Advertise Here

Friday, November 1, 2013

Dalili za Mtu aliyechukuliwa Msukule.


Na: Mchungaji Mwangasa

Shetani yupo na anafanya kazi lakini watu wengine hawaamini kama shetani yupo. Mtu anaweza kuingiwa au kutupiwa mashetani asiweze kula wala kunywa. Pia mashetani yanaweza kumfanya mtu akonde na kuwa mwembamba.
 
Marko 9:18 “na kila ampagaapo, humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda; nikasema na wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze”.
Pepo anaweza kumwekea mtu kifafa,kutaliwa na laana. Marko 9:20 “Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini, akagaa-gaa, akitokwa na povu”.

Dalili za mtu aliyechukuliwa Msukule
1. Anaanza kuwatokea jamaa zake baada ya kufariki.Kuwa anaonekana mtu aliyekufa ni dalili ya watu wa familia kuwa na mashetani.

2. Baada ya kufariki anatokea mtu ndani ya familia anang’ang’ania  au kulazimisha mazishi yafanyike siku hiyo hiyo.

3. Baada ya mazishi, siku ya pili au ya tatu kaburi la marehemu huyo linaanza kutitia, hii ni kwa sababu mtu aliyechukuliwa msukule anakuwa bado ndani ya mwili.  

4. Marehemu anaonekana ama mrefu au mfupi sana zaidi ya kipimo cha mwanzo kipindi cha uhai wake. Hapa yawezekana wamepima gogo refu au fupi Ukiona vile Anza kuomba na kuita “Njoo kwa Jina la Yesu” 

5. Kifo cha ghafla. Binadamu ni kama gari jipya hivyo haiwezekani likawa jipya halafu likaharibika bila sababu,hivyo ni lazima augue. Hospitali wanaweza kusema amepata mshtuko wa moyo.Na roho ya kifo huwa inatumwa kwa muda inakaa ndani mwako wala siyo siku moja hivyo jifunze kufuta tarehe ya ya kifo kilichopangwa kwa Jina la Yesu.

6. Mgogoro kwenye familia baada ya msiba. Watu wengine wana macho ya rohoni,moyo unachoongea jua kipo.

7. Maneno ya marehemu wakati anakata roho. Mfano “hao wanakuja, hao wananichukua”. Haya maneno yana maana sana,maneno haya yazingatie hivyo ita mtu huyo aliyechukuliwa.

8. Maiti inabadilika sura. Wachawi wanaweza kumchukua mtu na kukuachia kitu. Mara baada ya kugundua kachukuliwa anza kuomba kwa Yesu na tumia maandiko.

9. Watu wanalazimisha kulia. Watu hao waweza kuwa ndugu au watu wengine kama vile majirani. Mfano mfiwa aweza kuambiwa “wewe umefiwa na mama halafu hulii?”. Nia yao ni wewe(mfiwa) ukiri kuwa ndugu yako kafariki. Ukiona hivyo kataa kukiri haraka kuwa mtu waka amekufa. Mfano Yesu alisema Lazaro hajafa bali amelala. Lengo la kulazimisha watu kulia ni kurahisisha mtu kuchukuliwa, mana wasipolia hawawezi kumchukua na kwenda naye.

10. Wanajitokeza watu wanazuia wachungaji(walokole) wasimwombee.Wanaweza kusema hiyo “siyo imani yetu” au “kaombee huko lakini siyo hapa”.
 
11. Wanandugu wanakataa watu wasiombe wakisema hata akirudi sisi kwetu ni uchuro.

12. Ndugu wa marehemu wanawaita na kuwapa dawa ili marehemu asije kukutokea tena.

Kwa hiyo ni muhimu inapotokea kuna kifo au tukio limetokea na kuna dalili zilizotajwa, ni vema kuliita Jina la Yesu.

- Ufufuo na Uzima -

Apostle Onesmo Ndegi ndani ya SAUT - Mwanza.

Kanisa ladaiwa kupokonya ardhi.

WANAKIJIJI zaidi ya 75 wa Kata ya Nyalikungu katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, wameulalamikia uongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga kwa kuwapokonya eneo lao la kilimo lenye ukubwa wa ekari 600.

Kwa mujibu wa nakala za mahakama, wanakijiji hao awali walifungua shauri la madai namba 6 la mwaka 2012 kudai eneo hilo na kushinda kesi hiyo lakini hadi sasa uongozi wa kanisa haujawakabidhi eneo hilo.

Hata hivyo baada ya wanakijiji kushinda kesi hiyo, kanisa nalo lilikata rufaa ambapo hukumu ilitolewa kuwa hakuna mshindi bali kinachohitajika ni maelewano baina ya pande hizo mbili.

Wanakijiji hao ambao waliwakilishwa na Charles Ndaha, ambaye katika shauri hilo alidai kuwa eneo lenye mgogoro kati yao na jimbo liko katika Kata ya Nyalikungu ambalo kanisa linadaiwa kuvamia kwa kujenga Shule ya Seminari ya Shanwa.

Kutokana na sintofahamu katika kesi hiyo, wanakijiji waliamua kukaa kikao cha pamoja kujadili hatima ya mashamba yao na kukubaliana kulifuatilia suala hilo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Mjumbe aliyehudhuria mkutano huo, Richard Masele, alisema tangu eneo hilo lichukuliwe na kanisa wanakijiji hawaruhusiwi kulima wala kukatisha.

Ofisa Ardhi wa Wilaya ya Maswa, Elikana Duda, alisema kwa njia ya simu kuwa wananchi wana haki ya kumiliki eneo hilo, kwamba tatizo ni kudanganywa kwa aliyekuwa Mkuu wa mkoa wakati wa kutoa vibali.

Alisema kesi ilisikilizwa na wananchi walishinda lakini suala hilo lilikuwa gumu, kwani baadaye waliliingiza kidini, licha ya wamiliki halali kujulikana kuwa ni wananchi.

- Tanzania Daima -

Ngeleja achangisha Milioni 260 Ujenzi wa Shule AICT Shinyanga.

Katibu Mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Mchungaji Yakobo Mapambano akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake
Hatimaye Uongozi wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga umetangaza Jumla ya fedha zilizopatikana katika harambee iliyoendeshwa na Mbunge wa Jimbo la Sengerema William Ngeleja kuhusu ujenzi wa shule ya sekondari ya Bishop Nkola inayomilikiwa na kanisa hilo.
Katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga, Mchungaji Yakobo Mapambano amewaambia waandishi wa habari kuwa  lengo lilikuwa ni kupata Milioni 350, na Jumla ya pesa katika changizo zilizopatikana mpaka sasa ni Shilingi Milioni 263, Laki 2, Elfu 4 na Mia tisa.
Katika harambee hiyo kanisa  lilipokea Michango kutoka kwa Prince Mobutu(Mtoto wa Rais wa zamani wa Zaire, Mobutu Seseseko), Askofu Mkuu wa AICT Nchini Kenya, Silas Yego, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Nasoro Rufunga, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja, Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele, Mbunge wa viti maalum Rachel Mashishanga na watu mbalimbali wenye mapenzi mema juu ya Jambo hili.

- Kadama Malunde (Shinyanga) -

Historia ya Mwimbaji Kabula George.

Kabula George
Nimezaliwa miaka 30 iliyopita katika kijiji cha Kimiza Wilayani Kwimba mkoa wa Mwanza. Masomo ya elimu shule ya msingi nilipata Kimiza  mkoani Mwanza na baada ya haapo niliendelea na masomo ya sekondari jijini Dar es Salaam.
 
Huduma ya uimbaji nilianza nikiwa mdogo nikiwa kanisa la Romani kabla ya kujiunga na kwaya ya Uinjilisti ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Tabata Kinyerezi.

Mwaka 2005 ndipo nilianza rasmi uimbaji kama solo artis na kufanikiwa kurekodi albamu yangu ya kwanza iliyojulikanaa kwa jina la AMANI. Hata hivyo albamu hiyo niliifanyia marekebisha na kuamua kuirudia nikachukua nyimbo kama Nkomoji ulioimbwa kwa lugha ya Kisukuma wenye maana ya kombozi. MileleTanzania na Tunakulilia.

Niliongezea nyimbo nyingine na kuipa jina jipya la Pesa iki ikiwa na nyimbo 9 kama, Milele, Pesa, Ninamjua, Nkomoji, Tanzania, Tunakulilia, Yatima, Nakupa utuku na
Niguse.

Mwaka 2009 nilifanikiwa kutoka na albamu yangu ya pili iliyojulikana kwa jina la ‘Ushindi’ ikiwa na nyimbo nane ambazo ni Ushindi, Hakuna muweza, Tunaishi kwa Neema, Yerusalemu, Nikikumbuka, Dhihirisha, Yesu Wasitahili na Mshukuruni Bwana.

Mwaka 2011 nilifanikiwa kurekodi albamu yangu ya tatu inayokwenda kwa jina la Nitang’ara Tu, ikiwa na nyimbo sita ambazo ni Nitang’ara tu, Majaribu, Nimesogea, Nataka kumuona Yesu, Ni Mwema na Peleleza ikiwa katika mfumo wa DVD na iko sokoni.

Mbali na uimbaji pia namtumikia Mungu katika huduma ya kuhubiri na nimekuwa nikisafiri katika nchi mbalimbali kwa ajili ya kuimba na kuhubiri. Nina abudu katika Huduma ya Neno la Upatanisho (WRM) iliyochini ya Nabii Nicolaus Suguye.

Albamu ya Nitang’ara tu nimeamua kuiboresha tena kwani nataka kurekodi video mpya na nitaongeza baadhi ya nyimbo.

Katika albamu hii nitachukua nyimbo kama Nitang’ara tu, Majaribu, Nimesogea na Nataka kumuona Yesu, kisha nitachukua wimbo wa Pesa kutoka albamu ya kwanza na tatu kutoka albamu ya pili iitwayo Ushindi. Nyimbo hizo ni Tunaishi kwa Neema, Yerusalemu na Dhihirisha.

Sikiliza Wimbo wake huu ujulikanao Kama "Pesa"
Wasiliana na Kabula George kwa Namba zifuatazo:
+255 658 140 336
+255 757 140 336
Facebook: Kabula George