Advertise Here

Wednesday, September 4, 2013

Hii ndiyo Safari ya Mwisho ya Askofu Dr. Mosses Kulola.

Mwili wa Marehemu ukiingizwa Kaburini
Leo ndo ilikuwa ndiyo siku ya Mwisho ya safari ya Askofu Dr. Mosses Kulola, safari iliyohitimishwa kwa Mwili wake kupumzishwa katika nyumba yake ya milele.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu likiwa Kaburini
Mazishi yake yamefanyika katika Kanisa la EAGT Bugando na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Makanisa mbaimbali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mh. Jakaya Mrisho Kikwete
Viongozi wengine waliokuwepo ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Engeneer Evarist Ndikilo, Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa, Katibu Mkuu wa CHADEMA Wilbroad Slaa, Mbunge wa Nyamagana(CHADEMA) Ezekiel Wenje.
Edward Lowasa akiweka shada la maua katika Kaburi la Marehemu
Pia Waimbaji mbalimbali wa Nyimbo za Injili Tanzania walikuwepo kuhakikisha kuwa zoezi zima linaambatana na Nyimbo mbalimbali za kumuenzi Baba/Babu yetu Askofu Dr. Mosses Kulola.
Mh. Jakaya Mrisho Kikwete
Sasa naomba nikukumbushe Wasifu wa Marehemu Askofu Dr. Mosses Kulola uliosomwa Jana katika Uwanja wa CCM Kirumba wakati wa kutoa heshima za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu.

Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa. Jina la Bwana libarikiwe.

Rais Jakaya Kikwete kushiriki Mazishi ya Askofu Dr. Mosses Kulola.

Rais Jakaya Kikwete
RAIS Jakaya Kikwete leo anatarajiwa kushiriki maziko ya Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT, Moses Kulola (86), aliyefariki Agosti 29, jijini Dar es Salaam. Maziko hayo yatafanyika katika Kanisa la EAGT Bugando, ambapo ibada ya maziko, inatarajiwa kuanza kati ya saa 3 na 4 asubuhi na maziko yatakuwa kati saa 4 na 7.30 mchana.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa Mwanza, Evarist Ndikilo, alisema Rais Kikwete anatarajiwa kuwasili leo, ambapo atashiriki maziko ya Askofu huyo na baada ya hapo, atakuwa na ziara ya wiki moja mkoani Mwanza.

“Atafanya ziara katika wilaya zote saba za mkoa wa Mwanza na atakagua shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanyika katika wilaya hizo,” alisema Ndikilo.

Alisema baadhi ya shughuli anazotarajiwa kuzifanya ni kuzindua miradi ya nishati, ukiwemo mradi wa MCC unaofadhiliwa na Wamarekani katika wilaya za Sengerema, Ilemela, Misungwi, Nyamagana na Magu.

Alisema wilayani Sengerema kuna maeneo 30 ya mradi huo, Misungwi maeneo mawili, Ilemela mawili, Nyamagana mawili na Magu eneo moja la mradi, ambapo mradi huo utazinduliwa katika eneo la Bukokwa wilayani Sengerema. Pia katika ziara hiyo, Rais atazindua mradi wa kufua umeme wa megawati 60 katika eneo la Nyakato jijini Mwanza.

Kwa upande wa biashara, Rais ataweka jiwe la msingi katika jengo la kitega uchumi cha biashara lililopo eneo la Ghana na kufungua hoteli ya Gold Crest. Ndikilo alisema kwa maeneo ya afya, atazindua zahanati ya Rugeye, maabara ya hospitali ya wilaya ya Ukerewe na mashine ya X- ray katika hospitali ya Misungwi, ambayo ni ahadi yake ya muda mrefu, itakayowasaidia wananchi wa wilaya.

Kwa upande wa elimu, atafungua shule ya msingi Itulya iliyojengwa kwa msaada wa shirika la Marekani yenye madarasa saba na kuweka jiwe la msingi katika jengo la ghorofa tatu kwa ajili ya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Magu. Aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi wakati Rais atakapokuwa kwenye ziara katika maeneo yao.

- Habari Leo -

Tuesday, September 3, 2013

Yaliyojiri katika kuuaga Mwili wa Askofu Dr. Mosses Kulola Uwanja wa CCM Kirumba.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Engeneer Evarist Ndikiro akitoa heshima za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu
Lilikuwa si jambo la kuamini kwa haraka kama kweli Askofu Dr. Mosses Kulola katutoka, lakini ilibidi kukubaliana na ukweli huo kwani wakati huu watu waliweza kuushuhudia mwili wa Marehemu Babu/Baba yetu ukiwa katika Jeneza.
Mwili wa Marehemu ukiwa Uwanja wa CCM Kirumba
Watu wengi sana walifurika Uwanja wa CCM Kirumba japokuwa leo ilikuwa ni Siku ya kazi. Kila alitamani ajionee kwa macho yake ili aamini ukweli uliopo ya kuwa hatuko tena na Askofu Dr. Mosses Kulola.
Mch. Dastan Mboya akieleza namna alivyomfahamu Askofu Mosses Kulola
Viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama mbalimbali na Viongozi mbalimbali wa Makanisa tofauti tofauti waliweza kufika Uwanja wa CCM Kirumba ili kutoa heshima zao za mwisho kwa Mwili wa Marehemu wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Engeener Evarist Ndikiro.
Ndugu wa Marehemu wakiwa Uwanjani
Maaskofu, Wachungaji na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Mwanza walifika Uwanjani hapo, pia alikuwepo Mwl. Christopher Mwakasege kutoka Mkoani Arusha akiongozana na baadhi ya wanahuduma wa MANA.
Umati wa watu
Zoezi la kutoa heshima za Mwisho lilianza mida ya Saa 2:30 Asubuh, na lilikamilika mida ya Saa 10 Jioni, huku watu wakipata fursa ya kusikiliza Wasifu wa Askofu Dr. Mosses Kulola pamoja na viongozi mbalimbali kutoa rambirambi zao pamoja maneno machache namna wanavyomfahamu Marehemu Askofu Mossas Kulola.
Bango lenye picha ya Marehemu Askofu dr. Mosses Kulola
Sikiliza hapa chini Neno la Mungu lililotolewa leo katika kuuaga mwili wa Marehemu Askofu Dr. Mosses Kulola

Na huu hapa chini ndio Wasifu wa Askofu Dr. Mosses Kulola uliotolewa na Ndugu Limbu katika Uwanja wa CCM Kirumba

Kauli ya Mwl. Christopher Mwakasege akiwa Uwanja wa CCM Kirumba wakati wa kuwasilisha Rambirambi kwa Familia ya Marehemu

Kauli ya Askofu Eugene Murisa wa Kanisa la High Way of Holliness Cathedral akitoa rambirambi kwa Familia ya Marehemu

Mwili wa Marehemu utazikwa kesho katika Kanisa la EAGT Bugando kuanzia mida ya Saa 2:00 Asubuhi. Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina lake libarikiwe.

Zoezi la kuaga Mwili wa Askofu Dr. Mosses Kulola linaendelea hivi sasa CCM Kirumba.

Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Askofu Dr. Mosses Kulola
Zoezi la Kuaga mwili wa Marehemu Askofu Dr. Mosses Kulola linaendelea hivi sasa katika Uwanja wa CCM Kirumba na Mwisho itakuwa ni Saa 10:00 Jioni, na hii ni kwa Mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya Askofu Dr. Mosses Kulola.

Mwili wa Marehemu utazikwa kesho Siku ya Jumatano September 4, 2013 katika Kanisa la EAGT Bugando.

Imetolewa na M/Kiti - Kamati ya Mazishi
0754 394337/0688 857629

Monday, September 2, 2013

Huu ndio Wimbo ulioimbwa na Watangazaji wa Radio za Kikristo Mwanza Maalum kwa Askofu Dr. Mosses kulola.

Baadhi ya Watangazaji wa Hhc Alive Fm. Kuanzia Kushoto ni Flora Robby, Adolph Nzwalla na Sowane Emmanuel
Sikiliza wimbo huu Unaoitwa "Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa" ulioimbwa na Watangazaji wa Radio za Kikristo Mwanza ukiwa ni maalumu kabisa kwa Mpendwa wetu Askofu Dr. Mosses Kulola. Baadhi ya Waimbaji walioshiriki ni Adolph Nzwalla (Hhc Alive Fm), Sowane Emmanuel (Hhc Alive Fm), Jackline Raphael (Kwa Neema Fm Radio), n.k