James Kalekwa |
R -(Realistic). Lengo zuri lazima liwe na
uhalisia, ambao huja kutona na
kuangalia hali halisi ya pale ulipo, majukumu na nafasi yako. Mfano mzuri ni
huo hapo juu kwenye sifa ya kufikika. Unapoweka malengo juu ya jambo fulani
haimaanishi kwamba umeacha kufanya mambo mengine.
Unapoweka malengo ya kihuduma
haimaanishi kuwa umeacha kuwa baba au mama (kama Mungu amekupa watoto) kwahiyo
usijitoe kwenye wajibu mwingine uliopewa na Mungu, haimaanishi kwamba utastaafu
kuwa mme au mke (ikiwa umeoa kama mimi au umeolewa), haimaanishi kwamba wewe si
mtoto wa wazazi wako (ikiwa bado wa hai) kwahiyo unawajibu huo.
Lakini jambo
jingine la msingi kufahamu, ni je, utapata muda wa kutathmini kazi yako au
unaenda kienyeji kienyeji tu, Je, utapata muda wa kufuatilia mavuno hayo
na kuyaombea au kuyalea (hakuna umuhimu wa kuzaa kama huwezi kulea), Je kuna
mafundisho ya kutosha kwa watu hao? Lazima uzingatie kanuni ya kuwa mkweli juu
ya nafsi yako?
Watoto wengine wa Mungu wamekwama sehemu si kwasababu hawana
Yesu. Yesu wanae, Roho Mtakatifu yupo pamoja nao na wanaenda mbinguni lakini
wamekwama sehemu kwasababu hawana maarifa juu ya jambo hilo. Mtumishi mmoja wa
Mungu aliandika, "Upako unaletwa na maombi lakini maarifa ya neno
huja kwa kusoma.
Maombi kamwe hayawezi kufuta ujinga na kukupa
maarifa. Neno la Mungu limeweka bayana kuwa watu wanaangamizwa kwa kukosa
maarifa Hosea 4:6. Ina maana upako siyo tiketi ya kukuzuia kuangamizwa kama
huna maarifa ya neno la Mungu."
T -(Time bound). Kitu cha kuzingatia
katika kuweka malengo ni swala la muda, yaani tamati ya malengo husika. Hii
itasakusaidia sana kupima mafanikio na kuweza kufanya tathmini juu ya maendeleo
wakati wote wa utekelezaji wa malengo husika. Hebu fikiria nini kilimfanya
Bwana Yesu aseme “…hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.", kwasababu
malengo yake yalikuwa yamefungwa katika muda wa kuyakamilisha, alikuwa anaujua
mwisho tangu mwanzo, kama ni msafiri basi alikuwa anajua stendi au kituo cha
mwisho cha safari yake.
Hebu jiulize nini kinaweza kutokea kama malengo yako
hayatakuwa na muda wa kuyaona yakitimilika, ”time of their realization.”?.
Ngoja nikupe mfano wa kawaida sana ndipo utaelewa nini ninamaanisha, hebu
fikiri pamoja na mimi itakuwaje kama mwanafunzi wa darasa la tano akibakia
darasa hilo siku zote, bila kuhitimu wala kwenda darasa jingine, siku zote ni
darasa la tano?
Ingefika wakati mwanafunzi huyu angechoka na masomo kwasababu
hayana mwisho, lakini pia mzazi wake pia angechoka kulipia gharama za kitu
kisicho na ukomo au utimilifu. Maana yangu hapa ni kwamba kinachomfanya
mwanafunzi wa darasa la tano asome kwa bidii ni kwasababu kuna darasa la sita
mbele na la saba yaani kuna kipindi cha kuhitimu hatua husika ya masomo la
sivyo asingesoma kwa bidii.
Hebu fikiri nini kitatokea kama inatokea wanawake
wanakuwa wajawazito siku zote, bila mwisho!!! Najua wengine wasingetamani kuwa
na hali hiyo, kwasababu hakuna kuhitimu hali hiyo, yaani kujifungua.
Mfano wa
lengo ambalo ni SMART: Kuihubiri injili kwa watu 1000 nchini Tanzania katika
wilaya 4 kwa mwaka mmoja.
Je, lengo
hilo ni hususani (Specific)? Ndiyo kwasababu limetaja idadi ya watu,idadi ya
wilaya na nchi.
Je, lengo
hilo Linapimika (Measurable)? Ndiyo kwasababu ya idadi, eneo la kijiografia
(mahali) yaani mwisho wa siku unaweza kukaa chini na kuangalia kama wilaya 4
zimefikiwa na kwa kiasi gani, vilevile kuona kama watu 100 wamefikiwa.
Je, lengo
hilo linafikika (Attainable)? Ndiyo, kwa Jiografia ya Tanzania inawezekana
kuzifikia wilaya hizo kwa muda huo. Pia unaweza kupata muda wa kujiandaa, kifedha,
kimaombi, ujumbe kwani mwalimu mzuri ni mwanafunzi wa kudumu, kwahiyo lazima
ujifunze ili ukafundishe.
Je,lengo
hilo linauhalisia (Realistic)? Ndiyo, kwasababu
muda unaruhusu kufanya mambo mengine kama maandalizi ya uwanja/ukumbi wa
mikutano, mahali pa kufikia, watu wa kushirikiana nao (si unajua huwezi
kushirikiana na watu wote na kwa upande mwingine huwezi kushirikiana na
kila mtu?) n.k yaani kwa lugha ya kiingereza wanaita "logistics",
pia unaweza kuwa na muda wa kutimiza wajibu wako mwingine kama baba/mama
(mzazi), kama mme/mke, kama mtoto na vitu vya msingi kama hivyo lakini pia kuna
jambo la muhimu ambalo watu wengi hulipuuzia,lakini ni la muhimu
sana.
MAPUMZIKO! Mungu baada ya kutenda kazi siku sita alipumzika! Umuhimu wa
kupumzika ni kwamba unaporudi tena kwenye utekelezaji, unakuja na nguvu mpya
"fresh". Mungu akusaidie
kuyaelewa haya na kuyatendea kazi na maisha yako hayatakuwa kama yalivyo, na
hayo ndiyo maombi yangu kwa Mungu kwaajili yako msomaji wangu.
Somo litaendelea Jumatatu Ijayo.....
Mafundisho haya yameandaliwa na James Kalekwa
Mwanataaluma, Mwandishi wa vitabu na Mwalimu wa Neno la Mungu
+255 714 762 669
+255 754 917 764