Advertise Here

Wednesday, November 27, 2013

Mwimbaji Solly Mahlangu wa Afrika Kusini kushiriki Tamasha la Chrismas.

Solly Mahlangu
MWIMBAJI Solly Mahlangu wa Afrika Kusini amekubali kutumbuiza kwenye Tamasha la Krismasi linaloandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurungenzi wa Msama Promotion, Alex Msama alisema mwimbaji huyo atakuja pamoja na waimbaji wake kwani anamiliki kikundi chake cha muziki wa Injili.

“Nashukuru maandalizi ya tamasha yanaendelea vizuri na naamini tamasha la mwaka huu litavutia kuliko yaliyotangulia kwani mwimbaji toka Afrika Kusini, Solly Mahlangu ambaye anaimba baadhi ya nyimbo zake kwa lugha ya Kiswahili amekubali kuja,” alisema Msama.

Baadhi ya nyimbo ambazo Solly Mahlangu ameimba kwa ludha ya Kiswahili ni Mwamba mwamba na Ee baba na zimewavutia waumini wengi hasa kwenye kuabudu.

Alisema ujumbe wa mwaka huu ni “Tanzania ni ya Watanzania, tutailinda na kuidumisha amani yetu.”

Msama alisema mwimbaji huyo anatarajia kushiriki katika tamasha hilo jijini Dar es Salaam, tamasha ambalo litafanyika pia katika mikoa ya Morogoro (Desemba 26), Tanga (Desemba 28), Arusha (Desemba 29) na Dodoma (Januari mosi).

Aidha, Msama alisema bado wanaendelea kufanya mazungumzo na waimbaji wengine yameshakamilika kwa waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania ikiwa ni pamoja na Solomon Mukubwa (Kenya), Ephraim Sekeleti (Zambia), Liliane Kabaganza (Rwanda).

Waimbaji wa Tanzania ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Edson Mwasabwite, New Life Band na John Lissu.

- Habari Leo -