Sunday, September 30, 2012
Mwl. Christopher Mwakasege: Mambo ya Msingi ya Kutafakari kabla ya kufanya Uamuzi wa Kuoa/Kuolewa - VIII.
Mwl. Christopher Mwakasege: Mambo ya Msingi ya Kutafakari kabla ya kufanya Uamuzi wa Kuoa/Kuolewa - VII.
Je! Uko tayari kuoa au kuolewa?
Akasema, “ninaomba ruhusa”. Nikwamwambia, “kwa nini unaona ni rahisi kuomba ruhusa kwa mwajiri wako na unaona taabu kuomba ruhusa kwa mume wako?” Alishindwa kujibu hilo swali.
Mwl. Christopher Mwakasege: Mambo ya Msingi ya Kutafakari kabla ya kufanya Uamuzi wa Kuoa/Kuolewa - VI.
Uamuzi wa kuoa au kuolewa unaweza wakati mwingine
kukuletea marafiki au maadui.
Tuesday, September 25, 2012
Mwl. Christopher Mwakasege: Mambo ya Msingi ya Kutafakari kabla ya kufanya Uamuzi wa Kuoa/Kuolewa - V.
Uamuzi wa kuoa au kuolewa, unaweza ukabadilisha
utumishi wako na wito wako kabisa
Monday, September 24, 2012
Mwl. Christopher Mwakasege: Mambo ya Msingi ya Kutafakari kabla ya kufanya Uamuzi wa Kuoa/Kuolewa - IV.
kwa sababu utakufanya uwajibike zaidi.
Monday, September 17, 2012
Mwl. Christopher Mwakasege: Mambo ya Msingi ya Kutafakari kabla ya kufanya Uamuzi wa Kuoa/Kuolewa - III.
JAMBO LA TATU
Ukiamua kuoa au kuolewa, wakati mwingine
imani yako inaweza ikabadilika.
Wasomaji wa biblia wanamfahamu mtu mmoja aliyeitwa mfalme Sulemani (unafahamu ni kwa nini aliandika kitabu cha Mhubiri, maana alipoandika kitabu cha Mhubiri akasema, mambo yote chini ya jua ni ubatili mtupu). Biblia inatuambia wazi kabisa ya kuwa Mungu alimpa hekima ya ajabu, na wasichana wakatoka sehemu mbali mbali duniani kwenda kufuatilia ile hekima, walipoikuta hawakutaka kuondoka na wakabaki pale kwake.
Kosa alilofanya Sulemani ni kwamba wale wasichana walikuwa wanakuja na miungu yao, na alikuwa anawakaribisha wale wasichana na miungu yao, anawapa na mahali pa kujengea vibanda vya miungu yao. Biblia inatuambia wazi kabisa, ilifika mahali wale wakina mama wakamgeuza moyo wake usiendelee kumpenda Bwana.
Kitabu cha 1 Wafalme 11:4 kinasema hivi: “Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa BWANA Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake.”
Nimeona vijana wengi sana ambao wanakuwa moto sana kwenye wokovu kabla hawajaolewa au kuoa, wewe ngoja waingie kwenye ndoa na wafuatilie baada ya muda, utakuta wengine wamepoa mpaka wameganda kama barafu! Ukiwauliza ni nini kimewafanya wapoe kiroho kwa kiwango hicho – wanaweza wakashindwa kusema. Maana kuna watu wengine wanafikiri ni kuolewa tu na mtu yoyote kwa sababu tu anasema Bwana asifiwe, ibilisi Pia huwa anaweka na watu wa kwake huko ndani ya makundi ya watu waliookoka.
Na ukikaa na vijana utapata baadhi yao wanaosema, ukitaka kupata vijana waaminifu siku hizi nenda katikati ya waliokoka, kwa hiyo wanajifanya wameokoka. Akikufuatilia juu ya kuoana na ukimwambia mbona wewe hujaokoka, na ukamtaka kwanza aokoke ndipo mzungumze, utakuta baada ya siku chache kupita anajifanya ameokoka, lakini ni yakubabaisha tu ili akupate. Nimekutana na watu wa namna hiyo, msichana anaolewa akishafika ndani, ndio kijana anamwambia, na Yesu wako na wokovu wako nauvua hapa hapa, mimi nilikuwa nakutafuta wewe, nimekupata basi!
Nimeona! Sisemi kitu cha hadithi, ninasema kitu ambacho nimeona kwa macho. Ikiwa umefika katika hali hii basi, ni mpaka kifo kiwatenganishe, na alikwishawaambia wenzake kwamba Mungu amenifunulia; kwa hiyo hana ujasiri wa kurudi na kusema kweli nilikuwa nimekosea, yalikuwa ni mafuniko sio mafunuo! Akitaka kwenda kwenye maombi anaambiwa hakuna; akitaka kwenda kuhudumu anaambiwa hakuna; anataka kwenda ‘fellowship’, anaambiwa hakuna; kaa hapo ndani. Kwa hiyo inabaki kazi moja tu ya kuombea chakula na chai na kwenda kulala!
Na ni kwa sababu huyu mtu hakufikiri sawasawa, hakukaa akaona jinsi ambavyo hili jambo linaweza likambadilishia imani yake kabisa. Wewe nenda kwenye maandiko, utaona ya kuwa ndoa inaweza ikakubadilisha. Ndio maana kuna watu wengine wanaolewa, na wengine wanaoa na wanabadilisha dini, hii sio kitu cha mchezo, ni maamuzi magumu sana kuyafanya.
Unapobadilisha imani yako unabadilisha msingi wako kabisa wa maisha yako; kwa hiyo ni lazima uamue jambo ya kuoa au kuolewa kwa uangalifu sana.
Lakini pia inaweza ikawa ni mkristo kwa mkristo wanataka kuoana, lakini fahamu kuoa au kuolewa kunaweza kukakubadilisha dhehebu lako la kikristo, ndio maana lazima mkubaliane juu ya jambo hili kabla ya kuingia kwenye ndoa. Nilikuta vijana wamekubaliana kuoana, kijana mmoja mlutheri, kijana mwingine mpentekoste. Mambo yakawa magumu sana kwao, walipofika masuala ya kujadiliana, juu ya imani zao. Ilikuwa ngumu sana, mpaka wachungaji wao wakaingilia kati.
Walipokuja kuniona, nikawauliza mko tayari kabisa na mnataka kuoana? Wakasema, ndio. Wakati huo walipokuja kwangu walikuwa tayari wameshaenda nyumbani kwao, wameshazungumza na wazazi wao, na kote huko na wakati wote huo hawakufikiria hilo jambo. Sasa imefika mahali mchungaji wa kanisa hilo la pentekoste hakubali msichana wake aolewe kwa kijana wa kilutheri. Nikamuuliza maswali yule msichana akashindwa kujibu.
Unajua wapentekoste hawabatizi watoto, walutheri wanabatiza watoto. Mnapooana matokeo yake ni kwamba watoto watazaliwa. Ni lazima hicho kitu ufikiri kabla hajasema ndio kuolewa, au ndio kuoa. Sio umekwisha olewa ndipo unasema watoto wangu hawawezi kwenda huko, – ulikuwa wapi toka mapema ili uliseme hili tatizo? Maana unaweza ukafikiri ni masuala marahisi, sio masuala marahisi.
Maana wengine wanalichukulia jambo hili kirahisi, wakati jambo lenyewe sio rahisi. Masuala ya kwenda kusali kanisa tofauti tofauti huku mmeoana sio mambo rahisi. Nimeona watu wakisema hakuna tatizo maana tutaoana, lakini kila mtu wetu atakuwa anakwenda kanisani kivyake; sawa, ninyi mnaweza mkaenda kivyenu, na watoto je? Labda kama hamna mpango wa kuzaa!
Maana niliona kwenye TV, mtu mmoja, – dada mmoja huko ulaya amefuga mbwa akasema, tuliamua huku ndani tusizae watoto na badala yake tumefuga mbwa badala ya mtoto, wamempa na jina, wamempa na chumba wamempa na kitanda, anasahani yake, na bajeti yake, ana daktari, wameamua wasizae na badala yake, wamefuga mbwa! Labda kama unataka kuelekea njia hiyo! Lakini kama unaingia kwenye ndoa na unajua utakwenda kupata mtoto, suala la mahali mnapokwenda kusali ni muhimu sana kulijadili na kuliamua kabla ya kuingia kwenye ndoa.
Usiende kupeleka vita kwenye ndoa yako ambayo haitakiwi kuwepo! Unajua kuna vita vingine tunavianzisha bila sababu, hata Yesu alijua, wakati saa yake ya kupigwa mawe ilipokuwa haijafika, alikuwa anawakwepa wale watu waliokuwa wamepanga kumpiga mawe. Sasa kama Yesu alikuwa anakwepa majaribu mengine kwa nini wewe unajitumbukiza? Saa ikifika ya jaribu kuja kwako utalishinda tu, kwa sababu umetengenezwa na Mungu uwe na uhakika wa ushindi, kwa sababu ukiwa ndani ya Kristo unashinda na zaidi ya kushinda.
Imeandikwa hivi katika kitabu cha Warumi 8:37; “Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda”. Lakini majaribu ya kujitafutia, yanaweza yakayumbisha imani yako.
Maana watu wengi sana huwa hawajiulizi hili swali mapema lakini nimeona likiwapa shida. Wengine hata imefika saa ya kufunga ndoa, ndio kwanza wanaanza kujiuliza, ‘ndoa sasa tunakwenda kufungia wapi’, hilo sio swali la kujiuliza saa hiyo, utakuwa umechelewa! Wewe ulikuwa unajua kabisa mwenzako anasali mahali fulani, na wewe unasali mahali pengine, imefika saa mnataka kufunga ndoa mnaanza kujiuliza, tukafunge ndoa kwenye kanisa la nani, ikiishafika hapo mnaanza kushindana na kuvutana; na haifai mambo kuwa hivyo.
Somo hili bado linaendelea. Usikose sehemu ya Nne ya somo hili Siku ya Jumapili.
Sunday, September 16, 2012
Kibaka Aokoka, Asema Atawashawishi Wenzake Pia Waokoke .
Aliongeza kwa kusema kuwa, “Katika kipindi chote hiki nimekuwa nikishuhudia watu ninaokutana nao njiani wakiniangalia kwa hofu, jambo ambalo lilinifanya nijisikie kutokubalika na jamii na hivyo nikikumbuka vifo vya wenzangu nilipata picha kuwa ipo siku nami nitauawa kama hao hivyo kuamua kuokoka na kuacha tabia hiyo ili niwe raia mwema.”
Mwl. Christopher Mwakasege: Mambo ya Msingi ya Kutafakari kabla ya kufanya Uamuzi wa Kuoa/Kuolewa - II.
JAMBO LA PILI.
Unapoamua kuoa au kuolewa, fahamu ya kwamba hiyo ndoa
inakuunganisha na kukuingiza katika familia nyingine.
Unafahamu watu wengi sana wakioa au kuolewa wanafikiria tu mahusiano ya wao wenyewe tu; na hii ni hatari sana. Kwa sababu unapooa unaingia kwenye undugu na familia nyingine kabisa tofauti, na sio mahusiano ya kwenu tu wawili. Ninyi ni kigezo tu cha kuunganisha hizo familia mbili, lakini mkiishaoana hizo familia zenu mbili ni ndugu kuanzia wakati huo.
Ndio maana unapofika unataka kuoa au kuolewa, sio suala la kumtazama kijana tu, au kumtazama msichana yeye mwenyewe tu; kwa mfano alivyosoma, lakini ni lazima pia utazame na hali ya familia yake ili ujue unajiingiza kwenye familia ya namna gani. Unapofika kwenye masuala ya namna hiyo kuna vitu vingi sana vya kuangalia.
Unaweza ukaingia kwenye familia ambayo ni wavivu, mimi ninakuambia jasho litakutoka ukioa msichana wa namna hiyo; au ukipata kijana toka kwenye familia ya namna hiyo. Itakuwa kazi sana kumshawishi mwenzako juu ya kujishughulisha na maisha. Maana inategemea; kwa kuwa unaweza kuoa msichana hata kusonga ugali hajui. Sisi kwenye nyumba ya baba yetu, hatuna msichana, tumezaliwa watoto wa kiume watupu, msichana wa kwanza kuingia kwenye familia yetu ni mke wangu.
Lakini mama yetu alikuwa na bidii ya kutufundisha kila kitu, alitufundisha kupika, alitufundisha kufuma, alitufundisha kusuka nywele. Kwa hiyo nilijifunza kwanza kusuka tatu kichwa. Lakini sikuanzia kujifunzia kusuka nywele kwenye kichwa cha mtu, bali nilijifunzia kwenye majani; wao wakikaa wanasuka hapo na sisi tuko hapo tunafundishwa jinsi ya kusuka kwenye majani.
Sasa wengine hawapati nafasi ya namna hiyo, na ni mbaya zaidi kwa wasichana. Mungu amenipa nafasi ya kuwa na watoto wakike watatu na wa kiume mmoja, itakuwa ni aibu kwetu kama wazazi, ikafika wakati wanaingia katika ndoa zao na hawajui kupika ni aibu; kwa hiyo lazima wajue kupika. Maana kwa kujua hilo anaonyesha anatoka familia ya namna gani, na imemlea kwa namna gani!
Unaweza ukafikiri unamlea mtoto wako vizuri, maana siku hizi kuna shida ya kuwa na wafanya kazi majumbani mwetu. Ukishakuwa na mfanyakazi nyumbani basi watoto wengine hawafanyi kitu, wakati mwingine wanakula chakula na wanaacha sahani hapo hapo mezani.
Kuna watoto wengine inakuwa mpaka yuko sekondari hawezi kufua nguo zake. Kwa kuwa nyumbani kama hakuna wa kumfulia basi kuna mashine za kufulia. Huko unakokwenda kuolewa inawezekana hata mashine ya kufulia hawajawahi kuiona! Unafika pale na unauliza mashine iko wapi, wanakuambia yakufanyia nini, – ya kusagia mahindi? Maana ndio wanayoijua kuwa ndio mashine!
Hujui hata namna ya kushika kioo cha taa ya chemli wala namna ya kuiosha kule ndani lile vumbi likaondoka. Inawezekana mwingine umezaliwa kwenye nyumba yenye umeme, lakini utakapokuwa katika ndoa unaenda kwenye nyumba ambayo haina hata umeme, unafika kule na unashangaa kweli maana hujui hata namna kuwasha taa ya chemli! Kwa hiyo tunawaambia watoto wetu suala la kujifunza hivi vitu sio suala la kuchagua, hata kama kuna mtu pale nyumbani wa kuwasaidia, ni lazima wajue kufanya kazi!
Nilienda kwenye mkoa mmoja wakasema, sisi ukitaka kuoa kwenye nyumba ya mtu, ukitaka kujua huyo msichana amelelewa vizuri au vibaya wakasema usimtazame alivyovaa. Badala yake wanafika kwenye uwanja wa nyumba ya wazazi wake, na wanaangalia ile barabara inayokwenda nyumbani kwao, na wakiikuta chafu, basi wanajua huyu msichana ni mchafu, hawahangaiki tena kuja kuzungumza, wanajua hapa kama tunaamua kuoa tujue tunacho oa, huyu msichana ni mchafu!
Ukienda kuoa kwenye familia nyingine utakuta wanasumbuliwa na ugonjwa wa kurithi, na usipojua kitu cha kufanya unaweza ukapata shida sana. Lakini ninachotaka kukuambia ni kwamba, uamuzi wa kuoa au kuolewa unakuingiza kwenye familia nyingine kabisa, na inaunganisha hiyo familia yao na familia yako; kwa hiyo hayo sio maamuzi madogo. Kumbuka unapooa au kuolewa unawaingiza watu katika famila ambazo kama usipokuwa mwangalifu inaweza ikaleta shida sana, lakini pia inaweza ikaleta baraka!.
Somo hili bado linaendelea. Usikose sehemu ya Tatu ya somo hili hapo kesho.
Saturday, September 15, 2012
Mwl. Christopher Mwakasege: Mambo ya Msingi ya Kutafakari kabla ya kufanya Uamuzi wa Kuoa/Kuolewa - I.
JAMBO LA KWANZA
Kuoa au kuolewa kunabadilisha uhusiano
wako na wazazi wako.
Mwanzo.2:24 anasema, “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili moja”. Ukiangalia (Zaburi.45:10-11) anasema, “Sikia binti utazame (maana yake anazungumza na msichana) utege sikio lako. Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako na mfalme atautamani uzuri wako, maana ndiye bwana wako naye umsujudie”.
Najua watu wengi sana wanataka waingie kwenye ndoa, waoe au waolewe, lakini uhusiano wao na wazazi wao usibadilike, haiwezekani. Biblia imeweka wazi kabisa, unataka kuoa, mwanamume lazima kwanza aachane na baba yake na mama yake, maana yake kuna mabadiliko. Kuna mabadiliko mahali pakuishi, kuna mabadiliko juu ya mtazamo wako wa kwanza wa maisha yako. Mke wako hawezi kuwa mama yako, na mume wako hawezi kuwa baba yako. Mke wako anakuwa mke wako na si mama yako. Mume wako anakuwa mume wako na si baba yako.
Na kabla hujafikia maamuzi ya namna hiyo – ukiingia kwenye ndoa, ndoa yako itakuwa ngumu. Maana inawezekana unaishi vizuri na wazazi wako, kiasi ambacho maamuzi yako yoyote unayofanya lazima ushirikiane nao, na hiyo ni hatua nzuri kabisa. Lakini ukiishaingia kwenye ndoa, mtu wa kwanza wakushirikiana naye ni mke wako kama umeoa, na ni mume wako kama umeolewa lakini, sio baba yako, sio mama yako.
Na wazazi wengine wasingetaka kuona kwamba unakuwa mbali nao kwa jinsi hii, wanataka waendeleze maamuzi yao na utawala wao waliokuwa nao juu yako mpaka kwenye ndoa yako, haiwezekani. Biblia inakataa. Sasa ukisoma ile Mwanzo unaweza ukafikiri ni wanaume tu wakioa ndio wanatakiwa watoke, waachane na wazazi wao, lakini Zaburi 45:10,11 inatuambia wazi kabisa, inasema, “Sikia, binti, utazame, utege sikio lako, Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako. Naye Mfalme atautamani uzuri wako, Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie”.
Sasa haimaanishi usiwasalimie, haimanishi usiwasaidie, lakini ningekuwa nazungumza kwa kiingereza ningekuambia, “your priorities must change” lazima ubadilike jinsi ambavyo unaweka kipaumbele katika watu ulio nao.
Unapoamua kuolewa, wa kwanza sio baba yako wala sio mama yako, wa kwanza ni mume wako baada ya Yesu. Katika mahusiano ya kibinadamu anayekuja pale wa kwanza baada ya Yesu moyoni mwako ni mume wako. Ikiwa hujafikia maamuzi ya namna hii moyoni mwako basi bado hujafikia utayari wa kuolewa. Na ina madhara yake magumu. Maana biblia inasema, kabla hujawasahau watu wako na watu wa nyumba ya baba yako, mume wako hawezi kuutamani uzuri wako, ukitaka autamani uzuri wako lazima uwasahau kwanza watu wa nyumbani kwa wazazi wako.
Sasa kuna tofauti ya kupenda na kutamani. Kabla hujaolewa au kabla hujaoa huruhusiwi kutamani. Lakini ukiisha oa unaruhusiwa kutamani lakini mke wako tu. Ukiishaoa kutamani mke wako ruksa, na biblia imeweka vizuri kabisa, na ukiishaolewa kutamani mume wako ni ruksa. Lakini biblia imeweka utaratibu wa ajabu sana kwamba, ili mume amtamani mke wake, lazima mke wake awasahau kwanza watu wa nyumbani mwa wazazi wake. Hiki ni kigezo kigumu sana.
Ndio maana unaweza ukakuta mtu ana mke mzuri sana lakini hamtamani. Unaweza ukafikiri labda ni kwa kuwa hajajipamba vizuri; lakini hata kama atajipamba, atajikwatua kuanzia asubuhi mpaka jioni, – anaweza hata akatumia muda mwingi kwenye kioo kuliko kwenye maombi akijitengeneza, lakini bado mume wake asimtamani; kwa nini? Kwa sababu ndani yake hajaachia watu wa nyumba ya wazazi wake. Au watu wa nyumba ya baba yake wana nafasi kubwa moyoni kuliko mume wake.
Ni mabadiliko ambayo lazima uyatarajie, watu wengi sana huwa hawafikirii hayo, wanafikiri ni kitu rahisi. Unaweza sasa ukaelewa kwa nini watu wengine ikifika siku ile ya “send off”, yaani ya kum’send’ msichana ‘off’ asikae tena nyumbani kwa baba yake, hiyo siku ni ngumu sana kwa wazazi. Kwa sababu wanajua, wanaagana na msichana wao, mahusiano yao waliokuwa nayo toka mwanzoni, tangu alipozaliwa, alipokuwa tumboni mpaka wakati huo yanabadilishwa, yanajengwa mengine, sasa anakwenda kuwa mke wa mtu, hawawezi tena kuingilia maamuzi juu yake, amefunga agano mahali pengine.
Unakuta siku hiyo wazazi wengine wanalia, unakuta vijana wengine wanalia, wasichana wengine wanalia. Usije ukafikiri ni kitu rahisi. Ndani ya nafsi kuna vitu vinaachana, kati ya wazazi na wale watoto wanaoana.
Somo hili bado linaendelea. Usikose sehemu ya Pili ya somo hili hapo kesho.
Friday, September 14, 2012
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Benedict XVI ziarani nchini Lebanon.
Miaka kumi na tano baada ya ziara ya mtangulizi wake Papa John Paul II ambaye alitoa ujumbe wa amani katika nchi hiyo yenye asilimia 35 ya wakristo na 64.6 ya waislam. Benedict wa kumi na sita atatoa ujumbe kwa waumini hao waliugawanyika kisiasa na msimamo kuhusu vita vya nchini Syria.
Papa Benedict ambae anazuru nchi hiyo katika kipindi kigumu, anatakiwa kuwatia moyo wa kristo baada ya kuongeza kwa makundi ya kiislam na kuomba kusitishwa kwa machafuko nchini Syria.
Barabara nyingi za mji mkuu Beyrouth zimefungwa kwa ajili ya kuimarisha usalama, ambapo viongozi wamethibitisha kuwa vyombo vya usalama vimehamasishwa kuhakikisha usalama unaimarishwa na kuhakikisha kuwa ziara hiyo ya kiongozi wa kanisa Katoliki inafana.
Akiwa Lebanon Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki atahudhuria mkutano wa vijana ambao utawaleta pamoja waislam na wakristo ambapo Kiongozi huyo atahitimisha shughuli zake siku ya jumapili kwa kuongoza misa huko Beirut na inatazamiwa kuhudhuriwa na waumini elfu sabini na tano.
Wednesday, September 12, 2012
Yanayojili pale EAGT Lumala Mpya katika Kongamano la OYES.
Mwalimu Mrs. Kihoza akifundisha somo la Ujasiriamali |
Mrs. Kihoza akiendelea na Somo |
Sehemu ya watu waliohudhuria Kongamano hili siku ya leo |
Kongamano bado linaendelea kila siku Kuanzia saa 8:30 Mchana mpaka saa 12:30 Jioni. Mwisho wa Kongamano hili ni Siku ya Jumapili. Usikose kuhudhuria Kongamano hili katika kanisa la EAGT lililopo Lumala mpya nyuma ya soko jipya la saba saba, Jijini Mwanza.
Prophet TB Joshua In Fresh Trouble With Ex-Ghanaian Footballer, Richard Kingston Over Alleged Wife's Witchcraft Confession.
TB Joshua |
CONTROVESIAL man of God, Prophet Temitope Babatunde Joshua popularly known as TB Joshua may have landed himself into a fresh trouble with Ghanaian and ex-Birmingham City shot-stopper, Richard Kingston over an alleged confession by the footballer's wife, Adelaide Tawaih Kingston that she was a witch.
It is always said that 'whatever God has joined together, let no man put asunder'. This may be what Richard Kingston is trying to avoid in his marriage by coming out to defend his pretty wife.
Few days ago, during a satellite broadcast of TB Joshua's Synagogue Church of All Nations (SCOAN), Ikotun, Lagos church service, Adelaide purportedly confessed that she was a witch. She also purportedly revealed that she was the cause of her husband's nose-diving footballing career. The broadcast further purportedly showed that Adelaide allegedly confessed to be the cause of Richard's impotence.
She was quoted to have allegedly said, "I messed up Richard’s life ever since we got married (2010). I used my evil powers to trouble his career. I’ve been working on him spiritually, to the point he could not perform in bed."
Soon after the controversial broadcast, Adelaide was reported to have gotten harsh criticism back home in Ghana. She later reportedly claimed that she was hypnotised and was never aware of when such things were said by her.
In defence of his wife about the whole issue, 34 years old Richard took to Facebook to deny claims that his wife was responsible for his dwindling footballing career and that she made him impotent. The former Wigan and Blackpool goalkeeper wrote on his Facebook wall, "My wife is not a witch."
Richard Kingston with his wife Adelaide |
In the first week of September 2012, it was reported that Adelaide was at TB Joshua's church where she allegedly confessed being a witch. Last week Sunday, September 9, 2012, we gathered that Richard stormed TB Joshua's SCOAN to express his displeasure at the witch-tag placed on his wife after the global broadcast of the 'controversial' service his wife purportedly confessed being a witch.
This latest development has put the controversial man of God in the spotlight again. This is not the first time TB Joshua is getting into trouble with Ghanaians. Recall that soon after the death of Ghana's former President, Prof. Attah Mills, few months ago, he came under heavy criticism over his prophecies.
Richard has since leaving Blackpool in 2010 been on the low key career-wise. He recently revealed that he refused a tempting £190,000 bribe from Czech Republic, which was aimed at him allowing to make his country lose their match against Czech Republic at the 2006 FIFA World Cup group game.
Mtangazaji wa Kipindi cha Television na Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Vandarray, atoa wimbo mpya baada ya kunusurika ajali.
Cover la wimbo "I made It" |
Bofya Hapa
Tuesday, September 11, 2012
Semina ya Mwl. Christopher Mwakasege sasa kufanyika Viwanja vya jangwani na si Biafra.
Mwl. Christopher Mwakasege |
MTUMISHI wa Mungu Mwl. Christopher Mwakasege anatarajia kufanya Semina ya Neno la Mungu Jijini Dar es salaam Mwezi huu wa 9 kuanzia tarehe 23 -30 katika Viwanja vya Jangwani.
Mwl. Mwakasege anasema; "Wakati wa semina ya Arusha na Dar es salaam kutakuwa na kipindi cha vijana wa chuo, sekondari na walioko nyumbani siku ya jumamosi tarahe 15/9/2012 kwa Arusha(uwanja wa reli) na 29/9/2012 kwa Dar es salaam(uwanja wa jangwani) kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa sita mchana. Mungu awabariki sana na tunashukuru kwa maombi yenu na tunaendelea kuwaombea."
Pastor Daniel Moses Kulola anakukaribisha kwenye OYES CONFERENCE - Mwanza.
Pastor Daniel Moses Kulola |
MCHUNGAJI Daniel Moses Kulola wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya la Jijini Mwanza, anakukaribisha katika Kongamano la Kimataifa la OYES yaani "OPEN YOUR EYES AND SEE", Kongamano litakalofanyika katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Jipya la Saba Saba.
Mhudumu wa Kimataifa Mch. John Bigirimana kutoka Norway atahudumu. Kongamano hilo linatarajia kuanza Jumatano hii kuanzia Saa 8:30 Mchana mpaka Saa 12:30 Jioni, na Kongamano hili litaisha Siku ya Jumapili.
Kila siku ya Kongamano kutakuwa na shifti 2. Kwaya Mbalimbali na Waimbaji binafsi pia watakuwepo ili kuhudumu katika kongamano hilo. Ukipata taarifa hii, mtaarifu na Mwenzako.
NYOTE MNAKARIBISHWA!
Mchungaji Vinac Mwakitalu; Matatizo ya Serikali ya Tanzania, Chanzo ni Kanisa.
Mchungaji Vinac Mwakitalu |
WAKRISTO wametakiwa kujua kwamba matatizo makubwa katika serikali ya Tanzania yanatokana na wao kutokuwa waaminifu mbele za Mungu katika kufanya Ibada ya Utoaji.
Mchungaji Mwakitalu ameongeza kusema Mungu ndiye anayejua kipimo halisi cha utoaji kwa mtu wa Mungu na kwamba kwa kufanya hivyo hakuna anayeweza kumdanganya Mungu. Pia Mchungaji Mwakitalu amesema wengi wamefikiri kuwa kufunga na kuomba sana ndio miujiza itafanyika huku wakisahau utoaji wa Mafungu ya 10 na sadaka mbalimbali.
Sunday, September 9, 2012
Kanisa la Anglikana lataka kuwa na Raisi.
Alisema mtu atayechukua nafasi hiyo ataweza kusafiri kwa urahisi, na hivyo kumuacha Askofu Mkuu kushughulika zaidi na kuongoza kanisa.
Doctor Williams, ambaye anastaafu mwezi Disemba baada ya uongozi wa miaka 10, alikiri kuwa hakuweza kufanya mengi kuzuia mgawanyiko kanisani juu ya swala la uhusiano wa jinsia moja.
BBC Swahili
Mchungaji aliyebadili Dini kuwa mkristo, aachiwa huru baada ya kifungo cha Miaka 3 gerezani.
Sehemu mbalimbali Duniani kulikuwa na maombi ya mnyororo ya kufunga kwa wakristo ili kumuomba Mungu awezeshe kuachiwa huru kwa Mchungaji huyo na hilo Mungu amefanya leo kwani Mchungaji Youcef ameachiwa huru na kuungana na familia yake.
Glory to God!
Friday, September 7, 2012
Mahakama Mkoani Arusha yaitupilia mbali kesi ya Kanisa Anglikana.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Fatma Massengi, aliyesikiliza shauri hilo la madai namba 118/2011 na jinai namba 48/2011 yaliyofunguliwa na waumini wa kanisa hilo, Parokia ya Mtakatifu James, Lothi Oilevo, Godfrey Mhone na Frank Jacob, dhidi ya bodi ya wadhamini wa kanisa hilo pamoja na askofu huyo.
Hata hivyo baadaye mahakama ilimuengua kwenye shauri hilo Mhone baada ya kushindwa kukidhi vigezo kisheria.
Katika hukumu yake jana, Massengi alisema kuwa alifikia uamuzi wa kuliondoa shauri hilo mahakamani hapo bila gharama wala kutoa maagizo yoyote baada ya kuridhika na pingamizi zilizowasilishwa na mawakili wa wadaiwa, Albert Msando na Joseph Thadayo.
Mawakili hao walidai kuwa mahakama hiyo haina nguvu kisheria kusikiliza shauri hilo kwani katiba ya kanisa hilo iko wazi kuwa masuala yote ya uchaguzi ndani ya taasisi hiyo yatashughulikiwa na ngazi mbalimbali ndani ya kanisa, ambapo mamlaka ya mwisho ya rufaa ni nyumba ya maaskofu wa kanisa hilo inayojumuisha maaskofu kutoka dayosisi zote.
Jaji Massengi alisema kuwa hata mambo yanayobishaniwa kisheria hayapo kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali yako kwenye Katiba ya Kanisa la Anglikani, ambayo mahakama hiyo haina nguvu kisheria kuyaingilia.
Aliongeza kuwa kutokana na msingi huo mahakama haiwezi kuingilia suala hilo huku akikubaliana na hoja za Wakili Msando kuwa wadai hao walifanya makosa ya kisheria kwenye hati ya kufungua madai mahakamani hapo ambapo badala ya kuandika namba ya usajili wa bodi ya udhamini ya kanisa waliweka namba ya cheti cha usajili ya kanisa SO 4757.
Katika kesi ya msingi wadai hao kwa pamoja waliomba mahakama itoe tamko kuwa Hotay waliyedai alidanganya katika cheti chake cha kuzaliwa cha Februari 12, 2010 na kwamba cheti hicho kilitolewa kwa njia ya udanganyifu, hivyo mchakato wote wa uchaguzi ukiwamo wa Aprili 15 mwaka huu uliomweka madarakani ni batili.
Wadai hao kupitia wakili wao, Meinrad D’Souza, walidai kuwa Katiba ya Kanisa la Anglikani, inaeleza kuwa mchungaji wa kanisa hilo anayeweza kufikiriwa kutwaa cheo hicho cha juu, anatakiwa awe na miaka kati ya 40 na 60 wakati inadaiwa mchungaji huyo mwaka jana alikuwa ana miaka 38 .
Katika kesi yao ya pili, waliiiomba mahakama kuzuia sherehe za kusimikwa kwake zilizopangwa kufanyika Juni 12 mwaka huu jijini Arusha, hadi kesi zote zitakaposikilizwa na kutolewa maamuzi na mahakama hiyo.
Aidha, shauri hilo lilisimama kwa muda baada ya Juni 10 mwaka huu, Jaji Sambo aliyekuwa akisikiliza shauri hilo kutoa amri ya zuio la muda kuzuia Hotay asisimikwe kushika wadhifa huo katika sherehe zilizopangwa kufanyika siku mbili baadaye ili kumwezesha kutoa uamuzi wa mapingamizi hayo Juni 13, mwaka huu.
Licha ya zuio hilo, sherehe za kusimikwa Hotay ziliendelea na akapewa daraja la uaskofu bila kupangiwa kituo rasmi cha kazi, hatua iliyoibua mvutano mkali wa kisheria kati ya kanisa hilo na Idara ya Mahakama baada ya Jaji Sambo kutoa amri ya kukamatwa Askofu Mkuu wa kanisa hilo nchini , Dk. Valentino Mokiwa na askofu Hotay ambao walikata rufaa Mahakama ya Rufani.
Tanzania Daima
KKKT laitaka Serikali kuweka sheria Madhubuti Juu ya Unyanyapaaji wa Walemavu.
Katibu mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini bwana Julius Mosi ametoa kauli hiyo wakati akikabidhi viti mwendo nane kwa watu wenye ulemavu vilivyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la Gabriella Children Rehabilitation center katika kijiji cha Uhuru kata ya Arusha chini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.
Bwana Mosi amesema kutokana na kuendelea kubaguliwa kwa watu wenye ulemavu na kunyimwa haki zao za msingi ni vyema serikali ikaweka mkazo wa kuwalinda watu hao ikiwa pamoja na kuwapatia elimu maalumu itakayowawezesha kutumia viungo vyao ili waweze kujitegemea.
Nae mkurugenzi wa shirika la Gabriella Children Rehabilitation centre lenye makao yake mjini linalojihusisha na utoaji huduma kwa jamii kwa watu wenye ulemavu Bi.Brenda Shuma, amesema shirika lake litaendelea kutoa misaada kwa watu wenye ulemavu ili kuwajengea uwezo wa kutumia viungo vyao katika kufanya kazi mbalilimbali za kujiletea maendeleo.