Advertise Here

Wednesday, November 13, 2013

AFLEWO Tanzania yakutanisha Wachungaji katika Pastors' Breakfast.

Mlezi wa AFLEWO Tanzania, Bishop Fredrick Kyara
Wachungaji wa Makanisa mbalimbali Jijini Dar es salaam wamekutana siku ya jana katika Hoteli ya Peacock Dar es salaam, huku kukutana huko kukiwa kumeambatana na chai ya asubuhi ya pamoja(Pastors' Breakfast) kwa lengo la kuwashirikisha Wachungaji hao Maono na Mipango ya huduma ya AFLEWO kwa Mwaka 2014, na kuomba ushiriki wao na washirika wao katika maadalizi kwa ajili ya Mkesha huo unaotegemea kufayika June Mwakani.

Kusanyiko hilo la Wachungaji limetokea siku chache kabla ya Uzinduzi wa usaili wa Mass Kwaya ambao utaanza Jumapili hii saa 9:00 mchana Katika Kanisa la City Christian Centre (CCC) Upanga jirani na Chuo cha Mzumbe, na Usaili huo utaendelea mpaka Januari Mwakani.

Kusanyiko hilo la Wachungaji liliongozwa na Walezi wa huduma ya AFLEWO Tanzania ambao ni Pastor Paul Safari (DPC), Bishop Fredrick Kyara (P.C.E.A St. Columbus), Mwenyekiti Geoffrey Obielo na Administrator wa AFLEWO Tanzania Anna Abella Munyagi.

Kwa mara ya kwanza Tanzania AFLEWO ilinza kwa rasmi Mwaka 2011 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, 2012 ilifanyika katika kanisa la City Christian Centre (CCC) Upanga, AFLEWO 2013 ilifanyika katika Kanisa BCIC Mbezi Beach, Mwaka 2014 inategemewa kufanyika mwezi wa sita tutakufahamisha mahala itakapofanyika.

Hivi ndivyo Pastors' Breakfast ilivyokuwa
Mlezi wa AFLEWO Tanzania, Pastor Safari kutoka DPC akizungumza Jambo
Kikao kikiendelea
Wachungaji mbalimbali wakisikiliza kwa Makini
Watumishi wa Mungu wakifuatilia kwa Makini
Mama Shegga akichangia Jambo
Bishop Mwende kutoka DPC
Kisha shughuli nzima ikatamatishwa kwa Maombi
Maombi yakiendelea
Kisha Wachungaji wakapata Picha ya Pamoja
ZINGATIA: Katika usajili wa Kwaya kwa Waimbaji, na wapigaji wa vyombo, Vigezo ni uwe umeokoka na uwe unajua Kuimba au Kupiga chochote cha Muziki. Karibuni sana kwenye Usaili!

Kwa Maelezo Zaidi, Wasiliana na Kamati ya AFLEWO Tanzania
+255 712 586 643
+255 757 332 062
aflewodar@gmail.com

- Habari & Picha, na Tunu Bashemela -