Advertise Here

Saturday, June 15, 2013

Pastor Steven Wambura, James Kalekwa, Fred Msungu na Mc Pilipili wafanyika Baraka kwenye Kingdom Exploits.

Usiku wa Kuamkia leo katika Chuo cha Mt. Agustino-Mwanza, kulikuwa na Event iliyopewa Jina la Kingdom Exploits, iliyoandaliwa maalum kabisa kwa ajili ya Vijana waliopo chuoni hapo. Tukio hili lilianza Mida ya Saa 2:00 Usiku hadi Saa 5:00 Usiku huku Wanenaji wakiwa ni Bw. James Kalekwa-Mwanza, Fred Msungu-Dar na Mch. Steven Wambura-Dar.

Mchekeshaji wa Kimataifa toka Tanzania, Dar es salaam Bw. Emmanuel Mathias a.k.a Mc Pilipili alikuwepo Ukumbini hapo kuvunja mbavu za Wanafunzi wa Chuo hicho. Shughuli ilifanyika katika Ukumbi wa M10, na Praise Team iliyoundwa na Vijana wa Tafes, Casfeta, Huima na Uscf iliuongoza Umati wa Vijana waliokuwepo katika kuusogelea Uso wa Mungu.

Sasa tazama picha hizi uone jinsi Mambo yalivyokuwa chini ya Mc wa Event Bw. Barnabas Shija.
Mc wa Event Bw. Barnabas Shija
Wanafunzi waliohudhuria
Presentation ya Bw. James Kalekwa
Huyu jamaa hata kwenye Uimbaji yuko vizuri. Ni Fred Msungu

Bw. Fred Msungu akihudumu
Wakati wa Panel Discussion
Mc Pilipili akiingia kwenye Jukwaa tayari kufanya mambo yake
Mc Barnabas Shija akimtambulisha Mc Pilipili
Mc Pilipili baada ya kumaliza Show yake
Bw. James Kalekwa akihudumu katika Uimbaji
Pastor Wambura akiwaombea Wanafunzi wa SAUT
Kutoka Kushoto ni Barnabas Shija, Pastor Wambura na Mc Pilipili
Team Tukio
Kuanzia Kushoto ni Pastor Steven Wambura, Mc Pilipili, James Kalekwa, Billy, Fred Msungu, Adolph Nzwalla na Sowane Emmanuel.
= Utukufu Urudi Kwake yeye aliye Mkuu kupita Wote =