Advertise Here

Sunday, November 10, 2013

Donnie McClurkin atimiza Miaka 54.

Donnie McClurkin
Mwimbaji wa Kimataifa wa Nyimbo za Injili Donnie McClurkin Jana ametimiza Miaka 54 toka Kuzaliwa kwake Mwaka 1959.

Donnie alizaliwa na Familia ya Bw. Donald Sr na Mama Frances McClurkin mnamo Novemba 9, Mwaka 1959 katika Mji wa Copiague, New york na kukulia katika Mji wa Amityville.

Akiwa na umri wa miaka nane(8), mdogo wake wa kiume mwenye miaka miwili(2) aligongwa na gari na kufa papo hapo huku Donnie akishuhudia.Wakati Donne akiwa na majonzi mazito usiku huo huo ambao walimzika mdogo wake, mjomba wake alimbaka Donne.

Donnie ni moja ya waimbaji waliopitia Mambo magumu sana katika Maisha yake. Lakini Mch. Winans alimwalika Mcclurkin katika mji wa Detroit alikokua akiishi ili kumsaidia kuanzisha huduma(Kanisa) liitwalo Perfecting Faith Church.Miaka sita baadaye(1989). Donnie aliamua kuhamia Detroit na kuanza kufanya kazi na Pastor Winans.

Katika kipindi hiki ndipo Mcclurkin alipata wasaa wa kuzunguka sehemu mbalimbali na kufanya huduma akiwa chini ya Pastor Winans. Donnie anasema Familia ya Winans imekuwa karibu sana nay eye Kuanzia Bebe, Cece, na Pastor Marvin na wakat mwingine anafikiri yeye ni Donnie Mcclurkin Winans.

Mpaka sasa Donnie ameshinda Tuzo nyingi sana, na kati ya hizo ni Tuzo 3 za Grammy, Tuzo 10 za Stellar, Tuzo 2 za BET, Tuzo 2 za Soul Train, na Tuzo 1 ya Dove.

Happy Birthday Donnie McClurkin!!!