Advertise Here

Tuesday, February 12, 2013

Emmanuel Nyambita; Natamani sana kufanya Kazi na Mwimbaji Don Moen.

Emmanuel Nyambita
Emmanuel Nyamita ni Mwimbaji wa Nyimbo za Injili toka mkoani Mwanza ambaye kwasasa Makao yake Makuu yako Nchini Kenya katika Jiji la Nairobi.

Aina ya muziki anaoufanya, umekuwa kivutio tosha kwa kila anayemsikiliza na kumtazama. Kwa muda mrefu sana amekuwa akifanya Muziki wa LIVE huku akipiga Gitaa lake aina ya Acoustic ambalo alifundishwa na Bw. Joshua aliyekuwa akiishi Maeneo ya Nsumba Jijini Mwanza.
Emmenuel ambaye ni Mhitimu wa Shahada ya Elimu toka Chuo Kikuu cha Mt. Augustino cha Jijini Mwanza - Tanzania(2012), anasema alianza shughuli hizi za Uimbaji Mwaka 2000 akiwa nyumbani kwao.

Emmanuel anasema "Baada ya hapo nilianza kuwa serious nilipojiunga na Nsumba secondary iliyopo Jijini Mwanza, ambapo nilijiunga na kaka yangu na rafiki zake. Wao walikua Kidato cha 4 wakati Mimi nikiwa Kidato cha Kwanza. Hiyo ilikuwa Mwaka 2003.
 
Kwahiyo tukaimba pamoja nao kwa Mwaka 1 na Kisha wakaondoka na kuniacha peke yangu. Baadaye nikaunda Kundi nikiwa na Marafiki zangu tulilolipa Jina la LTS mpaka tunamaliza Kidato cha 4.

Nilibahatika kufaulu kidato cha 4 na hivyo kuchaguliwa Shule ya Serikali lakini sikujiunga na shule hiyo ya sekondari ya serikali na hivyo nikaamua kwenda shule Binafsi ya Ikizu High School sababu walikuwa wanafundisha somo la Muziki.
Emmanuel akiwa na Harris Kapiga katika kipindi cha Gospel Tracks kupitia Clouds Fm
Kwa bahati mbaya huko nako nikakuta Mwalimu wa Somo la Muziki kaondoka lakini palikuwa ni sehemu sahihi pa kukuza vipaji hasa vya Muziki mana kulikuwa kuna Talents Night, na pia uimbaji ulipewa kipaumbele sana.

Hapo shuleni nilikutana na Rafiki yangu aitwaye Gerlad Saul (kwa sasa yupo IFM) na kisha tukaunda kundi la "The Two Brothers" tukiwa wawili tu. Kwakweli tulikuwa tunafanya vizuri sana mpaka tunamaliza shule.
 
Baada ya hapo nikafanikiwa Kufaulu Masomo yangu na Kujiunga na Chuo Kikuu cha Mt. Augustino kilichopo Mwanza, Tanzania na kuendelea na Shughuli za Uimbaji mimi peke yangu."

ALBUM YAKE MPYA YA SASA
Emmanuel amefanikiwa kurekodi Album yake yenye Jina la NINARUDI, Albam aliyoifanya katika Studio ya 3J Studio ya Jijini Nairobi, chini ya Producer Allan Mayindo ikiwa katika Mfumo wa Audio Cd na Sasa anamalizia Video ya Nyimbo zake hizo katika Mfumo wa DVD na Muda wowote kuanzia Sasa itapatikana Madukani.

Album hiyo ina Nyimbo 7 zikiwemo Nyimbo kama Touch me, Wanataka kunitoa Roho, What do we do na Nyinginezo. Album hiyo itakuwa na Nyimbo zilizoimbwa kwa lugha 2 ya Kiswahili na Kiingereza. Na anasema aliamua kuimba kwa kutumia lugha ya kiingereza kwasababu ana lengo la kufanya muziki wa Kimataifa.
 

MALENGO YAKE YA BAADAE
Kwa Upande wa Malengo yake ya baadae, Emmanuel anasema anatamani sana Kufanya Muziki wa Injili katika level ya Kimataifa, na Pia anatamani sana kufanya Kazi na Mwimbaji wa Kimataifa wa Nyimbo za Injili Don Moen.

Kwa Maelezo zaidi, wasiliana Nae;
Email; e.nyambita@gmail.com
Facebook Account; Emmanuel Nyambita

JIANDAE KUJIPATIA NAKALA YAKO!!!

Monday, February 11, 2013

Vita vya Waislamu na Wakristo Geita, Mchungaji Auawa.

HUKO mkoani Geita, kuna vita kati ya Waislamu na Wakristo, kufuatia hatua ya Wakristo kuchinja mifugo kwa nia ya kuuziana wenyewe kwa wenyewe kwenye bucha walilotenga.

Jambo hilo linaelezwa kuzua tafrani kwa jamii ya Waislamu, kwani waliamua kuvamia eneo hilo na kuharibu bucha, pikipiki eneo hilo, na kusababisha watu kuingilia, na vita kuibuka, silaha za jadi zikitumika.

TUKIO:

Wakristo Mkoani Geita eneo la Katoro na Buselesele, waliamua kuachana na kununua nyama katika bucha za kawaida kwa madaikwamba hiyo ni ibada kwa waislamu, na hivyo wao hawako tayari kushiriki ibada hiyo, na badala yake watafanya ya kwao. Ndipo walipokwenda Kituo cha Polisi na kuomba kibali cha kuchinja, ambacho walipewa ilmradi wasiuze nyama hiyo.

hatimaye Wakrsito hao wakachinja na kuamua kupeleka kwenye bucha lao ambalo wamelitenga kwa ajili ya waumini wao kununua. Waislamu kuona hivyo, ndipo wakaenda kuripoti kituoi cha Polisi, na wakati Polisi (wachache) wanaongea na viongozi wa Kikristo eneo hilo ili kutatua na kurejesha amani, ndipo kundi la Waislamu likaja na kuanza kushambulia kilichokkuwa eneo hilo, wakivunja bucha, na pikipiki ya mkristo mmojawapo iliyokuwa eneo hilo.

Hatua hiyo imeelezwa kuibua hasia na kupelekea baadhi ya wat waliokuwa eneo hilo kuanza kujibu mashambulizi hayo, na mpaka hivi sasa inaripotiwa kuwa nguvu zaidi ya Jehi la Polisi haijafika eneo hilo, huku waumini wawili wa dini ya Kiislamu wakiwa katika hali mbaya kutokana na kipigo.

Silaha ni za jadi, na eneo hilo haliko salama kwa hivi sasa, kwani hata amduka mengine yamefungwa kuhofia usalama wa mali na maisha.

Akihojiwa na Beatrice Kamanga, katibu wa umoja wa makanisa ya Katoro na Buselesele, Mchungaji Silvanus Dominick, ameeleza kuwa kama hali haitatulizwa mara moja basi eneo hilo laweza kuleta madhara zaidi.

TAARIFA ZILIZOFIKA HIVI PUNDE:
Taarifa za hivi punde ni kuwa kuna Mchungaji ameuwawa kwa kushambuliwa na silaha mbalimbali ikiwemo mawe. Halikadhalika pia kuna msikiti ulichoma moto hapo awali.

- Gospel Kitaa -

Papa Benedict XVI atangaza rasmi kuachia madaraka.

Papa Benedict XVI
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict XVI ametangaza kuachia madaraka ya kuongoza kanisa ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, uamuzi ambao ni wa kwanza tangu karne ya 15 kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Habari la AFP.

Msemaji wa Papa, Federico Lombardi amesema kiongozi huyo wa juu kabisa wa Kanisa Katoliki duniani, ataachia ofisi rasmi tarehe 28 Februari, Mwaka huu saa mbili kamili asubuhi huku akiwa na Umri wa Miaka 85.

Wachambuzi mbalimbali wa masuala ya Vatican wanasema safari hii, kuna uwezekano mikoba ya Baba Mtakatifu Benedict XVI ikarithiwa na Kardinali kutoka Afrika.

Kardinali Peter Turkson wa Ghana ametajwa kama mrithi-mtarajiwa wa nafasi hii nyeti ndani ya Kanisa Katoliki, linalokadiriwa kuwa na waumini zaidi ya bilioni moja dunia nzima.

Mwingine ni Kardinali Francis Arinze; mzaliwa wa Nigeria ambaye alichukua nafasi ya Benedict XVI kama Kardinali-Askofu wa Velletri-Segni alipoteuliwa kuwa Papa miaka nane iliyopita.

- Mwananchi -

Saturday, February 2, 2013

Balozi wa Papa Nchini Tanzania ataka Hospitali ya Ndala kutoa Huduma Bora.



Askofu mkuu na balozi wa Papa hapa nchini Fracinsco Padilla akiwa na mkuu wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi wakikata utepe wa jengo la kutolea huduma ya Mama na Mtoto katika hospital ya Ndala - Tabora
ASKOFU Mkuu na Balozi wa Papa hapa nchini Askofu Fracinsco Padilla amesema kuwa Nchi ya Vatcan itafanya kila linalowezekana kuhakikisha hospitali ya Ndala iliyopo Mkoani Tabora wanaisaidia ili iweze kutoa huduma bora za afya kwa watanzania kwa miaka mingine 50 na kukabiliana na changamoto zilizopo kwa sasa katika hospitali hiyo.

Askofu Fracinsco Padilla alitoa Kauli hiyo baada ya kufungua majengo ya kutolea huduma kwa mama na watoto, pamoja na chumba cha upasuaji chenye vifaa vya kisasa ambavyo vyote vimegharimu jumla ya shilingi milioni 465.

Balozi huyo wa papa hapa nchini alisema kwamba huduma nzuri za afya kwa watanzania ndio kitu muhimu sana kwani bila afya hakuna amani, hakuna upendo na hakuna chochote ambacho wananchi wanaweza kupata kumbukumbu ya kuwepo kwake hospital hiyo hata baada ya miaka 50 ijayo.

Aidha aliwataka watoa huduma wote wa hospitali hiyo kufanya kazi kwa Moyo wa kujitolea kwa watanzania wote wanaofika katika hospitali hiyo kupata huduma ya matibabu ili kutimiza malengo ya Mungu kwa kutoa na kupokea.

Hata hivyo alisema kwamba hospitali ya Ndala kutimia miaka 50 ikiwa inaendela kutoa tiba kwa wananchi wa Tanzania, ni jambo zuri la kujivunia na la mafanikio makubwa sana kwa kanisa na waumini wake.

Awali Sista mkuu wa Hospitali hiyo Bernadette Kessy wakati akisoma risala kwa barozi wa papa nchini Askofu mkuu Fracinsco Padilla Kessy alisema kuwa mbali ya ukosefu huo wa fedha pia wanakabiliwa na ukosefu wa chumba chenye ukubwa wa kutosha kwa ajili ya kutolea huduma za maabara ya magonjwa ya binadamu.

Pia alisema kwamba hospitali hiyo inaukosefu wa gari la huduma kwa wagonjwa waliombali na hospitali gari ambalo hutumika kusarisha wagonjwa mahututi katika hospitali za rufaa.

Hata hivyo Sista Kessy alimweleza Balozi huyo wa Vatcan nchini kuwa pamoja na kuwepo kwa changamoto hizo lakini wameweza kuboresha miuondombinu ya majengo ya zamani na kuyafanya kuwa ya kisasa .

Aidha amebainisha kwamba mbali na kuboresha majengo hayo, wameanza kujenga majengo mengine manne mpya ambayo ni jengo la huduma ya upasuaji, jengo la huduma ya tiba kwa watu wanaoishi na VVU, jengo la huduma ya afya ya mama na mtoto pamoja na jengo la wodi ya wagonjwa wa kifua kikuu.

 Aidha hospitali hiyo inayomilikiwa na Kanisa Katoliki jimbo kuu la Tabora licha ya kutimiza miaka 50 tangu ianze kutoa huduma ya  afya kwa jamii mwaka 1963, bado inakabiliwa uhaba mkubwa wa fedha za kununulia madawa ya kutosha, vifaa tiba, vitendanishi na upungufu wa Watumishi wa kada zote.

Mahakama yazuia Kuapishwa kwa Mchungaji Kanisa la Moravian Dar.

Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi  wa Ilala, Duwani Nyanda akizungumza na viongozi  wa Kanisa la Moravian Jimbo la Misheni Mashariki
MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Ardhi Dar es Salaam, imetupilia mbali ombi  la  Bodi ya Wadhamini ya Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini, la kutaka kufunguliwa makufuli yaliyofungwa katika Kanisa la Usharika wa Tabata, ili waweze kumsimika mchungaji mpya, ambaye ni Lawi Mwankuga.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Mathew Mwaimu,baada ya bodi  hiyo ya wadhami wa Kanisa la Moravian Kusini chini ya Mchungaji Clement Mwaitebele, kupitia wakili wao, Henry Chaula wa Kampuni ya Uwakili ya C&M,  kufungua kesi namba 12  ya mwaka 2013 na kuomba isikilizwe chini ya  hati ya dharura.

Kwa mujibu wa kesi hiyo, Mchungaji Gervas Mwakafwila, Mchungaji Silas Mwakibinga, Tukuswiga Mwakabur, Atuganile Mbombo, Isakwisa Ernest  na Sekela Mukisele  ambao wanatetewa na Wakili Benjamin Mwakaganda wa Kampuni ya uwakili ya  BM,  wanadaiwa  kufunga makufuli kwenye  Kanisa la Usharika wa Tabata, ili kuzuia bodi hiyo  kumsimika mchungaji mpya.

Akitoa uamuzi, Jaji Mwaimu alikataa ombi la bodi hiyo  ya wadhamini la kutaka kufunguliwa kwa makufuli yaliyokuwa yamefungwa kwenye kanisa hilo, ili kupisha kumsimika mchungaji mpya.

Pia jaji huyo aliruhusu shughuli za kawaida za kanisani hapo kuendelea  na kusisitiza kwamba kilichozuiwa ni usimikaji wa mchungaji ili kuondoa uvunjifu wa amani.


Baada ya kutoa uamuzi huo, Jaji Mwaimu aliwataka wadaiwa  kupeleka kiapo pinzani mnamo  au kabla ya Februari 5, mwaka huu ambapo kesi hiyo imepangwa kusikilizwa.

Bodi hiyo ya wadhamini wa Kanisa la Moravian Jimbo la Rungwe  ni wadaiwa  namba 4 katika kesi namba 222 iliyofunguliwa mwaka 2012 katika Mahakama Kuu, ambayo inaendelea kusikilizwa Februari 6, mwaka huu mbele ya Jaji Augustini Mwarija.

Katika kesi hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Jimbo la Mashariki na Pwani ya Kanisa la Moravian Tanzania, Clement Fumbo na wenzake saba wanapinga kuondolewa madarakani na kusimamishwa kazi.

Katika kesi hiyo, Fumbo na wenzake hao saba wanaiomba Mahakama iamuru walipwe Sh500 milioni kama fidia na gharama ya kesi.

- Mwananchi -