Advertise Here

Sunday, November 10, 2013

Masanja awaongoza Sala ya Toba Mamia ya Wakazi wa Kahama.

Masanja akihubiri
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili ambaye pia ni Mchekeshaji Maarufu Emmanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji yupo Kahama kwa ajili ya Tamasha lijulikanalo kama 'Kahama Yote kwa Yesu".

Katika Tamasha hilo lililohudhuriwa na Waimbaji mbalimbali wa Nyimbo za Injili za Injili, Masanja pia alipata nafasi ya Kuhubiri pamoja na Kuimba katika Tamasha hilo.

Mamia ya Wakazi wa Kahama wamempokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yao baada ya Masanja kupiga Injili ya Ukweli katika Tamasha hilo, huku pia akipata nafasi ya Kuhudhuria Ibada ya siku ya leo katika Kanisa la EAGT Kahama.

Tazama Picha za Tamasha hilo lilivyokuwa


Watu wakimpa Yesu Maisha yao


Masanja akiombea watu waliompokea Yesu katika Kanisa la EAGT Kahama

- Picha Zote na Wlliam Bundala(Kahama) -