Advertise Here

Monday, August 19, 2013

Semina ya kubwa ya "Majira ya Urejesho" yakamilika Mwanza.

Mwl. Wilhard Mwanri (Arusha)
ILE Semina kubwa ya Neno la Mungu iliyoanza Jumapili ya tarehe 11 mwezi huu, imekamilika siku ya Jana huku watu mbalimbali wakifunguliwa na kurejeshewa vile vitu ambavyo Ibilisi aliviiba kutoka kwao.
Mwl. Mwanri akiombea watu mbalimbali wakati wa Semina
Semina hiyo iliyodumu kwa Siku 8, ilifanyika maeneo ya Nyegezi, Tema Hotel Ukumbi Mkubwa, huku wanenaji wakiwa ni Mwl. Wilhard Mwanri kutoka Arusha na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la New Vine Christian Centre.
Watu wakifunguliwa

Wednesday, August 7, 2013

Askofu Kakobe akanusha uvumi wa kulikimbia Kanisa lake.

Askofu Zakary Kakobe
ASKOFU wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship amekanusha uvumi ulio tapakaa kwa Watanzania yakuwa amewakimbia wakristo wake na kuenda nchi za nje.

Alikanusha uvumi huo baada ya kuongoza mazishi ya aliyekuwa Askofu wa kanisa la Christian Love lililopo  Kiwalani, aliyefaliki tarehe 2 Agosti mwaka huu.

Mazishi ya mchungaji huyo yaliambatana na ibaada ambayo iliongozwa na Kakobe katika makaburi ya Kinondoni juzi. Kakobe alisema kuwa yeye hajaondoka nchini kama Watanzania wengi wanavyosema. 

"Sijaondoka na siwezi kuondoka kwasababu mimi ni wa hapahapa na nitazidi kuwa hapahapa, na tutabanana hapahapa, hakuna kwingine tena. Huwa natoka kihuduma tu na huwa narudi tena, na sio kuwa nimehama", alisema Kakobe

Kumekuwa na ukimya sana kwa Askofu huyo kitu kinachowashangaza wengi, kwani walishazoea kumuona akiongea kwenye vyombo vya habari mara kwa mara.
 
Mmoja wa wakristo wake alikili kuwa kwa sasa Askofu wao amepoteza umaarufu tofauti na zamani ndiyo maana watu wengi wanafikia uamuzi wa kufikiri hayupo nchini.

Kwaupande mwingine kinachoshangaza ni kwamba ujio wake katika msiba huo wa Askofu mwenzake ilikuwa ni safari ya kutokea nchi za nje ambapo aliingia nchini siku ya jumapili ya Agost 4 mwaka huu.

Saturday, June 15, 2013

Pastor Steven Wambura, James Kalekwa, Fred Msungu na Mc Pilipili wafanyika Baraka kwenye Kingdom Exploits.

Usiku wa Kuamkia leo katika Chuo cha Mt. Agustino-Mwanza, kulikuwa na Event iliyopewa Jina la Kingdom Exploits, iliyoandaliwa maalum kabisa kwa ajili ya Vijana waliopo chuoni hapo. Tukio hili lilianza Mida ya Saa 2:00 Usiku hadi Saa 5:00 Usiku huku Wanenaji wakiwa ni Bw. James Kalekwa-Mwanza, Fred Msungu-Dar na Mch. Steven Wambura-Dar.

Mchekeshaji wa Kimataifa toka Tanzania, Dar es salaam Bw. Emmanuel Mathias a.k.a Mc Pilipili alikuwepo Ukumbini hapo kuvunja mbavu za Wanafunzi wa Chuo hicho. Shughuli ilifanyika katika Ukumbi wa M10, na Praise Team iliyoundwa na Vijana wa Tafes, Casfeta, Huima na Uscf iliuongoza Umati wa Vijana waliokuwepo katika kuusogelea Uso wa Mungu.

Sasa tazama picha hizi uone jinsi Mambo yalivyokuwa chini ya Mc wa Event Bw. Barnabas Shija.
Mc wa Event Bw. Barnabas Shija
Wanafunzi waliohudhuria
Presentation ya Bw. James Kalekwa
Huyu jamaa hata kwenye Uimbaji yuko vizuri. Ni Fred Msungu

Wednesday, June 12, 2013

Leo ni Birthday ya Tb Joshua. Atimiza Miaka 50.

Tb Joshua
Jina lake kamili ni Temitope Balogun Joshua, jina alilopewa na Wazazi wake baada ya kuzaliwa. Anajulikana sana kama Tb Joshua. Alizaliwa mnamo June 12, 1963. Leo ametimiza Umri wa Miaka 50 toka Kuzaliwa kwake.

Kwa kawaida na ilivyozoeleka ni kwamba, Mama wajawazito hujifungua watoto baada ya Miezi 9 toka wapate ujauzito. Lakini kwa Mtumishi wa Mungu “Wise Man” Tb Joshua, haikuwa hivyo kwani yeye alizaliwa baada ya Miezi 15 toka Mama yake Mzazi apate ujauzito wake.
 
Na baada ya Miezi hiyo 14 (yaani Mwaka 1 na Miezi 2) kutimia, ndipo alipozaliwa mnamo June 12, 1963 katika Mji wa Arigidi, nchini Nigeria. Kwa sasa Mtumishi huyu anaishi katika Mji wa Lagos, Nigeria.

Tb Joshua ni Kiongozi na Mwanzilishi wa Huduma ya “The Synagogue, Church of All Nations(SCOAN)” inayoendesha Kituo cha Luninga kijulikanacho kama Emmanuel TV, kituo kinachopatikana kupitia satelaiti na kwenye Mtandao wa Internet.

Tb Joshua amekuwa akitoa Misaada mbalimbali kwa watu wasiojiweza, wajane, yatima, walemavu, kuwalipia ada wanafunzi mbalimbali, nk. Kwa kutambua hili, serikali ya Nigeria imekuwa ikimpa tuzo mbalimbali kwa ajili ya kutambua mchango wake katika ustawi wa hali ya kimaisha ya wananchi wa Nigeria.
Tb Joshua akitoa Msaada wa Chakula kwa Wazee wasiojiweza huko Nigeria
Katika hili la Msaada, amekuwa akisema; “Ili ubarikiwe, inatakiwa utumie sehemu kubwa ya Mali yako kwa ajili ya wenye uhitaji wa msaada(wajane, yatima, walemavu, nk), na utumie sehemu ndogo kwa ajili yako”.

Katika Kanisa analohudumu Tb Joshua nchini Nigeria, linahudumia takribani Waumini zaidi ya 15,000 katika Ibada za Kila Jumapili ambazo huwa zinarushwa moja kwa moja na Kituo cha Luninga cha “emmanuel tv”.