Advertise Here

Saturday, November 23, 2013

Mwimbaji wa Nyimbo za Injili toka Nigeria Sammie Okposo atoa wimbo mpya.

Sammie Okposo
Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili toka Nigeria Sammie Okposo ambaye ameshinda Tuzo ya Mwimbaji bora wa nyimbo za Injili Nigeria, ametoa wimbo wake wa kwanza kutoka kwenye Album yake mpya anayotarajia kuzindua rasmi Mwakani mwezi wa April.

Kwa mujibu wa maelezo yake, wimbo huo mtu akiusikiliza kwa mara ya kwanza, anaweza akahisi kama sio wimbo injili kwani una "beat" inayokwenda kasi sana, hivyo kuueewa inahitaji mtu atulie na asikilize ujumbe uliopo kwenye wimbo huo.

Wimbo huo unajulikana kama "Who Tell You Say?", huku Okposo akisema sasa ni wakati wa kupeleka Injili katika Kumbi mbalimbali za Starehe ambako Injili haihubiriwi.

Hapa anasema, "Ni muda sasa kuhubiri Injili katika kumbi mbalimbali za starehe maarufu kama "Clubs" na maeneo mengine ambako Injili haihubiriwi. Injili haitakiwi kuhubiriwa makanisani tu, mana kuna watu walio nje ya makanisa na wanahitaji kuhubiriwa Injili".

Kabla ya kuzindua Album yake hiyo, Okposo amepanga kutoa Nyimbo mbili zilizopo kwenye Album yake hiyo mpya.