzi wa Kitabu cha "Wokovu ni Uhakika wa Maisha ya Sasa na ya Baadaye" kilichoandikwa na James Kalekwa.
HISTORIA YAKE KIUIMBAJI
Ruth alianza kuimba katika kwaya ya Sunday School, na baadae alianza kuimba katika Kwaya ya Kanisa la Kapolo EAGT Morogoro. Mwaka 2005 wakaanzisha kundi la King Jesus Family likiwa na Waimbaji kama Eliana, Witness, Penina, Pendo, Lyanga, Ruth Mwenyewe pamoja na David.

Mwaka huo huo 2005, Ruth, Lyanga, pamoja na Witness walishiriki Gospel Star Search wakiiwakilisha King Jesus Family toka Mkoani mbeya ambapo walikuwa Washindi wa Mkoa hivyo Waliiwakilisha Mbeya katika Mashindano hayo ya Gospel Star Search.
Ruth akiwa na Praise Team iliyohudumu Siku ya Uzinduzi wa Kitabu
Mshindi wa Kwanza katika Gospel Star Search hiyo ya Mwaka 2005 alikuwa ni Jesca Honore, wa 2 alikuwa Jonsia Njamanse, na wa 3 alikuwa ni Lwiza John. Washiriki Wengine wa Gospel Star Search hiyo ya Mwaka 2005 ni kama Betty Lucas, Victor Aron, Meshack Mwakyebula na Charles Thobias.

Mwaka 2007 Ruth akiwa na King Jesus Family walitoa Albam ya Kwanza kama Kundi iliyo05 ni kama Betty Lucas, Victor Aron, Meshack Mwakkuwa na Jina la “Twende Nawe” iliyokuwa na Nyimbo kama Sema nami, Hosanna, Yahwe pamoja na Twende nawe. Na kwasasa kundi hili lilikuwa linaundwa na Waimbaji toka familia Moja yaani Ruth, Lyanga pamoja na David.

Lyanga ni Mwimbaji na pia ni Audio Producer katika Studio yake Mwenyewe inayojulikana kama Icon Production iliyopo Maeneo ya Bandari Jijini Dar es saalam. Kwasasa ni Kiongozi wa Glorious Celebration ya Jijini Dar es salaam na pia yuko katika Mchakato wa Kumalizia Album yake ya Pili ambayo itatoka sambamba na Video baada ya album yake ya Kwanza ya "Umenishika Yesu" kufanya vizuri.


Tafes Saut (Praise and Worship Team) toka katika Chuo Kikuu cha Mt. Augustino campus ya Mwanza, ndipo ambapo Ruth anaendelea na Huduma yake ya Kumtumikia Mungu kupitia Uimbaji kwa sasa.
Ruth katika Pozi
Hii pia ilikuwa ni Sehemu ya Mazungumzo yetu kati ya Gospel News Media na Ruth Lyanga…….

Gospel News Media; Ni Mwimbaji gani wa hapa Nyumbani Tanzania unayevutiwa na uimbaji wake?


Ruth Lyanga; Ni wengi, lakini hasa ni Upendo Kilahiro, Jackon Benty na Marehemu Fanuel Sedekia kwasababu wao ni waimbaji walioegemea sana katika Upande wa Nyimbo za Kuabudu.


Gospel News Media; Na kwa Upande wa Nje ya Nchi Je!?


Ruth Lyanga; Kwa Nje ya Nchi navutiwa sana na Benjamin Dube pamoja na Kirk Franklin


Gospel News Media; Je! Una mpango wa kuwa Solo Artist kwa baadae?


Ruth Lyanga; Yah! Mpango huo upo, lakini ntakuwa nashirikiana na Waimbaji wengine kama wanavyofanya waimbaji kama Cece Winans, na Benjamin Dube.

Gospel News Media; Nini Matarajio yako ya Baadae?

Ruth Lyanga; Natarajia kuwa Mwimbaji wa Kimataifa, na Mtumishi wa Mungu katika eneo la Kufundisha Neno lake kama alivyo Joyce Meyer. Na si kwa baadae tu bali hata hivi sasa Mimi na Mtumishi wa Mungu na Bwana anaendelea Kuniandaa.


Gospel News Media; Nini Malengo yako ya Baadae?


Ruth Lyanga; Kwa baadae nina Malengo ya kuja kufungua Taasisi itakayojishughulisha na Utoaji wa Elimu kwa Vijana, na hasa Elimu ya Kumjua Mungu pamoja na Elimu ya Ujasiriamali, Muziki na Uimbaji.


Gospel News Media; Nashukuru sana kwa Ushirikiano wako!


Ruth Lyanga; Nashukuru pia!
 
Tazama Video hii, Ruth Lyanga aki’lead Wimbo wa “Katikati ya Wafalme”

Jenipher Mgendi kutoka na "Hongera Yesu".

Jenipher Mgendi
Mwimbaji Mkongwe wa Nyimbo za Injili Tanzania ambaye kwa Muda mrefu sasa amekuwa akijihusisha pia na utengenezaji wa Filamu Jenipher Mgendi, anatarajia kutoa album yake mpya Mwezi wa 5 Mwaka huu.

Akizungumza na Gospel News Media, Jenipher amesema kuwa album hiyo itakuwa na Jumla ya nyimbo 8 na Nyimbo zote ameimba peke yake pasipo kumshirikisha Mwimbaji yeyote.

Baadhi ya Nyimbo zitakazopatikana katika Albam hiyo ni kama Hongera Yesu(Wimbo uliobeba Jina la album), Msimamo, Asante Yesu, na nyinginezo. Kwa Mwezi huo wa 5, Album hiyo itatoka katika Mfumo wa audio peke yake.

Mtandao huu ulipotaka kujua sababu za Jenipher kuwa kimya kwa muda Mrefu, Jenipher amesema kuwa alikuwa akitengeneza Filamu 2 ambazo ni "Teke la Mama" pamoja na "Chai Moto".