Advertise Here

Sunday, November 10, 2013

Uzinduzi wa Live DVD ya GWT ni leo pale CCC Upanga.

KUNDI la Glorious Worship Team (GWT) linatarajiwa kuzindua DVD inayojulikana kwa jina la ‘Umenifanya Ibada’.

Kiongozi wa kundi hilo, Emmanuel Mabisa, amesema kuwa uzinduzi huo unafanyika leo katika ukumbi wa Kanisa la CCC Upanga jijini Dar es salaam.

DVD hiyo ambayo imerekodiwa ‘Live’ mwishoni mwa mwaka juzi, tayari ‘audio’ yake ilishatoka na kuwabamba wapenzi wa muziki wa Injili kutokana na nyimbo, sauti na mpangilio wa ala.

Mabisa amesema kuwa uzinduzi huo unasindikizwa na waimbaji wengine wa Injili wakiwamo Miriam Lukindo, The Next Level Team, Upendo Nkone, Florence Mureith kutoka Kenya, Rivers of Joy, Zion Band pamoja na kundi la Acapela The Voice.

“Hii ni albamu yetu ya pili, ya kwanza ilikuwa ‘Niguse’, na albamu hii ina nyimbo 14,” amesema Mabisa.

Amezitaja baadhi yake kuwa ni ‘Hakuna Rafiki, ‘Sogea’, ‘Nikubali’, ‘Nanyenyekea’, ‘Umedhihirika’, ‘Nimemuona’, na iliyobeba albamu ‘Umenifanya Ibada’.

“Nitoe wito tu kwa mashabiki wa muziki wa Injili, kujitokeza kuja kuona kitu cha tofauti, kwani sisi hatuimbi kwa CD bali tunafanya ‘live music’,” amesema Mabisa.