Advertise Here

Tuesday, February 19, 2013

Vitu vyenye thamani ya Millioni 3.5 vyaharibika kwenye Kanisa lililochomwa Moto huko Zanzibar.

LEO asubuhi vyombo vingi vya habari vimeripoti Juu ya Uchomwaji wa Kanisa la The Pool of Siloam la huko Zanzibar kwa kutupiwa vitu vilivyosababisha moto huo.

Jioni hii tumezungumza na Mchungaji wa Kanisa wa Kanisa hilo ambaye amethibitisha kuwa vitu vyenye Thamani ya Shilingi Milioni 3 na nusu vimeharibika vibaya na vyote vilikuwa upande wa Madhabahuni.

Aidha Mlinzi wa Kanisa hilo amesema kuwa, mida ya Saa 9 usiku aliona watu watatu wakipita karibu na Kanisa hilo na kutupia vitu viwili ndani ya Kanisa hilo upande wa madhabahuni na baada ya yeye kuona hivyo alikimbilia Upande wa pili na muda mfupi baadaye aliona moto ukianza kuwaka upande wa madhabahuni hivyo kuamua kumpigia Simu Mchungaji wa kanisa hilo.

Kwa Mujibu wa Maelezo ya Mchungaji huyo, tukio hili ni la pili kulikumba Kanisa hilo kwani lilishawahi kukumbwa na tukio lingine kama hilo.

Kwa Maelezo Zaidi, Sikiliza Kipindi cha Alive Fm Matukio leo Saa 2 Kamili Usiku kupitia Masafa ya 91.9Mhz kwa Wakazi wa Kanda ya Ziwa. Kama Uko Nje ya Mwanza, Sikiliza Hhc Alive Fm Online Kupitia; www.hhcalivefm.org