Advertise Here

Saturday, November 9, 2013

Kanisa laaswa kumtii Mungu.

Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania toka Moshi Michael Macha, amekemea matumizi mabaya ya mavazi kwa vijana huku akiwataka wazazi kuwalinda watoto wao ili wawe na maadili mema na kumtumikia Mungu. 
Mch. Michael Macha ameyasema hayo jana wakati akiongea na wananchi katika kata ya Malangali wilayani Mufundi katika Mkutano wa jimbo uliokutanisha waumini mbalimbali wa kanisa hilo na makanisa mengine uliofanyikia eneo la soko kuu la Malangali mjini.
 
Aidha Mchungaji Macha amesema kuwa waumini wa kikristo wanatakiwa kujihadhari na vitendo ambavyo vimekuwa vikishamili kwa sasa kama Ukahaba na ndoa za jinsia moja, na kwamba jambo hilo ni kumuasi Mungu.

-  Michael Ngilangwa -