Advertise Here

Friday, November 8, 2013

Nyota wa Injili Nigeria tayari kwa Tuzo za MEGA.

Okposo
Mwimbaji Sammie Okposo
Kila kitu sasa kipo tayari kwa ajili ya Usaili wa Mwaka 2013 wa Tuzo za Muziki wa Injili za Nchini Nigeria zijulikanazo kama "Music & Entertainment Gospel Awards" - MEGA, Usaili unaofanyika Ijumaa ya leo katika Kituo cha "The Haven Event Centre" Kilichopo GRA Ikeja, Lagos - Nigeria.

Mwanzilishi wa Tuzo hizo za MEGA, Femi Akintunde Johnson (FAJ), anasema yeye pamoja na wenzake, wanafuraha sana kuanzisha Tuzo hizo Maalum kabisa kwa ajili ya Kutambua na Kusherehekea vipawa vya Waimbaji wa Nyimbo za Injili nchini Nigeria.

Hapa anasema, "Tunajua kuwa waimbaji wengi wa Nigeria wamekuwa wakikosa uzoefu katika kazi zao. Sasa kupitia Tuzo hizi, tumewaalika wanazuoni na wanataaluma mbalimbali juu ya Muziki kuja kuungana nasi ili kutengeneza Msingi mzuri kwa ajili ya Kuinua Muziki wa Injili Nchini Nigeria".

Kati ya Waimbaji wengi wanaotarajiwa kushiriki katika Tuzo hizo, pia wapo Sammie Okposo, Buchi pamoja na Sola Allyson. Huku viongozi mbalimbali wa Serikali na wa kidini wakishiriki pia katika Tuzo hizo.