Advertise Here

Friday, August 30, 2013

Matukio katika Picha ya Tamasha la Hhc Alive Fm lililofanyika Nyakato Mwanza.

Hizi ni baadhi ya Picha za Tamasha la Radio ya Kikristo ya Hhc Alive Fm ya Jijini Mwanza liliyofanyika Kanisa la FPCT Nyakato Mwanza chini ya Mch. Saimon, Jumapili iliyopita, ikiwa ni muendelezo wa Ziara ya Matamasha ya Ujirani yatakayohitimishwa Mwezi wa 12, Mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba.
Agape Choir - Nyakato


Amani Choir
Waliopo mbele ni baadhi ya Watangazaji wa Hhc Alive Fm
Baadhi ya watu waliohudhuria Tamasha hilo
Revival Mission Band
Kutoka Kushoto: Flora John, Adolph Nzwalla na Sowane Emmanuel
Watu wakimsifu Mungu
EAGT Revival Kisesa - Wana wa Mshika Mbili

Utukufu kwa Mungu

Rehema Chalamila a.k.a Ray C abatizwa.

Hii ni Tweet aliyoiandika Ray C baada ya Kubatizwa


- Uncle Jimmy -

Thursday, August 29, 2013

Sikiliza Kauli ya Mch. Daniel Kulola Juu ya Kifo cha Baba yake Askofu Mosses Kulola.

Marehemu Askofu Dr. Mosses Kulola enzi za Uhai wake
Haya ni Mahojiano kati ya Mtoto wa Marehemu Askofu Dr. Mosses Kulola, Mch. Daniel Kulola na Mtangazaji wa Hhc Alive Fm(91.9Mhz - Mwanza), Maganga James Gwensaga yaliyofanyika Jioni ya leo, kuhusiana na Kifo cha Askofu Dr. Mosses Kulola.


Askofu Dr. Mosses Kulola afariki Dunia.

Marehemu Askofu Mosses Kulola enzi za Uhai wake

Wednesday, August 28, 2013

Yolanda Adams atimiza Miaka 52.

 

Jina: Yolanda Adams

Kuzaliwa: August 27, 1961

Mahali: Houston, Texas, United States

Nafasi: Singer, Record Producer, Actress, Radio Host

Kuanza kwa Huduma: 1979 Mpaka Sasa

Labels: Sound of Gospel, Tribute/Benson, Verity, Elektra, Antlantic, Columbia, N-House Music Group

Tuesday, August 27, 2013

Mihadhara ya kidini yaruhusiwa kwa Masharti.

MIHADHARA ya dini iliyokuwa imepigwa marufuku na Serikali imeruhusiwa kuendelea kwa masharti ya kutojihusisha na mahubiri yanayolenga kupandikiza chuki miongoni mwa Wakristo na Waislamu. Serikali pia imewataka viongozi wote wa dini kuwakataa na kuwapiga marufuku watu wanaojiingiza katika nyumba za ibada huku wakiwa na malengo ya siasa.

Akizungumza katika kongamano la Umoja wa Wahadhiri wa dini za Kikristo na Kiislamu Dar es Salaam juzi, Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja alisema Serikali haiwezi kuingilia shughuli za dini kama zinaendeshwa kwa ustaarabu bila kuvunja sheria.


Chagonja ambaye alimwakilisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Dk. Emanuel Nchimbi alisema Serikali haijawahi kupiga marufuku mihadhara yoyote inayoendeshwa bila kusababisha vitendo vya chuki na uhasama kwa Watanzania.

Kuruhusiwa kwa mihadhara hiyo kumekuja ikiwa imepita zaidi ya miezi minane tangu Serikali ilipopiga marufuku mihadhara hiyo nchi nzima ikiwa ni hatua ya kukabiliana na machafuko ya dini yaliyokuwa yanalinyemelea taifa.

Uamuzi huo ulichukuliwa siku chache baada ya baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu kujiandaa kuandamana kwenda Ikulu kutaka atolewa rumande Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda.

Katika kongamano la juzi, Chagonja aliwaasa viongozi hao kuwa na mfumo mpya wa dhana ya uhalisia ya kutangaza dini na kuacha kukejeliana kati ya dini moja na nyingine kuepuka vitendo vya chuki za dini.

Kiongozi wa Mihadhara ya Kiislam, Naibu Amir, Shekh Rajabu Salum, alisema mihadhara ya pande zote mbili ijulikanayo kama ‘mihadhara linganishi’ haijawahi kuwa tishio la amani nchini.

Naye Mwenyekiti wa mihadhara ya Kikristo, Mwinjilisti Daniel Mwankemwa alisema mihadhara yao imetoa mchango mkubwa kwa waumini wao kuimarika kiroho baada ya kupata ufafanuzi sahihi wa hoja mbalimbali zilizokuwa zikiwasumbua.


- Mtanzania -

Monday, August 26, 2013

Mwimbaji wa Ambassadors of Christ ya Rwanda achumbiwa Tanzania.

Photo: Thank you Lord
Warren Bright akimvisha pete ya uchumba Humure Rebecca
Mwimbaji wa Sauti ya kwanza wa  Ambassadors of Christ ya Rwanda Humure Rebecca amechumbiwa na Mwimbaji na Kiongozi wa kundi la Voices of Victory la jijini Dar es salaam,Warren Bright.

Sherehe fupi ya uchumba ilifanyika nyumbani kwa wazazi wa Warren Bright, Kunduchi  jijini Dar es salaam Agosti 17, 2013 na ilihudhuriwa na waimbaji baadhi wa nyimbo za injili nchini Tanzania na mwimbaji wa kiume wa Ambassadors of Christ, Nelson Manzi.

Warren ambaye ameweka picha za tukio hilo katika wasifu wake wa facebook  amesema arusi yao  inatarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Waimbaji wengine wa Ambassadors of Christ ambao wamefunga pingu za maisha na waimbaji wenzao ni Dushimimana Desire ambaye hivi karibuni alimuoa mwimbaji wa kwaya nyingine ya mjini Kigali na Umurisa  Yvonne mwimbaji wa solo ya wimbo wa Kwetu Pazuri  aliyeolewa na Josué Blaise Habimana aliyekuwa mwimbaji wa Halelujah Choir ya Gisenyi, Rwanda na kwa sasa wana mtoto mmoja wa kike.

Mchungaji Kanisa la FPCT acharazwa bakora.

MCHUNGAJI wa makanisa ya Pentekoste yaliyoko katika kijiji cha Buatika katika wilaya ya Butiama, mkoani Mara, amejeruhiwa na kushonwa nyuzi 12 kichwani baada ya kucharazwa viboko na wazee wa kimila wa Kizanaki akituhumiwa kuhamasisha watu kupinga tambiko kwa mizimu.

Mchungaji huyo Yohana Jimwaga wa Kanisa la Free Pentecost Church of Tanzania-FPCT, alifikwa na zahama hiyo juzi majira ya saa 10.00 baada ya kuvamiwa na kundi la wazee hao wakati akiwa njiani kutoka kisimani kuchota maji kwa baiskeli.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Yohana alisema akiwa hajui kinachoendelea ghafla wazee hao wa kimila waliokuwa wamevalia ngozi za wanyama na shanga shingoni, walimvamia na kuanza kumpiga wakidai anaenda kinyume na mila zao.

Kwa mujibu wa Yohana siku mbili zilizopita wazee hao wa kimila waliutangazia umma wa kijiji hicho kuwa hairuhusiwi kufanya kazi zozote za kiuchumi wala kijamii ikiwa ni pamoja na kusomba maji, kuchanja kuni, kupika, kuchinja nyama na kuuza maduka.

Alisema sababu za wazee hao kutangaza hilo ilikuwa kuwataka wakazi hao wajitakase tayari kwa kutambika kwa mizimu ili mvua inyeshe katika maeneo hayo sambamba na kuishawishi iwarejeshee dhahabu katika mgodi wa Buhemba ulioharibiwa na wawekezaji.

Alisema baada ya tangazo hilo la wazee, waumini wa madhehebu mbalimbali ya kidini kwa upande wao hawakulitilia maanani kwa vile haiendani na imani yao hali iliyowafanya waendelee na shughuli zao kama kawaida.

Mchungaji Yohana alisema baada ya wazee hao kuona kwamba wamepingwa na waumini wa dini, waliendesha operesheni maalumu ya kuwasaka viongozi wa dini ikiwa ni pamoja na kuzikamata mali zao ikiwemo mifugo kama faini huku wengine wakiambulia vipigo.

Kamanda wa polisi mkoani Mara Kamishna Msaidizi, Ferdinand Mtui, alipoulizwa kwa njia ya simu alikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu 11 wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi huku uchunguzi ukiendelea.

- Habari Leo -

Saturday, August 24, 2013

Kanisa la KKKT lachomwa Moto Dar.

Mchungaji Usharika wa Segerea wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Noah Kipingu akionyesha sehemu ya madhabahu ya kanisa hilo, iliyoungua moto baada ya kurushiwa vitu vinayosadikiwa kuwa ni mabomu ya petroli na watu wasiojulikana.
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la Kati, Usharika wa Segerea Wilaya ya Ilala, limechomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.

Tukio hilo lilitokea saa saba usiku, wakati waumini wa kanisa hilo wakiwa katika mkesha wa maombi ya maandalizi ya mkutano wa injili unaoanza leo.

Mchungaji wa kanisa hilo, Noah Kipingu alisema wakati wakiwa katika maombi ghafla walisikia sauti ya kitu kilichorushwa kutoka nje ya kanisa kikiambatana na moto, ambapo kilianguka madhabahuni na kuanza kuunguza baadhi ya vifaa vya kanisa.

“Tukiwa tumesimama mbele ya madhabahu kwa njia ya mduara ndipo nyuma ya madhabahu ukatokea mlipuko mkubwa kwa sauti ya kishindo, na moto ukatanda madhabahu,” alisema Kipingu na kuongeza kuwa:

“Katika namna ya kibinadamu hakuna aliyeweza kuvumilia, kila mtu alikimbia akitafuta namna ya kujiokoa.”

Kipingu alisema kuwa alipobaini kuwa ulikuwa ni moto wa mafuta aliwaambia waumini wake waingie ndani kwa ajili ya kuuzima, wakati wakiuzima moto huo walipata taarifa kuwa gari la Mchungaji, Toyota Cresta lenye namba za usajili T 482BAF lililokuwa nje ya kanisa lilikuwa likiwaka moto.

“Baadhi ya waumini waliokuwa ndani walikwenda nje kushirikiana na mlinzi kuuzima moto huo, tunamshukuru Mungu kwamba matukio yote mawili tumeyashinda kwa uwezo wake,” alisema.

Kipingu alisema kuwa shambulizi hilo lilizua taharuki kubwa kwa waumini wake, na kwamba baadhi ya watu waliwaona watu wanne wakikimbia kutoka eneo la kanisa baada ya kutukio hilo.

Shukuru Thobias mmoja wa waumini waliokuwepo kanisani wakati tukio hilo likitokea, anasema aliona vitu kama mshale vikianguka madhabahuni na vilipodondoka vililipuka kama moto.

“Moto ulianza kuunguza Biblia na makapeti, ndipo tukaanza kukimbia kwenda nje kuchukua mchanga na kuanza kuuzima.

Baada ya hapo tulianza kukimbia huku wengine wakidondoka na kujeruhiwa kidogo miguuni. Niliporudi baadaye niligundua zilikuwa ni chupa tatu za bia zilizokuwa zimetengenezwa bomu la petroli,” alisema Thobias.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo hakuna mtu aliyepoteza maisha na kulitaja kuwa ni jaribio la kiharifu lililoshindwa.

“Hakuna mtu aliyepoteza maisha, lilikuwa jaribio ambalo halikufanikiwa. Wakati tukio linatokea waumini walikuwa kanisani kwa hiyo waliwahi kuuzima moto kabla haujaleta madhara,” alisema Kova.

Mei 26, 2012, Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo Mtaa wa Kariakoo mjini Unguja, lilichomwa moto usiku na watu wasiofahamika.

- Mwananchi -

Naomba Mchango wako ili niweze kutoa Video ya Album yangu.

Neema Decoras
Rafiki na ndugu yangu mpendwa;

Ninamshukuru Mungu kwa kuniwezesha kutoa albamu yenye nyimbo nane inayoitwa Milele Nitalisifu Jina Lako (Zaburi 145:1-3) katika mfumo wa Audio CD.

Lakini nimeshindwa kukufikishia albamu hiyo hapo ulipo kwa sababu wasambazaji na wauzaji wanaamini wewe na ndugu zangu wengine mnapenda kuangalia Video kuliko kusikiliza Audio.

Ninahitaji shilingi za Tanzania milioni tatu (Tshs 3,000,000/=) ili niweze kulipia na kufanikiwa kutoa albamu yangu katika mfumo wa Video CD/DVD na hii ni changamoto mbayo imezidi uwezo wangu.

Kwa msaada wako wa kifedha, ufadhili, udhamini au kujitolea kunifanyia video bure au kwa gharama ndogo ninaamini nitaweza kufanikisha hili na kuwezesha huduma na kazi hii ya Mungu kusonga mbele.

Hivyo rafiki na ndugu yangu mpendwa, ninaomba mchango wako wa kiasi chochote cha fedha utakacho jaaliwa ili niweze kutoa video ya albamu yangu.

KUCHANGIA TAFADHALI TUMIA NAMBA
+255658027515 (tiGO Pesa & SMS)

Asante sana kwa kuthamini, kuzingatia na kutumia muda wako kusoma post hii!

Neema Decoras
Phone: +255 658 027515
Email: neemadecoras@yahoo.com

Kanisa lapanga kuzika tena mwili wa kasisi uliofukuliwa nchini Kenya.

Dominic Jordan
Maafisa wa polisi wakichunguza kaburi alimozikwa Padre Dominic Jordan katika makaburi ya Mathari Consolata Mission Nyeri Agosti 20, 2013.
MATAYARISHO ya kumzika tena Kasisi Dominic Jordan ambaye mwili wake ulifukuliwa kutoka kwa kaburi lake huko Mathari,Nyeri mnamo siku ya Jumanne yanaendelea.

Makasisi wa kanisa katoliki wamemteua Kasisi Gachanja ili kuandaa  matayarisho  ya mazishi  hayo ambayo yatakuwa ya kipekee kufanyiwa Kasisi wa Kanisa katoliki hapa nchini.

Alhamisi Polisi walithibitisha kwamba mwili wa Kasisi Jordan ulikuwa na viungo vyote huku wakishuku kwamba wahalifu wanaoshukiwa kuchimba kaburi lake maarehemu walikuwa na nia ya kuiba mali.

Mwili huo hata hivyo ulikuwa umeoza  kiasi kwamba ilibidi Mwalimu  mkuu wa shule ya upili ya St.Mary’s aitwe ili kuutambua mwili wa kasisi kwa kutumia mavazi aliyovalishwa wakati wa mazishi yake.

Marehemu Kasisi Jordan alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo kabla ya kifo chake. Viatu alivyovalia, shungi la nywele kichwani mwake na kola inayovalishwa makasisi wa Kanisa Katoliki ya Kirumi ndivyo vitu vilivyotumika kuutambua mwili wa marehemu.

Kasisi Jordan anasifika kwa kuwasaidia wanafunzi wengi kujiunga na chuo kikuu maarufu cha Harvard huko marekani wakati wa huduma yake.

Akiongea  na Taifa Leo kupitia kwa simu Afisa Mkuu wa Polisi mjini Nyeri  bwana Joseph Mwika alisema tofauti na ilivyodhaniwa hapo awali, ni mwili wa Kasisi Jordan ambao ulitolewa kwa Jeneza na kuwekwa kando  ya kaburi na wala hapakuwa na miili miwili ndani ya kaburi.

Bwana Mwika alisema mwili huo ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Konsolata Mathari huku matayarisho  ya mazizi yakiendelea.

Afisa huyo aliongezea kwamba  uchunguzi bado  unaendelea  lakini itakuwa vigumu kutoa ushahidi kwa bidhaa alizotumia mshukiwa kuchimba kaburi  kwani  mshukiwa huyo alikuwa amevalia glovu kwa mikono yake ili  kuficha alama za vidole.
Glovu alizovalia mshukiwa zilipatikana kando ya kaburi pamoja na jembe na sepetu.

Wakati huo huo Naibu wa Kamishna wa Kaunti ya Nyeri amewataka wakaazi kutohusisha tukio hilo na ushirikina.

Akiongea na waandishi wa habari Naibu wa Kamishna bwana John Marete alisema tukio hilo  lilikuwa ni uhalifu wa kawaida uliotekelezwa na watu waliodhania watapata mali kwenye  kaburi  la marehemu na wala lisihusishwe na  mambo mengine.

“Kama wakristo hatuamini ushirikina, tusifikirie kuna mambo mengine kuhusu tukio hili.Hili ni jambo la haibu na lisilostahili kutendeka katika jamii iliyostaharabika,”akasema bwana Marete.

Kasisi Bartholomew Mwangi  kwa upande wake alisema visa kama hivi vinaonyesha ukosefu wa maandili  katika jamii lakini akasisitiza kwamba  kanisa linatekeleza jukumu lake la kuwafunza wanadamu maadlili mema.

- Swahili Hub -

Thursday, August 22, 2013

Semina ya Neno la Mungu kwa akina Mama Buhongwa, Mwanza.

Mwl. Gilbert akifundisha
Semina ya Neno la Mungu kwa akina mama, imeanza siku ya Jana katika kanisa la KKKT Usharika wa Buhongwa, Mwanza chini ya Mwl. Gilbert aliyefundisha Somo lenye kichwa "Asili ya Kizazi", na namna Asili ya kizazi inavyoweza kuharibu maisha ya mtu, hasa mwanamke.

Semina hiyo itakayodumu kwa siku 5, imeanza rasmi jana na itamalizika siku ya Jumapili. Muda ni kuanzia saa 10:00 jioni hadi Saa 12:30 Jioni. Hivi ndivyo ilivyokuwa...








Praise Team

Wednesday, August 21, 2013

Video Mpya ya Paul Mwai - Kiambiriria.

Mchakato wa kumtangaza Kardinali Otunga kuwa Mwenye heri kukamilika Septemba 27.

Kardinali Otunga enzi za Uhai wake
Mheshimiwa Padre Celestino Bundi, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa na Kazi za Kimissionari nchini Kenya anasema, mchakato wa kumtangaza Kardinali Maurice Michael Otunga kuwa Mwenyeheri unatarajiwa kufikia ukomo wake kwa ngazi ya Kijimbo hapo tarehe 27 Septemba 2013.

Tukio hili linatarajiwa kutanguliwa na Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kumbu kumbu ya Kardinali Otunga pamoja na kuchangisha fedha ya kuanzisha Mfuko wa Kardinali Otunga hapo tarehe 6 Septemba 2013.

Kamati ya mchakato wa Kardinali Otunga inaendelea kukamilisha maandalizi, ikiwa ni pamoja na Kalenda za Mwaka 2014 zitakazosambazwa na Mabinti wa Mtakatifu Paul ambao wana mtandao mkubwa katika masuala ya maduka ya vitabu. Tarehe 6 Septemba 2013, Kamati itazindua mtandao utakaokuwa na taarifa na maelezo mbali mbali kuhusiana na maisha na utume wa Kardinali Otunga tangu alipozaliwa kunako mwaka 1923 hadi kufariki dunia kunako tarehe 6 Septemba 2003.

Kwa ufupi, Kardinali Otunga alizaliwa kunako tarehe 31 Januari 1923. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa hapo tarehe 3 Oktoba 1950. Tarehe 25 Februari 1957 akawekwa wakfu kuwa Askofu na Askofu mkuu James Robert Knox.

Tarehe 15 Novemba 1969 akateuliwa kuwa Askofu mkuu na hapo tarehe 5 Machi 1973, Papa Paulo wa VI akamteuwa kuwa Kardinali. Baada ya huduma iliyotukuka kwa Familia ya Mungu nchini Kenya, akafariki dunia hapo tarehe 6 Septemba 2003, Jijini Nairobi.

Itakumbukwa kwamba, Kardinali Otunga alikuwa ni kati ya Mapadre wa kwanza kwanza nchini Kenya. Akabahatika kuteuliwa kuwa ni Askofu, Askofu mkuu na hatimaye Kardinali. Ilikuwa ni tarehe 11 Novemba 2011 Jimbo kuu la Nairobi lilipoanzisha mchakato wa kumtangaza Kardinali Otunga kuwa Mwenyeheri na hatimaye Mtakatifu. Mchakato huu kwa ngazi ya Kijimbo unatarajiwa kuhitimishwa hapo tarehe 27 Septemba 2013.

Tuesday, August 20, 2013

Tukio moja, Kitabu kimoja, Maelezo na Habari ni tofauti. Tunafanyaje?

Habari wapendwa, tupeane maarifa katika  changamoto hii, ili tuwe na maelezo sahihi tuwapo kazini katika shamba la Bwana.


Najiuliza ivi je ni waandishi tofauti au ni yule katika Luka and Matendo? Na vipi sasa uwasilishaji  tofauti wa matukio yale yale-angalia pia Marco and Mathayo?Ni vema sana kukifahamu kitabu chetu (Biblia) ambacho ni bora kabisa kuliko vitabu vilivyowahi kuwako na kama vitakuwako vingine. Wakati mwingine Watu wa Mungu tunapokutana na changamoto ktk Kitabu chetu tukisomapo au hasa tukiuulizwa/kubanwa na wana dini,tunawahi kukemea pepo la upinzani na kufoka ili mtu huyo anyamaze milele au tunakua na hofu kua ni kukaribia kufanya makufuru kuchunguza/kufuatilia kila jambo ktk Neno!-mambo ambayo KiBiblia hayana msingi hata chembe, ni ya kibinadamu tu.

Kama/kwakua hiki ni Kitabu chetu cha ukweli na tunaamini kwa nguvu nyingi kua humo kuna maneno ya ukweli, kuliko kukimbia wajibu wa kulielewa Neno/Maandiko kwa kukemea pepo la kutoelewa ktkt ya watu( ana dini, majirani,wanafunzi tunaowafundisha, hadhira tunayohihubiri), ni faida na busara kufanya kila jitihada kukielewa Kitabu hiki kitamu mfano kukisoma na kukitakafari sana kila mara ili kupata kweli nyingine nyingi zilizomo kuweza ongelea mada/jambo/changamoto kadhaa, kusoma vyanzo vingine vya maarifa, kuuliza Viongozi wetu wa Kiroho au Mkristo mwenzio, kuomba/kumuuliza Roho Mtakatifu afunue/anunurishe ndani yetu pia  hata kuuliza watu wengine wa dini waliosomea tu Imani/Biblia kidarasani na njia nyingine bora na sahihi za kupata maarifa na ufahamu wa jambo.

Tukiulizwa haya yafuatayo ya kitabu chetu tukiaminicho sana, tunafanyaje? Tukemee pepo au tujibu kwa ujasiri na hakika kabisa? Tujadiliane kwa haya chini.

Mdo.1:1=Mwandishi Dr. Luka anatoa dokezo kwa Mpendwa Theofilo kuhusu kile   kitabu cha  ‘’kwanza’’ alichoandika kuhusu aliyoyafanya na kufundisha Yesu. Ni kitabu gani icho alichoandika kuhusu aliyoanza kufanya na kufundisha Yesu? soma hii ina connect..Luka.1:1-4 Anasema Luka kua ‘’nimeona vema kukuandikia mpendwa Theofilo upate kujua hakika ya mambo uliyofundishwa.....’’. Kwaiyo inaonekana kwamba aliyeandika kitabu cha Luka( see 1: 3) ndiye aliyeandika Matendo(check mstari 1:1) ambaye ni Mr. Luka aliyekua tabibu( bila shaka utagundua pia aina ya uandishi na namna alivyo-present coverage ya maisha ya Yesu ukilinganisha na injili nyingine kama ya Marko na Mathayo. Mfano- Luka ananza kwa kusema- nimependa ktk Kiingereza.. ‘‘Having perfect understanding of all things from the very first to write you an ORDERLY account'', tafsiri nyingine zinasema..''I, myself have carefully investigated everything from the beginning''.. ), Kwa iyo huyu daktari baada ya kufanya ''careful investigation ndipo akaandika in an orderly manner.. Sasa kwakua ukweli ndio huo, kumetokea nini hapa? Tunawekaje uwiano hapa?

Mdo.9:4-7 hasa mstari 7…waliokua pamoja na Paul ktk msafara pia ‘’WALIISIKIA ile  sauti’’, si Paul tu lakini ktk Mdo.22:1-10 hasa mstari 9..Paul anaposhuhudia/anajitetea mbele ya kundi la waliompiga vibaya kidogo wamuue,anasema….waliokua naye ktk msafara ‘HAWAKUSIKIA ile sauti’.Hapa Mwandishi ni mmoja, ndani ya kitabu kimoja na tukio  lilelile moja.

Pia Mathayo.27:24-28 hasa mstari 28 ..Wakamvua Yesu nguo na kumvika vazi JEKUNDU (scarlet robe) lakini Marco.15:15-17 hasa mstari 17..Wakamvika vazi la rangi ya ZAMBARAU (purple).Hapa waandishi ni wawili tofauti ila tukio lilelile.

Kama mtu wa Mungu tena mwana wa Mungu ambaye Biblia kwako ni Kitabu chenye maneno ya Baba, Bwana na Roho wetu, unasemaje juu ya hili?

Swali limeulizwa Na: Edwin Seleli

Mabomu mawili yapatikana Nje ya Kanisa Nairobi.

POLISI Jumatatu walilipua mabomu mawili yaliyokuwa yametegwa kwenye lango la Kanisa la Soldiers of Faith, eneo la Kiamaiko, Kaunti ya Nairobi. Mabomu hayo, moja lenye uzani wa kilo tano na lingine kilo mbili, yalipatikana na wananchi.

Wataalamu wa mabomu waliyatwaa mabomu hayo kuyalipua wakisema yalikuwa na uzito mkubwa na kwamba yangesababisha hasara kubwa kama yangelipuka yalipokuwa yamewekwa. 

“Hatungelilipua mabomu hayo mahali yalipokuwa kwa sababu yangeleta hasara kubwa katika eneo hilo,” akasema afisa mkuu wa polisi eneo la Starehe, Bw Samuel Anampiu.

Alisema polisi “hawawezi kukana dhana kwamba kanisa hilo lilikuwa linalengwa na washambulizi. Mabomu haya ni muundo ule uliotumika wakati wa vita vikuu vya kwanza na vya pili vya dunia. Yangali na nguvu na ni hatari sana.”

Bw Anampiu alisema mabomu hayo yalikuwa na uwezo wa kubomoa majumba na kufanya eneo hilo tambarare kama yangelipuka.
Aliwapongeza wakazi wa eneo hilo kwa kuchukua hatua ya haraka na kuwaarifu polisi.

 “Tunatambua juhudi za wakazi wa hapa kwa kuwaarifu polisi badala ya kukaa kimya kuhusu mabomu haya ambayo ni hatari kubwa kwa kila mtu,” akasema Anampiu.

Bi Maureen Adhiambo aliyeona bomu la kwanza, alisema alikuwa anasafisha lango la kanisa hilo alipoona kifaa hicho.

“Nilivuta kifaa hicho lakini kilikuwa kizito ndipo nikamwambia jirani na kumuomba ushauri,” akasema.

Alisema aliona bomu hilo mwendo wa saa tatu asubuhi na kwamba watu wachache walilichezea kabla polisi kufika. Bw Husein Nura, mkazi wa eneo hilo aliyemsaidia Bi Adhiambo kuondoa bomu hilo, alisema lilikuwa zito.

“Nilimwambia kwamba kifaa hicho si cha kawaida na huenda ni bomu,” akasema Bw Nura.

Muda mfupi baadaye, polisi walibeba bomu hilo kwa mfuko mweusi uliojaa changarawe. Bomu la pili lilipatikana muda mfupi baadaye.
Polisi walizingira eneo hilo huku wakitumia mbwa wa kunusa kutafuta mabomu zaidi. “Tumetafuta mabomu zaidi tukutumia mbwa wa kunusa. Hatujapata mengine na tuna hakika eneo hili ni salama sasa,” akasema Bw Anampiu.

Aliwatahadharisha wanaouza na kununua vyuma vikuukuu wajihadhari na vifaa vya chuma wasivyofahamu. Mkuu huyo wa polisi alisema hakuna mshukiwa aliyekamatwa kuhusiana na mabomu hayo.
Tukio hilo lililemaza biashara zote katika eneo hilo huku wakazi wakimiminika kanisani humo kuona mabomu hayo.

Mtawa wa Kanisa Katoliki avamiwa Zanzibar.

MTAWA wa Kanisa Katoliki la Bububu visiwani Zanzibar, Sister Irene Ludovik Mwenda (34), amevamiwa na watu wasiojulikana na kushambuliwa na marungu, hali iliyomsababishia maumivu makali mwilini. Sakata la mtawa huyo lilitokea jana, baada ya kuvamiwa na vijana wapatao kumi, baada ya mtawa huyo kuwa anafuga mbwa ambaye inaelezwa kuwa alikula kuku wa mmoja wa vijana hao.
 

Tukio hilo lilitokea juzi saa 11 jioni, jirani na maeneo ya Kanisa la Kigango cha Mtakatifu Thesia Beit –el-rus, katika nyumba wanazoishi watawa wa kanisa hilo.

Akizungumza jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini na Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtu huyo aliyepigwa ni mwanamke ambaye ni mtumishi wa Kanisa Katoliki la Bububu, Zanzibar.

Kamanda Mkadam, alisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliosababishwa na tuhuma za mbwa wa mtawa huyo kuwa amekula kuku wa kijana huyo, ambapo baada ya majibizano kijana huyo alipata jazba, hali iliyosababisha kumpiga ngumi mtawa huyo.

Kamanda huyo alisema kuwa baada ya kutokea tukio hilo, mtawa huyo alikwenda kufungua jalada la malalamiko katika Kituo kidogo cha Polisi cha Beit-el-rus, kuhusu kupigwa kwake na kijana huyo.

“Tupo tunaendelea na uchunguzi juu ya tukio hili, kwani ni ugomvi wa mitaani unaweza kuleta athari kubwa zaidi, lazima tufanye kazi hii kwa umakini zaidi,” alisema Kamanda Mkadam.

Hata hivyo alisema kuwa Jeshi la Polisi linamshikilia kijana huyo kwa ajili ya mahojiano zaidi, ili kujua sababu za kushambuliwa kwa mtawa huyo ambapo mpaka sasa yupo mikononi mwa polisi.

Alisema baada ya kesi hiyo kufikishwa polisi, wazazi wa kijana huyo walifanya juhudi za kuzungumza na mtawa Irene ili kuweza kufikia maridhiano na kijana huyo na pindi wakishindwa kuelewana, shauri lao litafikishwa mahakamani.

Hata hivyo kutokana na makubaliano hayo, mtawa huyo alikubali kumsamehe kijana huyo, huku polisi ikisema kutokana na sababu za kisheria na usalama, kijana huyo hataachiwa na jalada la kesi limepelekwa katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar, ili atoe ushauri kuhusu sakata hilo.

Shilingi Milioni 319 zaombwa kufanikisha Mkutano wa Bonnke Dar es salaam.

Reinhard Bonnke
BAJETI iliyowasilishwa na Kamati ya Maandalizi ili kufanikisha mkutano wa Injili wa mhubiri wa kimataifa, Mwinjilisti  Reinhard Bonnke unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania Agosti 21 hadi 25, mwaka huu ni dola 199,314.38 sawa na Shilingi za kitanzania 318,903,000

Kamati hiyo inaongozwa na Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG, Magnus Mhiche (mwenyekiti), Mchungaji Kiongozi wa huduma ya The Oasis Healing Ministry, Prosper Ntepa (makamu mwenyekiti), Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania-Pentecoste Council of Tanzania (PCT), Askofu David Mwasota (katibu), na Askofu Bathlomew Sheggah, ambaye ni mhamasishaji.
Wataalamu wa kufunga jukwaa ambalo litatumika katika mkutano wa Bonnke
Hadi Jumatano Agosti 14, kamati hiyo ilikuwa imepokea dola 60,000 sawa na Shilingi za kitanzania karibu milioni 100. Kwa mujibu wa bajeti hiyo, waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali ambao watahudhuria mkutano (press conference) kabla ya Bonnke kuanza kuhubiri, watatia kibindoni shilingi laki moja kila mmoja. Bajeti kwa ajili ya tukio hilo tu imepangwa kuwa dola za Marekani 1,212.50 sawa na shilingi za kitanzania 1,940,000.00

Katika bajeti hiyo imeelezwa kuwa viongozi watano wa kamati hiyo kila mmoja atapata malipo ya shilingi za kitanzania 200,000 kwa ajili ya mawasiliano na shilingi 350, 000 kwa ajili ya mafuta ya gari kwa siku moja. Bajeti hiyo inaonesha kutenga shilingi za kitanzania 2,100,000 kwa ajili ya wamama watakaokesha kuombea mkutano huo. Bajeti kamili imewatengea Wamama Shilingi za kitanzania 11,180,000. 
Gari lililobeba vifaa vya kujenga jukwaa likiwa tayari uwanjani
Bajeti kamili imekaa kama ifuatavyo:
Hospitality  Tsh 765, 0000   USD 478.13
Protocol      Tsh 9,665,000   USD 6,040.63
Counselling & Follow-up  Tsh 10,779,000 USD 6,736.88
Transport  Tsh 32,300,000   USD 20,187.50
Security Tsh 9,902,000   USD 6,188.75
Intercessory  Tsh 7,800,000  USD 4,875.00
Ushers  Tsh 4,600,000   USD 2,875.00
Music and Praise Tsh 8,400,000  USD 5,250.00
Admin & Central Committee Tsh 50,940,000.00 USD 31,837.50
Women  Tsh 11, 180, 000  USD 6,987.50
Publicity  Tsh 83,100,000    USD  51,937.50
Interpretation  Tsh 3,000,000 USD 1,875.00
Technical  Tsh 4,000,000     USD 2,500.00
Fire Conference Tsh 6,000,00 USD 3,750.00
Youth  Tsh 5,000,000    USD  3,125.00

Bajeti hiyo haigusi gharama za malazi ya Bonnke na watumishi atakaoambatana nao akiwemo Mchungaji Daniel Kolenda. Zinahusisha malipo katika ukumbi wa watu maalum katika uwanja wa ndege (VIP Lounge) kwa siku mbili watu 11 ambapo zimeombwa shilingi za kitanzania 2,200,000.

Hhc Alive Fm yaendelea na Ratiba yake ya Matamasha ndani ya Jiji la Mwanza.

Maganga James Gwensaga akiwa na Adela Mwampamba katika Tamasha lililofanyika Mkudi
Radio ya Kikristo ya Hhc Alive Fm(91.9Mhz) ya Jijini Mwanza, imeendelea na ratiba ya Matamasha yake ya kila jumapili katika maeneo mbalimbali ya Jijini Mwanza, ikiwa ni sehemu ya utangulizi wa Tamasha kubwa kabisa la FRIENDS FOREVER litakalofanyika Mwezi wa 10 Mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
Sehemu ya Umati uliohudhuria Tamasha la Kiseke
Akizungumza na Mtandao huu, Meneja wa kituo hicho Bw. Maganga James Gwensaga amesema kuwa Matamasha haya yatakuwa yakiendelea hadi mwezi wa 10 na hitimisho lake litakuwa ni Tamasha kubwa litakalofanyika CCM Kirumba.
Moja ya kwaya zilizohudumu katika Tamasha la Kiseke
Lengo la Matamasha hayo ni kuweka Wasikilizaji pamoja na jamii kuwa karibu zaidi na Timu nzima ya Hhc Alive Fm. Katika Matamasha hayo kwaya mbalimbali na waimbaji binafsi hupata fursa ya kuhudumu, huku timu nzima ya Watangazaji wa Hhc Alive Fm wakifanya Performance Jukwaani.
Adela Mwampamba na Japhet Busanji
Mpaka sasa Matamasha hayo yamefanyika Maeneo ya Mkudi na Kiseke.

Monday, August 19, 2013

Semina ya Mpenyo Mkoani Shinyanga.

Zaidi ya Shilingi milioni mbili zapatikana Ujenzi wa Kanisa Njombe.

KAMA maandiko yanavyosema Mwenye Nacho Huongezewa na Ombeni Mtapewa Basi Maandiko Hayo Yamejidhilisha Pale Wakati wa Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la Lutherani Katika Kitongoji cha Makungu Kijiji cha Igwachanya Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe Ambapo Idadi ya watu na Kiasi Cha Fedha Kilichopo patikana Huwezi Kuamini Kwa Macho yako Kama Sio Tomaso.

Zaidi ya Shilingi Milioni Mbili Pamoja na Ahadi zimeweza Kupatikana Jana Katika Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la KKKT Mtaa wa Nazareth Usharika wa Usuka Wilayani Wanging'ombe,Kiserikali ni Kitongoji cha Makungu Kijiji cha Igwachanya Kata ya Igwachanya Kufuatia Udogo wa Kanisa Lililopo na Kupelekea Waumini Hao Kutumia Hema Katika Kuendeshea Ibada zao siku Zote za Bwana Kwa Kipindi cha Miaka Mitatu Sasa.

Aidha Wananchi na Waumini wa Kitongoji Hicho Wameeleza Kutumia Hema Hilo wakati wa Jua na Mvua Katika Ibada zao Hali Iliyopelekea Kuchukua Uamuzi wa Kuanza Kujenga Kanisa Ambalo lipo katika Hatua za Awali za Msingi na Kisha Kuamua Kuitisha Harambee ya Kuchangia Ujenzi Huo.
Waumini wakichangia vifaa mbalimbali kama Mabati
Risala ya Ujenzi wa Kanisa Hilo Iliyosomwa na Mwanjilisti wa Igwachanya Bi.Lonika Yelemia Yombwi Imebainisha Malengo ya Dhati Katika Kujenga Kanisa Hilo Litakalo Gharimu zaidi ya Shilingi Milioni Kumi Hadi Kukamilika kwake na Kwamba Waumini wa Mtaa Huo Tayari wameshaanza Kwa Kuandaa Tofali Elfu Kumi,Mawe Pamoja na Kukamilisha Ujenzi wa Msingi.
Hali ya Kanisa kwa sasa
Kufuatia Taarifa Hiyo iliyoibua Hisia za Waumini na Wageni Mbalimbali walioshiriki Harambee Hiyo Ilimfanya Mgeni Rasmi Bwana Belshaza Muhanga Ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Igwachanya Kutoa Neno Lililomgusa Kila Mmoja Hadi Kupelekea Kufanikisha Zaidi ya Shilingi Milioni Mbili.

Miongoni Mwa Maneno yaliyosemwa na Bwana Belshaza Kutoka Kwenye Maandiko Matakatifu ni Pamoja na Kwamba Kushindwa Kutoa Sadaka Kubwa Wakati Unayo ni Kumuibia Mwenye Mungu Kwani Kila Kitu ni Mali yake,Maneno Ambayo yalitabiri Ukweli Katika shughuli Hiyo Muhimu na Kufanikisha Kiasi Hicho.

 
Mara Baada ya Kuzungumza na Kuchangia Mchango wake Huo Pamoja na Ahadi ya Shilingi Laki Mbili Kutoka Kwa Mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi Mhandisi Gerson Lwenge Ndipo Bwana Belshaza Akasimama na Kutangaza Mafaniko ya Harambee Hiyo.

Kwa Upande wake Mchungaji wa Usharika wa Usuka Ambaye Alishiriki Ibada Hiyo Bwana Gideon Mtagawa Amepongeza Jitihada Kubwa na Mafanikio yaliyopatikana Kupitia Mgeni Rasmi Aliyeweza Kuhamasisha Harambee Hiyo.

Ombeni Nanyi Mtapewa,Njooni Kwangu Msumbukao na Mnaolemewa Na Mizigo nami Nitawapumzisha.

Na: Gabriel Kilamlya (Njombe)

Kiwewe na Matumaini waokoka.

Kiwewe na Matumaini katika Pozi
MSANII wa Kundi la Ze Komedi, Robert Augustino ‘Kiwewe’ na mwenzake Tumaini Martin ‘Matumaini’ wameamua kuacha anasa na kumrudia Mungu kwa kuokoka.

Wakizungumza na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti, wasanii hao walisema kilichosababisha kuchukua uamuzi huo kwa wakati mmoja ni kutokana na manzingira waliyolelewa tangu wakiwa wadogo, yaani kumjua Mungu.

“Niliamua kufanya uamuzi sahihi ambao naamini utanibadilishia maisha yangu kwa kiasi kikubwa, kwa kufuata mambo yanayompendeza Mungu na siyo starehe za ujana,” alisema Kiwewe huku akiungwa mkono na Matumaini na wakabainisha kuwa kwasasa wanasali kwa Mchungaji Josephat Gwajima.

Wasanii hao walisema, ili kuhakikisha wanaungana na Mungu katika kila jambo, wameamua kuanzisha kundi lao la muziki wa Injili, lijulikanalo kama Comedians Gospel linaloundwa na wao pamoja na Mkono.

CHANZO: Grobal Publishers