Advertise Here

Tuesday, November 12, 2013

Papa akemea wanaofadhili Kanisa kwa Kuuibia Umma.

Papa Francisko
Papa Francisko amesema, ni dhambi kubwa kuwa mfadhili wa Kanisa kwa kuiibia serikali. Kufanya hivyo ni kuvaa sura mbili na hivyo ni kuwa kinyume na maisha ya Kikristu.

Papa amekemea wanaotoa msaada Kanisani kwa kutaka waonekanani Wakristu wema kwa kutumia fedha batili. Amesema, hakuna rushwa wala maisha bandia ya kujifanya kuwa Mkristu mwema lakini kumbe ni mtu wa hatari anayeliletea uchungu mkali Kanisa, yanayoweza kusafisha dhambi hiyo ya rushwa. Papa Francisko alieleza hayo wakati wa Ibada ya Misa , mapema asubuhi katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta

Alisema ni kweli sisi sote tuna dhambi, lakini ni lazima kujilinda dhidi ya Rushwa na ulaghai. Na hasa hatari ya kutaka kujionyesha kuwa ni muumini safi , mwenye kutoa msaada kwa kanisa na wahitaji kwa kutumia fedha ya wizi. Kuwaibia wengine, iwe kwa mtu binafsi au serikai au taasisi, na kutumia fdha hiyo kutoa msaada kwa kanisa.

 Papa anasema kufanya huko si haki, ni sawa na yule anayotoa rushwa ili ahudumiwe, huko ni kuvaa sura mbili katika maisha, ikiwa tofauti na maisha ya Mkristu aminifu.

Papa aliyarejea masomo ya siku ambamo katika Injili, Yesu anatutaka kuwa na moyo wa kusamehe wanao tukosea hata mara saba kwa siku, na kamwe bila kuchoka, inatuonyesha Yeye mwenyewe Yesu asivyochoka kutusamehe pale tunapotubu kwa dhati dhambi zetu.
Wakati Yesu anatutaka kusamehe mara saba kwa siku , alibaini Papa , tunaiona huruma ya Mungu kwa wakosaji.

Lakini pia kifungu hiki cha Injili Yesu anakanya kwa nguvu dhidi ya kuwa watu wachochezi na wazabina zabina na wala rushwa wanaokwaza wengine na kusababisha dhambi.Yesu, alismea, kuliko kumkwaza mmoja wa wadogo hawa, heri mtu huyo afungwwe jiwa la kusagia shingoni na kutupwa baharini.

Maneno haya ya Yesu yanatuonyesha jinsi ilivyo vibaya, kuwapotosha watu wengine katika njia za ukweli na aminifu . Papa alieleza na kuhoji, tofauti kati ya dhambi na rushwa. 

- Radio Vatican -