Advertise Here

Monday, February 11, 2013

Papa Benedict XVI atangaza rasmi kuachia madaraka.

Papa Benedict XVI
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict XVI ametangaza kuachia madaraka ya kuongoza kanisa ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, uamuzi ambao ni wa kwanza tangu karne ya 15 kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Habari la AFP.

Msemaji wa Papa, Federico Lombardi amesema kiongozi huyo wa juu kabisa wa Kanisa Katoliki duniani, ataachia ofisi rasmi tarehe 28 Februari, Mwaka huu saa mbili kamili asubuhi huku akiwa na Umri wa Miaka 85.

Wachambuzi mbalimbali wa masuala ya Vatican wanasema safari hii, kuna uwezekano mikoba ya Baba Mtakatifu Benedict XVI ikarithiwa na Kardinali kutoka Afrika.

Kardinali Peter Turkson wa Ghana ametajwa kama mrithi-mtarajiwa wa nafasi hii nyeti ndani ya Kanisa Katoliki, linalokadiriwa kuwa na waumini zaidi ya bilioni moja dunia nzima.

Mwingine ni Kardinali Francis Arinze; mzaliwa wa Nigeria ambaye alichukua nafasi ya Benedict XVI kama Kardinali-Askofu wa Velletri-Segni alipoteuliwa kuwa Papa miaka nane iliyopita.

- Mwananchi -