Advertise Here

Thursday, November 7, 2013

Papa awaita Maaskofu.

Papa Francis
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, ametuma waraka kwa maaskofu duniani kote kuomba mawazo yao kuhusu changamoto mbalimbali zinazolikabili kanisa la sasa, likiwemo suala la familia za kisasa na ndoa ya jinsi moja kama sehemu ya mageuzi makubwa katika mafundisho ya kanisa hilo yanayofanywa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na makao makuu ya kanisa hilo, dodoso hilo limetumwa kwa maaskofu kuwauliza kwa kina kuhusu hali nyingi mpya zinazojitokeza sasa, zinazopaswa kuangaliwa kwa umakini na kanisa kwa huduma ya kichungaji.

Mambo ambayo yalikuwa vigumu kujadiliwa na kusikilizwa hadi miaka michache iliyopita, yamejitokeza sasa kama matokeo ya hali tofauti kutoka.

Wachunguzi na masuala ya dini walisema dodoso hilo lina maswali 39 mengi yakiwa mambo ambayo kwa kawaida ni yale ambayo yalikuwa hayajadiliwi na kanisa hilo hadi miaka kadhaa ya karibuni.

Kujadiliwa kwa vitendo hivyo kunaweza kutafsiriwa kuwa ni ishara ya uwazi kuongezeka kwa huduma za kichungaji bila kujali historia ya muhimu kama ilivyokuwa zamani.

Akizungumzia kuhusu ndoa za mashoga, Papa katika waraka huo amenukuliwa akiuliza swali “ni uangalizi gani makini wa kichungaji unaopaswa kutolewa na kanisa kwa watu waliochagua aina hiyo ya maisha?” 

Pia kwa muungano wa ndoa za jinsi moja ambazo wamepata watoto kwa njia ya kuwarithi, anauliza “nini kifanyike kwa familia za aina hii kwa busara ya kichungaji ili kupeleka mwanga wa imani kwao.”

Aidha, kuhusu kuoa au kuolewa tena wanandoa waliopewa talaka ambao chini ya sheria ya sasa hawaruhusiwi kupokea komunio takatifu, dodoso linauliza kama wanahisi kuwa wametengwa au wanakabiliwa na tatizo gani kutokana na kutokuwepo uwezekano wa wao kupokea sakramenti.

Kuhusu talaka, dodoso limehoji maaskofu waseme wanakabiliana vipi na hali hiyo kwa busara za kichungaji kwa kazi za kila wanapokumbana na tatizo hilo.

Hoja ya talaka inatarajiwa kuwa mojawapo ya mambo ya kujadiliwa na kanisa katika Sinodi ya Maaskofu mwaka 2015, kwa hiyo kutajwa katika dodoso hii kumetafsiriwa kama maandalizi ya sinodi ili ifikapo mwaka 2015 kanisa liweze kuunda miongozo ya kufanya kazi katika huduma za kichungaji katika ngazi ya mtu mmoja mmoja na katika ngazi ya familia.

Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu, Lorenzo Kardinali Baldisseri, aliwaambia waandishi mada ya mkutano huo kuwa sinodi ni nzuri na inaonyesha vizuri zaidi bidii ya kichungaji ambayo Baba Mtakatifu anataka mbinu mpya za kutangaza injili kwa familia katika dunia ya leo. 

- Tanzania Daima -