Advertise Here

Thursday, March 7, 2013

Namna ya Kushinda Tamaa za Mwili.

Mwl. Patrick Sanga
Septemba 2011, Mwanafunzi mmoja wa shule ya Sekondari alinitembelea nyumbani kwangu hapa Dodoma. Alipofika nilimkaribisha ndani nikajua amekuja kunisalimia tu. Baada ya muda akaniambia kaka Sanga nina swali nahitaji msaada wako sana. Tukatoka nje mahala penye utulivu ndipo akaniambia tamaa za mwili kwa maana ya uasherati/zinaaa zinanitesa nifanye nini ili kushinda? Jambo hili linanitesa kiasi kwamba nahisi kama vile sijaokoka kutokana na vita niliyonayo katika fahamu zangu na mwilini mwangu.

 Kwa kuwa vijana wengi wamekuwa wakiuliza swali hili kwa namna tofauti tofauti na kwa njia mbalimbali, nimeona ni vema nikaliweka somo hili kwenye ‘blog’ hii  kwa kuwa tunao vijana wengi ambao changamoto hii inawakabili pia. Naam yafuatayao ni mambo ya msingi kuzingatia ili kijana aweze kuwa na ushindi dhidi ya tamaa za  mwili (dhambi) nk.
  • Kwa kutii na kulifuata neno la Mungu
Biblia katika Zaburi 119:9 inasema ‘Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako’. Ukisoma Mstari huu katika tafsiri ya Biblia ya Kiingereza ya GNB unasema How can young people keep their lives pure? By obeying your commands’. Mtazamo wa tafsiri hii ya kiingerza ni kujaribu kutafuta ufumbuzi wa namna ambayo vijana wanaweza kuishi maisha ya utakatifu na yenye ushuhuda. Inawezekana mwandishi huyu wa Zaburi aliona namna vijana wanavyohangaika katika eneo hili, ndipo ikabidi amuulize Mungu, ni jinsi gani kijana aisafishe njia/au anaweza kusihi maisha ya utakatifu? Kipengele cha pili kinatupa jibu la swali la kwanza kwamba ni kwa kutii, akilifuata neno lako.

Naam hii ina maana ni lazima kwanza kijana achukua hatue  ya kuliweka neno la Mungu moyoni mwake kwa wingi, maana hawezi kutii neno ambalo halimo ndani yake au hajalisoma na kulitafakari. Zaburi 119:11 inasema ‘Moyoni mwangu nimeleiweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi’. Maana yake ni kwamba, kama kijana atajijengea tabia ya kuhakikisha analiweka neno la Bwana moyoni mwake kwa kulitafakari kila siku, kwa vyovyote vile lazima atakuwa na ushindi dhidi ya tamaa za mwili na kazi zote za Shetani. Naam usiishie tu kuliweka moyoni mwako bali fuatilia sauti ya neno uliloliweka ndani yako, ukaiitii.
  • Kuacha michezo ya mapenzi na kuwa makini na nini unatazama/unasikia.
Michezo ya mapenzi (foreplay) ni maalumu kwa ajili ya wanandoa. Kwa bahati mbaya vijana wetu nao sasa wamekuwa wakifanya mambo haya ambayo kimsingi si yao. Michezo ya mapenzi ni sehemu ya vitendo vyvyote ambavyo hupelekea ashiki ya kufanya tendo la ndoa hii ni pamoja na kushikana shikana/kugusana maeneo mbalimbali ya mwili na pia kunyonyana ndimi.

Zaidi Katika dunia ya sasa Shetani ametumia teknolojia iliyopo kuteka fikra za vijana wengi. Vijana wengi kupitia simu, computer, video nk wanaangalia picha chafu za ngono na kusoma jumbe za aina hiyo kitu ambacho kinaharibu fahamu zao bila wao kujua. Na kwa kufanya hivyo wanakuwa wanayachochea mapenzi na kuamsha tamaa zao za mwili. Naam mambo haya ni hatari tena kinyume na mapenzi ya Mungu. Na kwa bahati mbaya vijana wetu tena waliokoka baadhi yao bado wamefungwa katika kufanya mambo haya.

Katika kile kitabu cha Wimbo Ulio Bora 2:7 Biblia inasema ‘Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe’. Kulingana na mstari huu tunajua kwamba, kumbe mapenzi yanaweza kuchochewa na kuamshwa, naam na hili ni jambo hatari sana kama litafanywa na wahusika ambao si wanandoa kwa maana ya (foreplay) hata kama wana kiroho cha iana gani.

Jambo la msingi kuepuka hapa ni kuwa kwenye mazingira ambayo yanaweza yakawashawishi kufanya mambo haya. Vijana ambao si wanandoa kutembeleana mahali wanaposihi kwa maana ya eneo ambalo wako pekee yao, au kwenda guest na  maeneo yote ya namna hii eti kwa lengo la kupanga mipango yenu. Fahamu kwamba kitendo cha vijana wawili ambao si wanandoa kukaa katika mazingira ya aina hii ni kumpa Iblisi nafasi ya kuwamaliza, naam kijana uwe makini usifanye ujinga huu, Shetani asije akakumaliza.
  • Kuenenda kwa Roho.
Mtume Paulo alikutana na kesi ya aina hii kwa wandugu wa kanisa la Galatia. Moja ya ufumbuzi juu ya suala hili aliwataka waenende kwa Roho ili wasisitimize kamwe taamaa za mwili. Wagalatia 5:16 ‘Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili’. Kuenenda kwa Roho kukoje? Ni kuishi/kuenenda kwa kufuata utaratibu/uongozi wa Roho Mtakatifu maishani mwako (Zaburi 32:8). Jambo la msingi ni kuwa mtiifu kwa Roho Mtakatifu, naam atakusaidia kushinda dhambi kama alivyomsaidia Bwana Yesu alipokuwa hapa duniani.
  • Kujitenga na marafiki/makundi mabaya
Zaburi 1;1 inasema ‘Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; Wala hakusiamama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha’. Jiulize muda wako mwingi unautumia kwa kufanya nini? Na kama ni marafiki ni marafiki wa aina gani?  Siku zote wale unaokuwa nao karibu wanachangia sana kujenga (kushape) mfumo wa maisha yako.

Biblia katika 1 Wakorinto 15:33 inatuambia ‘Msindanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema’. Naam kama utakuwa na marafiki wabaya basi tegemea na mazungumzo yao yatakuwa mabaya na hivyo tegemea na wewe kuwa na tabia mbaya. Jambo la msingi ni kujitenga nao usiende katika shauri lao, wala njia yao na pia kuketi katika baraza yao.

Mtume Paulo akizungumza na kijana wake Paulo alimwambia hivi ‘Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi’ 1 Timotheo 4:12. Wazo ninalotaka ulipate hapa ni kwamba kama Paulo angejua kwamba vijana hawawezi kuishi maisha ya utakatifu na yenye ushuhuda katika dunia hii, asingemwambia Timotheo afanye haya. Basi kwa kuwa alijua inawezekana, ndiyo maana Roho Mtakatifu alimwongoza kuandika haya ili kumwagiza Timotheo na sisi vijana wa leo katika jambo hili. Naam uwe kielelezo katika shule, chuo, kanisa, kazini nk ili Mungu aone sababu ya kuendelea kukutumia kwa utukufu wake.

Kama unataka KUOKOKA hivi sasa, Bofya Hapa
Neema ya Mungu iwe Nawe!

Mwl. Patrick Samson Sanga
+255 755 816 800

Huyu ndiye Adolph Robert Nzwalla.

Adolph Robert Nzwalla ni Kijana wa Kwanza kwenye Familia ya Marehemu Bishop Robert Nzwalla na Bishop Irene Nzwalla  kutoka katika kanisa la Hosanna Christian Centre lililopo Ghana, jijini Mwanza. Addo kama ajulikanavyo na wengi , anao wadogo zake wapatao wanne ambao ni Priscilla na Gladyce hawa ni mapacha na mdogo wao wa Mwisho anaitwa Joseph Robert Nzwalla.
Adolph Robert Nzwalla akipiga Keyboard wakati wa Ziara ya John Lisu jijini Mwanza
Adolph Nzwalla ni Mtangazaji  wa redio ya kikristo ijulikanayo kama  HHC Alive Fm yenye makazi yake maeneo ya Kirumba jijini Mwanza inayorusha matangazo yake kupitia  masafa ya 91.9 Fm. Tofauti na utangazaji Addo pia ni Music Director wa Hosanna Praise team ya Jijini Mwanza. Kwa muda mrefu sasa amekuwa akijishughulisha na muziki wa injili akiwa kama muimbaji, mpigaji na mshauri kwa makundi na matukio mbalimbali yafanyikayo jijini Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla.
Slim B
Adolph Nzwalla alianza rasmi kujishughulisha na muziki akiwa  mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Nyanza na baada ya hapo alijiunga na shule ya sekondari Mwanza(Mwanza Sec). Baada ya kumaliza elimu yake ya Sekondari, Addo alipata nafasi ya Kwenda kusoma Nchini Marekani katika Chuo cha Word of Life School of Ministry ambacho kiko katika Jimbo la Delaware na baada ya kumaliza masomo alirejea Nyumbani na kuunda kundi la Hosanna Praise Team ambalo ndilo anafanya nalo kazi hivi sasa Kama Music Director na Worship Leader wa kundi hilo.
 
Mwaka 2009 Addo alikuwa ni mmoja wa majaji  katika shindalo la Kusaka Vipaji kwa kanda ya Ziwa lijulikanalo kama “Zaburi Gospel Star Search” ambalo lilikuwa likirushwa na kituo cha Television cha Star Tv cha jijini Mwanza. Mwaka juzi Addo alikuwa miongoni mwa watumishi walio-organise ujio wa New Life Band katika jiji la Mwanza. Katika ujio huo kulifanyika Tamasha kubwa la kihistoria katika viwanja vya Furahisha lililohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Mwanza pamoja na mama Diana Mwakasege kutoka Arusha.
Adolph Nzwalla akirun show ya Cross Rythm ndani ya Hhc Alive Fm
Addo anauwezo mkubwa wa kupiga Gitaa la solo, Keyboard, drumz na tumba, lakini kwa muda mwingi huonekana akipiga keyboard. Katika Huduma hii ya Uimbaji amefanya Huduma na Waimbaji wakubwa kama Jackson Benty, John Lisu, Miriam Lukindo, Pastor David Yared pamoja na waimbaji wengi wa sifa na kuabudu. Katika jiji la Mwanza Addo amekua akiandaa na wakati mwingine kushirikishwa katika kuandaa matamasha mbalimbali ya kusifu na kuabudu.
Adolph Nzwalla akiongoza worship pamoja na mtumishi Ihano Nestory wakati wa ThanksGiving Concert
  Tazama Video hii ambapo Addo alikuwa aki'lead Wimbo wa Ahsante Yesu.

Wednesday, March 6, 2013

Hasara ya Kufanya Tendo la Ndoa kabla ya Ndoa.

Mwl. Patrick Samson Sanga
 Andiko la Msingi ni Mithali 5:1-20
"Mungu ndiye aliyewaumba mtu mume na mtu mke, akawaweka bustanini ili wamtumikie. Mungu akamuumba mwanadamu na kumpa viungo mbalimbali katika mwili. Akawapa wanadamu maungo maalumu kwa ajili ya tendo la ndoa na kisha akaliweka tendo la ndoa kuwa takatifu, tena la halali kwa wanandoa tu, tena hasa wale waliounganishwa na yeye."

Sasa katika kizazi cha leo tunaona watu wengi hasa vijana ambao bado hawajaoana (kwa maana ya kuwa wanandoa) vijana hao wanafanya tendo hilo la ndoa (ngono) tena kwa uchafu usio wa kawaida, wanafanya kwa kuzidi mipaka ambayo Mungu amempa mwanadamu, maana yake wanatumia isivyo (mis-use) maumbile/ maungo ambayo Mungu amewapa.

Soma warumi 1:24-27. Sasa wao wanapofanya haya hawajui kwamba kuna hasara kubwa wanayoipata na wao wanafikiri ndio wanakwenda na dunia. Lengo la ujumbe huu ni kukueleza hasara za kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa nazo ni;

(1)Ni dhambi
Kufanya ngono kabla ya ndoa ni dhambi na warumi 6:23a inasema mshahara wa dhambi ni mauti; na pia katika Ezekiel anasema Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa, hivyo kwa sababu hiyo hicho kitendo kitakusababishia kifo cha kimwili na kisha utahukumiwa tu na mwisho kutupwa jehnamu.

(2)Kuwashibisha wengine nguvu zako
Mithali 5:10 Tendo la ndoa ni tendo linalohitaji mtu atumie nguvu, hivyo kadri mtu (hasa mwanume) anapofanya  mara kwa mara anajipotezea nguvu zake anawashibisha wengine nguvu zake na hivyo dhoruba itamkuta katika ndoa yake pindi atakapooa kwa sababu hatakua na nguvu tena kama awali.

(3)Utavunjiwa heshima
Mithali 5:7, Siku zote yule unayefanya naye tendo la ndoa kwanza atakuona wewe ni mpumpavu kwa sababu anajua afanyaye tendo hilo hana akili kabisa (mithali 6:32) kwa hivyo atakudharau, zaidi atakutangaza kwa wengine na wewe mwenyewe pindi utapooa au kuolewa kwa kuwa nguvu zako uliwashibisha wengine basi utavunjiwa heshima na huyo mwenzi wako.

(4)Unafanya jambo litakaloiangamiza nafsi yako
Mithali 6:32. Nafsi kwa kiyunani inaitwa Psuche, ndani yake kuna hisia, akili na maamuzi ya mtu. Hivyo kuiangamiza nafsi yako ni kuangamiza future yako na mipango yako uliyokuwa umejiwekea ya mbele.

(5)Unajitengenezea majeraha na fedheha maishani
 Mithali 6:33. Sikiliza katika ngono unaweza ukapata kilema cha maisha, na magonjwa ya hatari kama vile kaswende, ukimwi n.k. Haya magonjwa yatapelekea nyama na mwili wako kuangamia utashindwa kufikia malengo uliyojipagia, utabakia kujuta tu na watu watakufanyia fedheha na wakati huo upo kitandani hujiwezi.

(6)Kuwapa wengine miaka yako
  Mithali 5:9 , Uchunguzi chunguzi unaonyesha kwa mtu anayependelea kufanya ngono mara kwa mara hasa anapoanza kabla ya ndoa mara nyingi hawezi kuishi kwa muda mrefu si hivyo tu lakini pia tumeona mara nyingi vijana wakijiua/wakiuana /wakifa kwa ajili ya mapenzi, wengine wanaugua hadi wanakufa wadogo na kupatwa na magonjwa mabaya, na hivyo muda waliostahili waishi hapa duniani na hivyo wanakuwa wamewapa wengine miaka yao.

(7)Kuvamiwa na maroho machafu
 Katika kufanya ngono, wengine wanaenda hadi kwa waganga wa kienyeji na wachawi na huko wengine wanapewa madawa ya ajabu ambayo yanapelekea kuwamiwa na mapepo ya ajabu, na wengine kwa kupenda ngono wamefanya ngono na majini bila wao kujua na tayari yamesha wamiliki na hawaji watatokaje kwenye kifungo hicho.

Mimi nimekuonyesha hasara zile za kibiblia tu, sasa zipo za kijamii, kitaifa, kifamilia nk. Naamini baada ya kuwa umesoma ujumbe huu, kama bado unafanya ngono basi utabadili tabia yako na kuacha ngono mpaka wakati utakapo fika na kama haujaokoka nakusihi uokoke ili Yesu akupe nguvu za kushinda hiyo dhambi.

Kama unataka KUOKOKA hivi sasa, Bofya Hapa
 Bwana Mungu akulinde na kukutunza.

Mwl. Patrick Samson Sanga
+255 755 816 800

Monday, March 4, 2013

Mambo ya Kuangalia katika Mvulana afaaye kuwa Mme.

 
JANA tulielezea Mambo ya kuangalia katika  Msichana afaaye kuwa Mke. Sasa leo tutazame Mambo ya kuangalia katika  Mvulana afaaye kuwa Mme.

Kabla Msicha yeyote hajatoa mkono wake kwa Mvulana, kwanza na ajiulize kama Yule mvulana wanayekaribia kuoana anafaa ama vipi. Mwenendo wake na tabia yake ya Siku zilizopita ilikuwa ya namna gani? Maisha yake ni Masafi? Upendo anioneshao unatoka Moyoni na Unaonesha heshima na tabia njema? Ama ni Upendo wa hivi hivi tu?

Anao mwenendo ambao utanifanya kuwa na Furaha? Mimi kama Mke nitaweza kuwa na Furaha niwapo kwake? Ataniruhusu kudumisha tabia yangu nzuri na kunipa Uhuru, ama itanilazimu kutupilia mbali yote na kuangukia katika Mamlaka yake?

Nikiwa nae kama Mme wangu, nitaweza kumuheshimu Mwokozi wangu kama Mkuu katika yote? Mwili na Roho, Matendo na Mawazo vitaweza kuhifadhiwa katika hali timilifu na takatifu? Maswali haya kama yakizingatiwa kwa Busara yatakuwa ya Manufaa sana katika Maisha yajayo ya Msichana anayetarajia kuolewa.

Kila Msichana anayetumainia kuwa na familia yenye furaha na Amani ambayo haitajua Udhaifu wala Huzuni katika siku za mbele na ajiulize Maswali haya kabla ya kutoa ukubali wake wa Upendo. 

Je! Mpenzi wangu ana Mama? Tabia ya Mama yake ikoje? Anatambua wajibu wake kwa Mama yake? Anajali Upendo na Furaha ya Mama yake? Ikiwa hajali wala Kumuheshimu Mama yake, Je! Kweli ataweza kuonyesha Heshima na Upendo, Wema na Usikivu kwa Mkewe?

Shani ya harusi itakapokwisha, atakuwa na Huruma kwa Makosa yangu ama atakuwa akinikosoa mara kwa mara akiwa Mgomvi na Mkali? Katika kuyajibu Maswali haya, shauku nyingi yaweza kupishia Mbali Makosa na Kasoro za Mchumba wako lakini Upendo wa kweli hautaficha Neno.

Mkubali afaaye kwa Tabia
 Katika kuchagua Mwenzi wa Maisha, Msichana na achague Mvulana aliye na Tabia na Mwenendo safi wa kibinadamu, aliye na bidii, Mwangalifu, Mwenye heshima, na aliye Mwaminifu na mnyoofu. Yule ampendaye na kumuogopa Mungu.

- Ellen G. White -

Saturday, March 2, 2013

Mambo ya kuangalia katika Msichana afaaye kuwa Mke.


VIJANA wengi wamekuwa wakikimbilia Ndoa pasipo kujua ni vitu gani vya Msingi wanatakiwa kuzingatia kabla ya kufika hatua ya Kufunga ndoa. Sasa leo tutazame Mambo ya Msingi ya Kuangalia katika Msichana afaaye kuwa Mke.

Kijana Mvulana na achague msichana ambaye atasimama imara kando yake na ambaye ataweza kuchukua sehemu yake ya mzigo wa maisha. Mke ambaye mvuto wake utamfanye mumewe kuwa na Heshima na kumwezesha kuwa na mwenendo mwema, na ambaye kwa ajili ya upendo wake, atamfanya kuwa na raha maishani mwake.

“Mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana”. Moyo wa mumewe humwamini……………! Humtendea mema wala si mabaya, siku zote za Maisha yake. Hufumbua Kimya chake kwa Hekima, na Sheria ya wema I katika ulimi wake. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; wala hali chakula cha uvivu.

Wanawe huondoka na kumwita heri, mumewe naye humsifu, na kusema binti za watu wengi wamefanya mema, lakini wewe umewapita wote. “Yeye apataye mke wa namna hiyo, apata kitu chema; naye ajipatia kibali kwa Bwana.

Hebu vijana na wajishauri kwa uangalifu mkubwa kuhusu mambo haya yafuatayo, na bila shaka kama yakizingatiwa kwa makini yatakuwa Msaada mkubwa kwa mvulana mwenye nia ya kuoa; Je! Yule unayekusudia kumuoa atafanya Nyumba yenu iwe na furaha? 

Yeye ni Mwangalifu awezaye kutunza Mali zenu? Au ni mtu ambae hutawanya Mali kipumbavu huku akionyesha Upendo wa Juu Juu tu? Mwenendo wake alionao ukoje kwa wakati huu? Anacho kitu chochote akitumainicho kwa wakati huu?

Nafahamu kwamba Mvulana ambaye ametumbukia katika Kisima cha Mapenzi, atayadharau Maswali haya kana kwamba hayana mana wala manufaa yoyote lakini hayana budi kufikiriwa kwa uangalifu Mkubwa iwezekanavyo.

Wakati wa kuchagua Mke, tafakari na uelewe tabia na Mwenendo wa Mwanamke unayetaka kumuoa, ili uone kama atakuwa Mstahimilivu na Mwenye bidii. Uone kama atachoka kuwatunza wazazi wako walio wazee wakati ule watakapokuwa wanahitaji Msaada wako.

Uone kama atakutenganisha nao na kukushawishi umpende yeye peke yake na kutumikia Starehe zake tu, na kukufanya uwasahau Baba na Mama yako ambao badala ya kupata binti, watakuwa wamepoteza Mwana. 

Kesho tutakuletea Mambo ya Kuangalia Katika Mvulana afaaye kuwa Mme.

 - Ellen G. White -