Advertise Here

Wednesday, November 6, 2013

Jabu Hlongwane na Mthunzi Namba kutoa Album ya pamoja.

http://www.showbizone.co.za/images/stories/news/JabuMthunzi.jpg
Pastor Jabu Hlongwane(Kushoto) na  Mthunzi Namba(Kulia)
Baada ya Miaka mingi kupita katika Utendaji wa Projects mbalimbali zilizowaweka kwenye Nafasi moja, Wachungaji Jabu Hlongwane na Mthunzi Namba wa Afrika Kusini sasa wameamua kufanya Album ya pamoja.

Waimbaji hao nguli wa Muziki wa Injili kwa sasa wapo studio wakimalizia vionjo vya Mwisho mwisho tayari kabisa kwa ajili ya kuachilia Album hiyo katika Msimu huu wa Sikukuu.

Waimbaji hawa waliofahamika zaidi kupitia kazi yao kubwa ndani Kundi la Muziki wa Injili la Afrika Kusini lenye Mafanikio makubwa Joyous Celebration, watatoa Album yao hiyo kupitia kampuni ya Sony Music Entertainment.

"This collaborative project was just bound to happen sooner or later," alisema Pastor Jabu Hlongwane. Waimbaji/Waandishi/Watayarishaji na Waanzilishi hawa wa kwanza wa Joyous Celebration wamekuwa Marafiki kwa zaidi ya Miaka 25 sasa.

"I believe in my heart that the time is right for this project," aliongeza Mthunzi Namba, na kuongeza kuwa huu ni Wakati wa Mungu, na wao wako tayari.

Album hiyo yenye Jumla ya Nyimbo 20 inatarajiwa kutoka Mwanzoni mwa Mwezi wa 12, huku Mwimbaji mwingine Siphokazi akitajwa kushirikishwa katika album hiyo.