Advertise Here

Sunday, November 24, 2013

Lifahamu kiundani Kundi la "Beyond Vocal" kutoka Afrika Kusini.

Beyond Vocal
Beyond Vocal ni kundi lenye Vijana Watano wanaoimba Muziki wa Injili. Kundi hili Maskani yake ni Nchini Afrika Kusini, na Staili ya Muziki wao ni wa kuimba pasipo kutumia chombo chochote cha muziki(yaani Acapella), huku "Beat" ikitengenezwa kwa Midomo tu.

Kwa hapa nyumbani Tanzania Kundi hili la Beyond Vocal tunaweza kulifananisha na Kundi la The Voice Acapella, ambao nao huwa wanafanya Muziki wa aina kama hii.

Kundi hili la Beyond Vocal lilianzishwa Mwaka 2008, na Waanzilishi wa kundi hili ni Alex Granger, Lisanse Changwe, Mduduzi Dlamini ,Willard Sibande na Scelo Mhlanga.

Mpaka sasa kundi hili lina Album mbili. Album yao ya Kwanza ilikuwa ni "Trust In The Lord" na Album ya Pili inajulikana kama "Hold On", Kazi iliyofanywa chini ya Record Lebel ya "Spirit Music".

Waimbaji katika kundi hilo wamekuwa wakija na wengine kutoka na mpaka sasa kundi hilo linaundwa na Scelo Mhlanga kama "Lead", Mduduzi Dlamini kama "Bassist", Mbuso Vundla kama "1st Tenor", Nkosana Msimang kama "2nd Tenor/Baritone/Vocal Percussion", na Ntako Mosia kama "Baritone".
Beyond Vocal katika pozi
Kundi hili limepata nafasi pia ya ku'perform kwenye Jukwaaa moja na Waimbaji nguli mbalimbali kama vile Benjamin Dube, Solly Mahlangu, Ernie Smith, Brenda Fassie, Tshepiso, Andile B, Mari Michael, the late Isaac Mthethwa, Nathi Zungu, Dr Gumbi, na wengine wengi.

Pia wameshafanya ziara za Kimuziki katika Nchi mbalimbali kama Swaziland, Botswana, Zimbabwe pamoja na nyumbani Afrika Kusini.

Malengo Makubwa ya kundi hili la Beyond Vocal ni kuwa Huduma inayobadili Maisha ya watu, kwao wenyewe lakini pia kwa watu wengine.

Sasa hebu Tazama Video hii, Beyond Vocal wakiimba "Live" wimbo wa "Ndixolele" katika Show ya "expresso"