Advertise Here

Saturday, June 1, 2013

New Vine Christian Centre yaandaa Tamasha la Kusifu na Kuabudu.

Kanisa la New Vine Christian Centre lililopo Nyegezi Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Kiongozi Pastor Goodluck Kyara, limeandaa Tamasha la kusifu na Kuabudu lijulikanalo kama "Higher Praises" litakalofanyika June 9, 2013 katika Ukumbi Mkubwa wa Tema Hotel uliopo Nyegezi, Jijini Mwanza.

Tamasha hilo litaanza Saa 8:00 Mchana na kumalizika Saa 12:30 jioni, huku New Vine Praise & Worship Team ikiongoza Sifa na Kuabudu. Vikundi Mbalimbali vya Kusifu na Kuabudu pia Vimealikwa kama vile BCIC na MICC Praise & Worship Team.

Kwa Maelezo Zaidi waweza Kupiga Simu Namba: 0754 435951, 0712 113305.