Advertise Here

Friday, February 22, 2013

Kadinali Timothy Dolan azungumzia Kashfa za kimaadili kanisa katoliki.

http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/7d84cef20b45c62c8b260e6d60216ea4_XL.jpg
Kadinali Timothy Dolan wa Kanisa Katoliki
 Kadinali Timothy Dolan ambaye ni mmoja wa maaskofu wanaotarajiwa kumrithi Papa Benedict wa XVI aliyejiuzulu hivi karibuni amesema kuwa kuanzia sasa watu wote wanaotarajiwa kuwa mapadri na maaskofu watakuwa wanachunguzwa tabia zao tokea utotoni.

Matamshi hayo yamekuja baada ya mchungaji mwingine mmoja wa mji wa Milwaukee ambao ni moja ya miji mikubwa ya jimbo la Wisconsin nchini Marekani kuwatumia vibaya kijinsia watoto wadogo. Kwa upande wake, Frank Lokoko, mtaalamu wa masuala ya sheria wa mji wa Milwaukee amesema kuwa, Kadinali Dolan alihojiwa kwa muda wa masaa matatu  na mawakili wa watoto waliotumiwa vibaya kijinsia na makasisi wa mji huo.

Amesema, Timothy Dolan alikuwa Askofu mkuu katika kipindi cha miaka ya 2002 hadi 2009 na ni mmoja wa makadinali 10 wanaowania nafasi ya kurithi kiti cha Papa Benedict wa XVI.

Ijapokuwa limekuwa ni jambo la kawaida kwa wakuu wa Kanisa Katoliki kufanya vitendo vichafu vya kijinsia huko Magharibi, lakini kuongezeka vitendo viovu vya ufisadi wa kimaadili na ubadhirifu wa fedha, vitendo ambavyo vimewahusisha hata viongozi wa ngazi za juu kabisa wa kanisa hilo, ni jambo ambalo limeyatumbukiza makanisa hayo ya Magharibi katika mgogoro mwingine mkubwa zaidi, tangu ule wa karne za kati wakati kanisa hilo lilipofanya mauaji makubwa ya watu kwa imani za kidini.

Watu wengi hivi sasa wamekuwa wakiyapa nguvu madai kuwa maaskofu wa kieneo na hata wa Vatican kwenyewe wanafanya kwa siri vitendo viovu vya udhalilishaji wa kijinsia na ni kwa sababu ndio maana maaskofu wa chini nao wakapata nguvu za kuwatumia vibaya hata watoto wadogo. Hali hiyo imejitokeza katika hali ambayo tangu miaka mingi nyuma, wachungaji walikuwa na heshima kubwa kati ya wananchi wa Magharibi.

Hata hivyo imani hiyo ya watu imepungua hasa baada ya kugunduliwa kashfa za kimaadili za wakuu wa Kanisa tena basi dhidi ya watoto wadogo. Takwimu zinaonesha kuwa watu wenye imani na Kanisa hasa kati ya wanawake, inazidi kupungua huko Magharibi huku idadi ya wanaokwenda kanisani nayo ikizidi kushuka chini.

Yamkini majibu ya sababu za kushuhudiwa hali hiyo yakawa yamo ndani ya matamshi ya Kadinali Martini ambaye hakuona tabu hata kidogo kutangaza malalamiko yake kuhusiana na utendaji mbaya wa Kanisa Katoliki. Kadinali Martini wa Milan, Italia, alikuwa askofu kwa muda wa miaka 20 na hata alitajwa kuwa ndiye Papa wa baadaye wa Kanisa Katoliki.

Alisema miaka michache kabla ya kufariki kwake dunia na katika mahojiano yake ya mwisho kwamba, Kanisa Katoliki liko nyuma kwa miaka 200. Alisema kama mabadiliko ya kimsingi hayatafanyika katika Kanisa Katoliki, basi kizazi kipya kitajitenga na kanisa hilo na kwamba mabadiliko hayo inabidi yaanze kwa Papa mwenyewe na kufuatiwa na maaskofu.