Advertise Here

Friday, November 15, 2013

Mchungaji ajiua kwa kuhisi Mungu hayupo karibu nae.

Mch. Parker enzi za Uhai wake
Mchungaji mmoja kutoka Macon, Georgia wa Kanisa Bibb Mount Zion Baptist Church, Teddy Parker Jr amejiua kwa risasi baada ya kuhisi kuwa Mungu hayuko karibu naye.

Ilikuwa siku ya Jumapili, Mch. Teddy Parker Jr alipoamua kuwatanguliza mke na watoto wake wawili kanisani. Wakati wa kuanza ibada ulipofika, Mchungaji huyu hakutokea na kuacha waumini wakijiuliza kilichomtokea.

 Baada ya kusubiri kwa muda muhudumu wa kanisa hilo Russell Rowland alienda nyumbani kwake kujua kilichojiri na kukuta Mchungaji Parker amejipiga risasi na kuanguka nje ya nyumba yake. 

Alishangaa sana kwani alisema mchungaji huyo hakuwahi kuhubiri kuwa watu wajiue, na hicho ndicho kinachowachanganya zaidi.

Parker aliwahi kuwaambia waumini wake kuwa anahisi hayuko karibu na Mungu tena, na kila anapoendelea kuomba Mungu anaona kama Mungu hamsikii tena.

Mch. Parker aliwahi kusema, Najaribu kuomba lakini sihisi kama Mungu ananisikia. Najaribu kuhudumu lakini sioni kama Mungu ananitumia".

Parker akaendelea kusema kuwa kuna kipindi Mungu anaweza kuamua kutokukusikiliza lakini si kwa nia mbaya bali kukufanya wewe ujitegemee na kukomaa.