Advertise Here

Friday, November 1, 2013

Historia ya Mwimbaji Kabula George.

Kabula George
Nimezaliwa miaka 30 iliyopita katika kijiji cha Kimiza Wilayani Kwimba mkoa wa Mwanza. Masomo ya elimu shule ya msingi nilipata Kimiza  mkoani Mwanza na baada ya haapo niliendelea na masomo ya sekondari jijini Dar es Salaam.
 
Huduma ya uimbaji nilianza nikiwa mdogo nikiwa kanisa la Romani kabla ya kujiunga na kwaya ya Uinjilisti ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Tabata Kinyerezi.

Mwaka 2005 ndipo nilianza rasmi uimbaji kama solo artis na kufanikiwa kurekodi albamu yangu ya kwanza iliyojulikanaa kwa jina la AMANI. Hata hivyo albamu hiyo niliifanyia marekebisha na kuamua kuirudia nikachukua nyimbo kama Nkomoji ulioimbwa kwa lugha ya Kisukuma wenye maana ya kombozi. MileleTanzania na Tunakulilia.

Niliongezea nyimbo nyingine na kuipa jina jipya la Pesa iki ikiwa na nyimbo 9 kama, Milele, Pesa, Ninamjua, Nkomoji, Tanzania, Tunakulilia, Yatima, Nakupa utuku na
Niguse.

Mwaka 2009 nilifanikiwa kutoka na albamu yangu ya pili iliyojulikana kwa jina la ‘Ushindi’ ikiwa na nyimbo nane ambazo ni Ushindi, Hakuna muweza, Tunaishi kwa Neema, Yerusalemu, Nikikumbuka, Dhihirisha, Yesu Wasitahili na Mshukuruni Bwana.

Mwaka 2011 nilifanikiwa kurekodi albamu yangu ya tatu inayokwenda kwa jina la Nitang’ara Tu, ikiwa na nyimbo sita ambazo ni Nitang’ara tu, Majaribu, Nimesogea, Nataka kumuona Yesu, Ni Mwema na Peleleza ikiwa katika mfumo wa DVD na iko sokoni.

Mbali na uimbaji pia namtumikia Mungu katika huduma ya kuhubiri na nimekuwa nikisafiri katika nchi mbalimbali kwa ajili ya kuimba na kuhubiri. Nina abudu katika Huduma ya Neno la Upatanisho (WRM) iliyochini ya Nabii Nicolaus Suguye.

Albamu ya Nitang’ara tu nimeamua kuiboresha tena kwani nataka kurekodi video mpya na nitaongeza baadhi ya nyimbo.

Katika albamu hii nitachukua nyimbo kama Nitang’ara tu, Majaribu, Nimesogea na Nataka kumuona Yesu, kisha nitachukua wimbo wa Pesa kutoka albamu ya kwanza na tatu kutoka albamu ya pili iitwayo Ushindi. Nyimbo hizo ni Tunaishi kwa Neema, Yerusalemu na Dhihirisha.

Sikiliza Wimbo wake huu ujulikanao Kama "Pesa"
Wasiliana na Kabula George kwa Namba zifuatazo:
+255 658 140 336
+255 757 140 336
Facebook: Kabula George