Miaka kumi na tano baada ya ziara ya mtangulizi wake Papa John Paul II ambaye alitoa ujumbe wa amani katika nchi hiyo yenye asilimia 35 ya wakristo na 64.6 ya waislam. Benedict wa kumi na sita atatoa ujumbe kwa waumini hao waliugawanyika kisiasa na msimamo kuhusu vita vya nchini Syria.
Papa Benedict ambae anazuru nchi hiyo katika kipindi kigumu, anatakiwa kuwatia moyo wa kristo baada ya kuongeza kwa makundi ya kiislam na kuomba kusitishwa kwa machafuko nchini Syria.
Barabara nyingi za mji mkuu Beyrouth zimefungwa kwa ajili ya kuimarisha usalama, ambapo viongozi wamethibitisha kuwa vyombo vya usalama vimehamasishwa kuhakikisha usalama unaimarishwa na kuhakikisha kuwa ziara hiyo ya kiongozi wa kanisa Katoliki inafana.
Akiwa Lebanon Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki atahudhuria mkutano wa vijana ambao utawaleta pamoja waislam na wakristo ambapo Kiongozi huyo atahitimisha shughuli zake siku ya jumapili kwa kuongoza misa huko Beirut na inatazamiwa kuhudhuriwa na waumini elfu sabini na tano.