Advertise Here

Wednesday, November 13, 2013

Shusho kuwasha Moto Tamasha la "Nataka Nimjue".

Christina Shusho
MWIMBAJI wa nyimbo za Injili Tanzania, Christina Shusho, anatarajiwa kuwasha moto katika tamasha linalokwenda kwa jina la ‘Nataka Nimjue’.

Tamasha hilo linalofanyika katika ukumbi wa Kanisa la City Christian Centre (CCC), Upanga jijini Dar es Salaam Novemba 24, mwaka huu, limebeba video mpya ya muimbaji huyo ya wimbo huo wa ‘Nataka Nimjue’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Shusho alisema kuwa uzinduzi huo utakuwa wa kipekee na utasindikizwa na waimbaji wengine kama The Voice, John Lisu, Bahati Bukuku, Kinondoni Revival Choir, Joshua Mlelwa, Upendo Kilahiro, Amani Kapama, Paul Clement na wengineo.

Shusho alisema katika tamasha hilo ataimba ‘live’ bila kutumia ‘CD’ na kuwataka mashabiki na wapenzi wa muziki wa injili kujitokeza kumuunga mkono.

Tamasha hilo litakuwa la kwanza kwa msanii huyo kulifanya, tangu ashinde tuzo ya mwanamuziki bora ya "Africa Gospel Music Awards" kwa ukanda wa Afrika Mashariki.
Shusho anatamba na nyimbo mbalimbali kama vile ‘Nipe Macho’, ‘Wakuabudiwa’, ‘Mtetezi’ na nyinginezo.

- Happiness Mnale -