Advertise Here

Saturday, September 21, 2013

Dotnatha ajenga Kanisa lake.

Dotnatha
STAA wa sinema za Kitanzania,  Illuminatha Poshi ‘Dotnatha’ amejenga kanisa lake, Bomba Mbili, Ukonga nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo anatarajia kulizindua hivi karibuni baada ya kukamilisha vitu vyote muhimu.
 
Akizungumza na gazeti hili, Dotnatha alisema amekuwa haonekani mara kwa mara kutokana na  kutingwa na shughuli mbalimbali za ‘kulisimamisha’ kanisa hilo pamoja na kwenda shule kusomea taaluma ya  Biblia ili kujiweka katika nafasi muhimu ya kuongoza wanakondoo wa Bwana.
 
“Kanisa langu linakadiriwa kuchukuwa watu wapatao 2000 kwani ni kubwa na litakuwa likihudumiwa na wachungaji mbalimbali, ambao watakuwa wakipita kwa ajili ya kuongoza akiwemo Nabii Flora, ” alisema Dotnatha.
 
Hata hivyo, msanii huyo hakusita kutoa shukurani zake kwa muumba wa mbingu na nchi kwa kumuwezesha kutimiza ndoto zake za muda mrefu, bila kusahahu jitihada za mumewe, Mohamed Posh ambazo ni pamoja na ushauri wa karibu.

- Global Publishers -

Thursday, September 19, 2013

Diwani atajwa kuhusika na Uchomaji wa Kanisa nchini Kenya.


Stephen Chemalan ni mmoja wa waliotajwa na shahidi wa kwanza hiyo jana  katika kesi za ICC ya Uchomaji wa Kanisa la Kiambaa Nchini Kenya, lakini kwa wengi Chamalan hajulikani  licha ya kuwa yeye ni diwani  katika Kaunti ya Uasin Gishu.

Wednesday, September 18, 2013

Mwl. Christopher Mwakasege: Zijue Karama Za Roho Mtakatifu – I.

Mwl. Christopher Mwakasege

I Wakorintho 14:12. Inasema ‘vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za rohoni, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa. Mungu hafanyi kitu bila kusudi, na kusudi la semina hii ni:-

Kuna jambo Mungu anataka kufundisha katikati yetu ambalo litahusisha sana utendaji wa karama za Roho Mtakatifu.

 

Kurahisisha ujenzi wa kanisa lake na kazi zake. Mfano, kuna urahisi wa kujenga kwa kutumia mashine za kujengea na kubeba matofali kuliko kutumia mkono, ni sawa na kufanya kazi ya Mungu kwa kutumia karama za Roho Mtakatifu.
 

I Wakorintho 12:4; anasema pana tofauti za karama bali Roho ni yeye yule. Karama si za mtu ni za Roho Mtakatifu na kazi yake ni kulijenga kanisa.
Yesu alisema katika kitabu cha Mathayo 16:18; ”nitalijenga kanisa langu wala milango ya kuzimu haitaliweza”. Karama zinatokea mahali kama apendavyo Roho. Katika kitabu cha Yohana 14:16, Yesu alizungumza habari za kutuletea msaidizi mwingine, yaani Roho atakapokuja atachukua nafasi ya Yesu katika kulijenga kanisa lake.

Roho Mtakatifu sio karama bali anazo karama, pia Roho Mtakatifu sio nguvu bali anazo nguvu. Tunda la Roho linapofunuliwa ndani ya mtu tabia ya Mungu hujitokeza kwake.

Katika kutafuta vitu vya Mungu, ili kufahamu karama za Roho Mtakatifu na kazi zake, kuna gharama. Mfano, kwenye ndege kuna first class, business class na third class. Ukitaka kupata huduma nzuri zaidi lazima uongeze pesa (gharama) ili upande business class au first class. Lakini dereva wa ndege (captain) ni yule yule.

Vivyo hivyo katika maswala ya Mungu wako wanaokaa first, business au third class, lakini wote tunakwenda mbinguni. Hivyo tunahitaji kuingia gharama ili tukae first class ndani ya Yesu. Gharama hizo ni kama:-
i) kusoma neno la Mungu kwa bidii kwa kadri inavyowezekana ili neno hilo likae ndani yako kwa wingi, maan kujua karama za Roho Mtakatifu bila kuwa an maneno ya Mungu ni vigumu.
ii) Maombi n.k.

I Wakorintho 12:1 inasema ‘basi ndugu zangu kwa habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu’. Tunahitaji kuwa na hamu ya kuona kwamba karama za Roho Mtakatifu zinafanya kazi na zinafahamika. Hamu hiyo imepotea katika kanisa la Mungu na hivyo kufanya kazi ya ujenzi wa kanisa la Mungu kutofanyika kama Mungu anavyokusudia.

 

I Wakorintho 14:12; ”Vivyo hivyo na ninyi kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa”. 

 

UTENDAJI KAZI WA KARAMA
Mambo muhimu (ya msingi) kufahamu ili karama ziweze kufanya kazi. Mambo hayo ni:-
1.) Kubali kuwa karama za Roho zinaweza kufanya kazi kwako pia.

 

I Wakorintho 12:4.11; ”Basi pana tofauti za karama bali Roho ni yeye yule, lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye”.

 

Roho Mtakatifu ndani ya mtu anazo karama zote bali anamgawia kila mtu kama apendavyo yeye. Rumi 12:3-6; inasema ”kwa maana kwa neema niliyopewa na mwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyo mpasa kunia ……….., basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali …………..”.

 

Mkutano Mkubwa wa Injili Dar es salaam.

Tuesday, September 17, 2013

Operesheni "Kimbunga" yakamata wachungaji zaidi.

Ofisa Uhamiaji Mwandamizi, Julieth Sagamiko akimworodhesha raia wa Malawi na mtoto wake katika ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam jana ambako mamia ya wahamiaji haramu kutoka nchini humo walijitokeza kujiorodhesha ikiwa ni sehemu ya agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuwarejesha kwao wageni wasio na vibali. (Picha na Mroki Mroki).
Afisa Uhamiaji Mwandamizi, Julieth Sagamiko akimworodhesha Raia wa Malawi na Mtoto wake katika Ofisi ya Uhamiaji Dar es salaam
MSAKO wa wahamiaji haramu kupitia Operesheni Kimbunga inayoendelea nchini, umejikita kanisani kutokana na wahamiaji haramu sita wa Nigeria, kubainika wakijishughulisha na kazi za kichungaji.

Akizungumza jana kwa niaba ya Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Hokororo, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Sylvanus Mwakasekele, alisema wahamiaji hao walikuwa katika Kanisa la Praise la Tabata.

Kwa mujibu wa Mwakasekele, Uhamiaji walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu kuwapo kwa wahamiaji hao kwenye Kanisa hilo.

Baada ya taarifa hiyo, alisema maofisa Uhamiaji walifika kanisani hapo juzi saa tano asubuhi na watu hao walipogundua, waliruka madirishani kukwepa mkono wa sheria na kukimbia wakitumia gari dogo aina ya Toyota Vitz.

“Walipokimbia walikuwa sita, vijana waliokwenda kufanya kazi hiyo waliwafuatilia na walipoona wako hatarini kukamatwa walitelekeza gari na kukimbia kwa miguu na kukamatwa wanne huku wawili wakitoroka,” alisema Mwakasekele na kuongeza kuwa wako katika harakati za kusaka waliokimbia.

Aliwataja waliokamatwa na jinsi walivyoingia nchini, ni Moses Opara mwenye pasipoti namba A04809965, ambaye alikuwa kiongozi wa Kanisa hilo na ameishi nchini kwa miaka mitatu.

James Ateli mwenye pasipoti namba A04665804, aliyeingia nchini kama mfanyabiashara na kuishi kwa mwaka mmoja. Pia Keneth Onyebuchi aliyeingia nchini kama mfanyabiashara tangu Januari na kudai kupoteza pasipoti yake alipoingia nchini na mwingine ni Augustine Ndubilisi aliyeishi nchini mwaka mmoja.

“Huyu Augustine anadai anaishi na familia ya mchumba wake Mtanzania aliyetajwa kwa jina la Caro Mdegela, msichana huyu tunamshikilia kwa kuhifadhi wahamiaji haramu,” alisema.

Alisema baada ya kukamilika kwa mahojiano na watu hao, watafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuishi nchini bila kibali muda wowote kuanzia leo.

- Habari Leo -