Advertise Here

Saturday, November 23, 2013

Mchungaji aapa kumlinda Mwanamuziki Justin Bieber.

Mchungaji Judah Smith(Kushoto) akiwa na Justin Bieber
Mchungaji mmoja wa Kanisa la "Washington-based City Church" Mchungaji Judah Smith amesema kuwa yupo tayari kumlinda Mwanamuziki Justin Bieber dhidi ya Vyombo vya habari zinavyomchafua Mwanamuziki huyo kila iitwapo leo.

Kauli ya Mchungaji Smith imekuja siku chache baada ya Ripota mmoja wa Hollywood kuandika Makala iliyodai kuwa Siku chache zilizopita Mwanamuziki huyo Justin Bieber alizini na Kahaba mmoja wa Kibrazili, huku Mchungaji Smith akidai kuwa Ripoti hiyo si ya kweli na ina lengo la kumchafua Justin Bieber.

Mchungaji Smith amemsihi Justin Bieber kutupilia mbali madai hayo na asonge mbele zaidi, huku akiwataka watu kumtazama justin Bieber katika Mtazamo mpana wa Mazuri anayoyafanya kuliko kumchafua kila siku.

Smith ambaye mara nyingi amekuwa akizungumza kwenye Vyombo vya Habari kwa niaba ya Justin Bieber, ni rafiki wa karibu wa Mama yake Justin Bieber ambaye walifahamiana naye Miaka mitatu iliyopita.

Katika kuhakikisha kuwa Justin Bieber anakaa kwenye Mstaari Mnyoofu wa Kimungu, Mchungaji Smith amekuwa akimtumia Mistari mbalimbali ya kwenye Biblia Justin Bieber kupitia Mitandao mbalimbali ya Kijamii.