Advertise Here

Friday, November 1, 2013

Mtandao wa "The Kenyan Daily Post" umetoa Orodha ya Waimbaji na Watangazaji wanaomuabudu Mungu katika Roho na Kweli.


Mtandao wa The Kenyan Daily Post umetoa Orodha ya Waimbaji wa Nyimbo za Injili na Watangazaji wa vipindi vya Kikristo pamoja Radio za Kikristo wa Nchini kenya wanaomuabudu Mungu katika Roho na Kweli.

Utoaji wa orodha hii umetokana na Skendo mbalimbali zinazowakumba waimbaji wa Nyimbo za Injili, ikiwa ni pamoja na skendo za ngono, ulevi na kutanguliza pesa kuliko huduma.

Yafuatayo ni Majina yaliyoorodheshwa kwa Mujibu wa mtandao wa Kenyan Daily Post kuwa Watu hawa ndio wanaomuabudu Mungu katika roho na Kweli.

Watangazaji wa Radio na Tv
1.Njugush na Joyce Omondi (Kubamba)
Watangazaji wa Citizen Tv ambao kwa sasa wapo Masomoni.

2. Anthony Ndiema
mtangazaji wa Kipindi Maarufu cha "Tuzuka" cha KTN. Ni mume wa Mke mmoja na Kiongozi wa Kanisa huko Kenya, na ni Mtu ambaye ni wa kiroho zaidi.

3. Lawrence Thuku
Japokuwa si mtu maarufu sana, kipindi chake kinachorushwa na Radio isiyo Maarufu sana ya "Truth FM" kimekuwa kikigusa Maisha ya watu wengi. Hajawahi kusikika katika "Scandal" yoyote.

4. Faith Muturi (Cross-Over Chart)
Japokuwa amekuwa akitangaza kipindi hicho na watu wenye Scandal mbalimbali hasa za Kupenda pesa Dj Sadic na Dj Mo, ni Mtu ambaye yupo vizuri Kiroho na pia ni Kiongozi wa Kuabudu kanisani kwao.

5. Mwinjilisti Lucy Ngunjiri (Kameme FM)
Ni mtu ambaye pia yupo vizuri kiroho, na ni moja ya Watangazaji wenye wasikilizaji wengi sana. Sauti yake pindi anapokuwa kwenye Kipindi imekuwa ikiwaponya watu wengi pasipo hata kuwagusa.

Waimbaji wa Nyimbo za Injili
1. Daddy Owen
Amekuwa kwenye Tasnia ya Muziki wa Injili kwa Kipindi kirefu sasa, na ameweza kutunza heshima yake. Wimbo wake wa "Kapungala" ulimfanya ajulikane zaidi, na aliomba kabla ya kurekodi wimbo huo.

2. Rufftone
Huyu ni Baba wa tasnia ya Muziki wa injili Nchini Kenya, na hajawahi kutajwa katika "Scandal" yoyote ile kwa zaidi ya Miaka 10 ya Uimbaji wake. Rufftone ni kiongozi katika Kanisa analosali na Wachungaji wamekuwa wakimpenda sana kutokana na Kujiheshimu kwake.

3. Mr. Googz
Huyu aliacha kuimba Miziki ya kidunia na Kuamua kuanza kuimba muziki wa Injili na Kuja kuwa Mchungaji. Mr. Googz aliachia wimbo ujulikanao kama "Gospel Celebrity", Wimbo uliokuwa ukiwataka Waimbaji wengine wa Nyimbo za Injili kuacha kumkejeli Mungu. Ni Muimbaji ambao amekuwa akichukia sana dhambi.

4. Ben Githae
Ni Muimbaji ambaye aina ya Muziki wake umekuwa ukiwagusa sana watu wa Rika mbalimbali. Ni mtu ambaye anajali sana Ukristo na mara nyingi amekuwa akiombea sana watu wanaoenda kwenye kumbi za Miziki ya kidunia ili waokoke.

5. Solomon Mukubwa
Ni kiongozi wa Nyimbo za kuabudu na Mara nyimbo Nyimbo zake zimekuwa zikiwaponya watu pasipo hata kuwagusa. Aliomba sana na kufunga kwa miezi mitatu kabla ya kutoa wimbo wake wa "Mfalme wa Amani".

6. Gloria Muliro
Ni moja ya Waimbaji wenye Mafanikio makubwa sana nchini Kenya ambaye ameolewa na Mchungaji. Muimbaji huyu anamiliki Kanisa, na pia ana tabia ya Kuomba na Kufunga kabla ya kutoa wimbo wowote ule. Siku za Karibuni amekataa Ombi la Willy Paul ya kuimba kwenye wimbo wake kwasababu Willy Paul ni Muimbaji mwenye Scandal nyingi sana na hana hofu ya Mungu.

7. Eunice Njeri
Ni Muimbaji wa nyimbo za kuabudu na Mtu anaeweka mkazo sana kwenye Maswala ya wokovu. Kwake yeye kutengeneza wimbo, ni mpaka aende Milimani kuzungumza na Mungu ili ampe wimbo wa kutengeneza.

8. Mercy Wairegi
Naye pia ni Kiongozi wa Kuabudu, na Mtu pia anayejali sana Maswala ya Wokovu.


ZINGATIA: Orodha hii ni kwa Mujibu wa Mtandao wa The Kenyan Daily Post