Bi. Christiane Taubira, Waziri wa sheria wa Ufaransa |
Watunga sheria wa Ufaransa
wamehalalisha ndoa za jinsia moja baada ya miezi ya mjadala mkali na
maandamano ya mitaani yaliyopelekea mamia kwa maelfu kwenda Paris.
Kura 331 dhidi ya 225 za siku ya jumanne zimeangukia kwa walio wengi ndani ya bunge ambao ni Socialist. Waziri wa sheria wa Ufaransa Christiane Taubira, amesema ndoa ya kwanza kufungwa itafanyika mapema mwezi june.
Wanaopinga sheria hiyo wanasema Ufaransa haiko tayari kuhalalisha ndoa za jinsia moja, na kura zinaonyesha kuwa wafaransa wamejitenga juuu ya swala hilo.
Mamia ya askari walimwagwa nje ya viwanja vya bunge kabla ya kura hizo kupigwa, kwa maandalizi ya kama kungekuwa na maandamano kuzunguka jengo la bunge na kando kando ya Mto Seine.
Ufaransa ni nchi ya 14 ya kuhalalisha ndoa za jinsia moja, na kura ya Jumanne imekuja wiki moja baada ya New Zealand kuruhu wanandoa wa jinsi moja kuoana.