Advertise Here

Sunday, November 10, 2013

Mafuta ya Upako ya TB Joshua yamnusuru Muigizaji wa Nigeria.

nneoma
Nneoma Ukpabi akiwa na Mtoto wake ndani ya SCOAN - Nigeria
Muigizaji wa Kike toka Nigeria(Nollywood) Nneoma Ukpabi amefanikiwa kujifungua bila operesheni baada ya kutumia Mafuta ya Upako kutoka kwa TB Joshua wa SCOAN Nigeria.

Kulingana na Historia ya Kujifungua kwake, Muigizaji huyo Nneoma Ukpabi amekuwa akijifungua kwa Opesheni na mara hii baada ya kuambiwa na Madaktari kuwa hataweza kujifungua kwa njia ya Kawaida, Nneoma Ukpabi alianza maombi pamoja na kuchukua Mafuta ya Upako kutoka kwa TB Joshua.

Baada ya kuchukua Mafuta hayo, anasema alianza kuyatumia huku akitaja Jina la Yesu na baada ya Dakika 15 hatua ya kwanza ya Kujifungua ilianza ghafla na baadaye kufanikiwa kujifungua salama bila operesheni.

Nneoma Ukpabi sasa anafuraha baada ya kujifungua mtoto wa kike ambaye kwa sasa ana Umri wa Miezi miwili. Waigizaji wengine kutoka Nigeria ambao wameshawahi kufika kwa TB Joshua ili kupata Msaada wa Maombi ni pamoja na Enebeli Elebuwa, Camilla Mgberekpe, na Jim Iyke.