Advertise Here

Thursday, October 31, 2013

Mwimbaji Peter Kaberere wa Kenya asherehekea Miaka 4 ya Ndoa yake.

Kaberere akiwa na Mkewe Njesh
Mwimbaji wa Nyimbo za Kusifu na Kuabudu Peter Kaberere wa Nchini Kenya, leo October 31, 2013 anasherehekea Miaka 4 ya ndoa yake na Mkewe Njesh Kahuru. Wawili hawa walifunga ndoa October 31, 2009 kwa kula kiapo Kanisani huko Kitusulu, Kenya.

Mara ya kwanza kukutana kwao, walikutana katika Tamasha la Muziki huko Mombasa, Kenya wakati Kaberere akiwa katika ziara ya kimuziki.

Huu ni wimbo wa Peter Kaberere ujulikanao kama "Nisamehe"

Mwimbaji Namatayi Chipanga wa Zimbabwe achaguliwa Kushiriki Tuzo za "Women in Enterprise".

New and celebrated music couple, Charles and Namatayi Chipanga, are back in the limelight
Namatayi akiwa na Mumewe Charles Chipanga
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka Zimbabwe Namatayi Chipanga amechaguliwa kushiriki katika Tuzo za Heshima za “Women in Enterprise Awards" za Nchini Zimbabwe, Tuzo zitakazotolewa kesho huku Mgeni Rasmi katika Tuzo hizo akiwa ni Mwanamke Mfanyabiashara kutoka Afrika Mashariki Gloria Serobe.

Mwenyekiti wa Dawati la Wanawake la "Zimbabwe National Chamber of Commerce" Divine Ndlukula amesema Tuzo hizo zina lengo la kuwatunuku Wanawake waliofanikiwa katika Shughuli zao.

Namatayi alizaliwa Livingstone, Zambia na ameolewa na Mwimbaji Charles Chipanga. Licha ya Upekee wa Sauti yake, pia Namatayi ni Mwimbaji mwenye Mafanikio Makubwa sana Nchini Zimbabwe katika Tasnia ya Muziki wa Injili Nchini Zimbabwe.

Tazama moja ya Kazi za Namatayi akiwa anaimba LIVE Wimbo wa "Gore Rangu" yeye pamoja na Mumewe Charles Chipanga

Tamasha la Krismasi kufanyika Uwanja wa Taifa.

Bw. Alex Msama
TAMASHA la Krismasi 2013 limepangwa kufanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Desemba 25.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama, ilieleza awali mikoa sita iliomba kuwa mwenyeji wa tamasha hilo, lakini kamati yake imeteua Dar es Salaam iwe ya kwanza.

“Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Krismasi imeamua lifanyike Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, halafu Desemba 26 tutatizama mkoa mwingine. Tunaomba mashabiki wetu waendelee kutuunga mkono,” alisema Msama.

Alisema awali walipokea maombi kutoka kwa wadau mbalimbali wa muziki wa Injili nchini wakiomba lifanyike katika mikoa yao, ambayo ni Mbeya, Mwanza, Arusha, Dodoma, Dar es Salaam na Shinyanga.

Tamasha la Krismasi linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Pasaka kila mwaka.

Kwa mujibu wa Msama, wanataka Tamasha la Krismasi liwe bora zaidi kuliko la Pasaka kwa kualika wasanii maarufu kutoka nje na ndani ya Tanzania.

Alisema hilo ni tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu na litakuwa na tofauti kubwa kulinganisha na mengine yaliyowahi kuandaliwa na kampuni yake.

- Tanzania Daima -

Wednesday, October 30, 2013

Mchungaji Rwakatare atengwa.

MBUNGE wa Viti Maalumu, Mchungaji Getrude Rwakatare (CCM) wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, ametengwa katika Ushirikiano wa Makanisa baada ya kanisa lake kulalamikiwa kufungisha ndoa inayodaiwa kukiuka taratibu za kikanisa, kisheria na kimaadili, Tanzania Daima Jumatano limejulishwa.

Ndoa inayolalamikiwa kufungishwa na kanisa hilo ni ile iliyoibuliwa na gazeti hili wiki iliyopita ambayo inamhusisha Mbunge  wa Viti Maalumu, Rosweeter Kasikila (CCM) mwenye umri wa miaka 60 na kijana Michael Christian wa miaka  26.

Ndoa hiyo ambayo ilifungwa katika kanisa hilo Septemba Mosi mwaka 2011, imebaki kuwa gumzo na kuwaacha hoi baadhi ya mawaziri, wabunge pamoja na majirani wanaoishi jirani na mbunge huyo mjini Bagamoyo, Pwani.

Akizungumza siku ya jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Haki za Jamii ya makanisa hayo, Mchungaji William Mwamalanga, alisema uamuzi wa kulitenga kanisa la Mama Rwakatare umetokana na kikao cha Kamati ya Maadili iliyokutana jana jijiji Dar es Salaam.

Alisema Kanisa la Mchungaji Rwakatare halifai kuendelea kuwa katika ushirika huo kutokana na kubariki ndoa hiyo aliyodai kuwa ni batili.

Mchungaji Mwamalanga alisema utaratibu wa ndoa katika makanisa unafahamika, ikiwa ni pamoja na wafungaji wa ndoa kutakiwa kutangaza ndoa hiyo hadharani kwa kipindi cha wiki tatu.

“Ndoa hii haikutangazwa hadharani, kibaya zaidi inasemekana imefungwa ndani ya ofisi na sio kanisani. Hiyo haiwezi kuitwaa ndoa maana haijakidhi vigezo na taratibu za kikanisa, ni lazima Mchungaji Rwakatare awajibike,” alisema.

Alisema lazima nyumba za ibada zikubali kutogeuzwa kichaka cha kusaidia uovu kama ilivyofanywa na kanisa hilo la Mikocheni B kwa kukubali kufanikisha ndoa hiyo kinyume cha taratibu.

“Tunalaani ndoa hiyo kuanzia mawio hadi machweo kwa kuwa hata maandiko ya kitabu kitakatifu cha Biblia kinawathamini yatima kama alivyo huyo kijana Michael anayeonekana kutoafiki ndoa hiyo kwa matakwa yake,” alisema mchungaji huyo.

Alisisitiza kuwa wanamtenga Mchungaji Rwakatare na kanisa lake kwani amewachafua  na kuyatia aibu makanisa mengine yote nchini.
Mchungaji huyo pia alimtaka Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete kuwaengua kwenye chama hicho Mchungaji Rwakatare na Kasikila kuhusiana na ndoa hiyo.

“Rwakatare ni mtunga sheria, anajua wazi kuwa ndoa inatakiwa pia kubandikwa katika ubao wa matangazo. Ni wazi kuwa wameamua kuvunja sheria na kutenda kosa la jinai,” alidai.

Mwamalanga alisema kuwa kwa hatua hiyo ndoa hiyo ni batili na haramu kwa kuwa ni aibu pia kwa mtoto kumuoa mwanamke mwenye umri wa mama yake.

Katika hatua nyingine, mchungaji huyo alisema umoja wao unafanya kila iwezalo kuhakikisha kijana Michael anarudishiwa vyeti vyake ambavyo kwa sasa vimezuiliwa na Mbunge Kasikila.

Pia aliitaka Kamati ya Maadili ya Bunge kuwaita na kuwahoji wabunge hao kwa kitendo chao cha kuhalalisha ndoa hiyo kwani kimeutia doa muhimili huo.

Alisema Bunge ni sehemu tukufu, hivyo Rwakatare na Kasikila hawana hadhi ya kukaa huko, hivyo alishauri waenguliwe.

Alipopigiwa simu kueleza msimamo wake juu ya uamuzi wa umoja wa makanisa hayo kumtenga kwa kuhalalisha ndoa hiyo, Mchungaji Rwakatare aling’aka na kukata simu.

Alipopigiwa tena simu yake ilizimwa na hakuweza kupatikana tena hadi tunaenda mitamboni.

- Tanzania Daima -

Kanisa la FPCT Sengerema latoa Mafunzo Maalum kwa Vipofu.

Kanisa la FPCT Kata ya Disabageni, Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza, limetoa Mafunzo maalum kwa watu wasioona ili waweze kusoma Neno la Mungu.

Kwa Taarifa Kamili tuungane na Reporter wetu Peter Maresa kutoka Sengerema

Askofu Mkuu apinga wazo la kuwapa viongozi wa Makanisa silaha.


Bunduki na risasi.
Bunduki na Risasi
ASKOFU Mkuu wa kanisa la Redeemed Gospel nchini Kenya Arthur Kitonga amepinga wito wa baadhi ya mapasta kutaka serikali iwape bunduki ili kujikinga kutokana na mashambulizi katika makanisa.

Akiongea na Taifa Leo kwa njia ya simu kutoka Amsterdam Jumanne, Askofu Kitonga alikariri msimamo wa kanisa lake kuhusu suala hilo ambalo  limezua mjadala katika vyombo vya habari huku wananchi wengi wakionekana kutofurahia pendekezo la mapasta.

Mashambulizi ya mara kwa mara na watu wasiojulikana hasa katika sehemu za Mombasa na Kilifi yamepelekea kuuawa kwa mapasta wawili hivi majuzi akiwemo pasta wa Kanisa la Redeemed kwa jina Charles Matole.

Katika mazishi ya Pasta Matole, viongozi wa makanisa waliilaumu serikali kwa kutowalinda vilivyo na kuitaka Serikali iwape bunduki aina ya AK47 ili wajikinge kutokana na mashambulizi ya adui.

Askofu Lambert Mbela ambaye ni Kiongozi wa kanisa la Redeemed Gospel eneo la Pwani Kaskazini alinukuliwa akiitaka serikali iyakabidhi makanisa bunduki aina ya AK47.

Lakini hapo Jumanne Askofu Kitonga alipinga jambo hilo na kusema huo sio msimamo wa kanisa.

“Tunapiga jambo la watumishi wa Mungu kupewa bunduki. Jambo hilo  halifai,”akasema Askofu Kitonga kwa njia ya simu.

Askofu huyo mkuu aliahidi kutoa maelezo zaidi kuhusu jambo hilo pindi tu atakaporejea nchini kutoka kwenye ziara yake ya Australia.

Mwito wa mapasta kujihami umezua mjadala mkali kwenye vyombo vya habari huku wengi wakisema ni kinyume na mafundisho ya Biblia  na maandili  ya Kikristo.

“Kama Wakristo hatufai kumwaga damu. Mwito wa mapasata kupewa bunduki una maana watatumia bunduki hizo kuua kinyume na amri kumi za Mungu,”akasema shabiki mmoja huku akichangia kwenye mjadala katika kituo kimoja cha Redio Jumanne.

Wengi wa waliochangia katika mjadala huo walinukuu maandishi matakatifu yanayopendekeza kutolipiza kisasi na kumwachia Mungu kupambana na maadui zao.

Amri za Mungu
Mnamo wiki jana Askofu Kitonga pamoja na viongozi wengine wapatao 200 kutoka kwa madhehebu mbalimbali ya Kiijilisti walikutana mjini Nyeri na kutoa mwito  kwa serikali izidishe usalama katika makanisa.

Viongozi hao wa makanisa walisikitishwa na ukosefu wa usalama nchini na makanisani  na wakaitaka serikali ichunguze wageni walioko nchini  kunyume cha sharia huku wakisema huenda wageni hao ndio wanaosababisha visa vya uhalifu kuongezeka.

Hata hivyo, Askofu Kitonga na wenzake hawakuitisha bunduki mbali walisema ni jukumu la serikali kuwalinda wananchi wote ikiwepo  ni pamoja  na viongozi wa makanisa.

- Swahili Hub -

Tuesday, October 29, 2013

Emmy Kosgei ashinda Tuzo ya BEFFTA.

Emmy Kosgei akiwa na Annie
Mwimbaji maarufu wa Nyimbo za injili toka Nchini Kenya Emmy Kosgei Ijumaa iliyopita alipata Tuzo ya "Best International Gospel Act", Tuzo iliyotolewa na BEFFTA (Black Entertainment Film Fashion Television and Arts) iliyofanyika huko U.K.
Emmy Kosgei
Emmy Kosgei akiwa anaingia Ukumbini hapo
Emmy Kosgei ambaye amefunga ndoa kipindi kifupi kilichopita na Mtume Anselm Madubuko wa Nigeria, alikuwa Russia kihuduma baada ya Kutoka Honeymoon ya Ndoa yao, na Mwaka huu kwake umekuwa ni Mwaka wa Baraka sana.
Emmy Kosgei akipokea Tuzo yake
Kupitia ukurasa wake wa Facebook Emmy Kosgei kaandika Maneno haya It is here ladies n gentlemen... The BEFFTA AWARD 2013. 'Best International Gospel Act ‘! Home safely! This is ur award. .. Thanks for voting n support. , we give all the glory to God!!! He has done it for us again … May God bless u n have a blessed week ahead...lov yall!

Pia katika Orodha ya Washindi yupo Anne Kasiime kutoka Uganda aliyeshinda Tuzo ya "Best Comedian".

Kanisa la TAG kuanzisha Benki.

Askofu Barnabas Mtokambali
KANISA la Tanzania Assemblies of God (TAG) lipo katika mchakato wa kuzungumza na wasomi ili kuanzisha benki yao.

Hayo yalielezwa na Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Barnabas Mtokambali, wakati akizindua jengo jipya la Kituo cha Uamsho na Umisheni lililopo Msasani.

Mtokambali alisema haiwezekani wakakosa wasomi wenye mioyo ya kusaidia kanisa hilo kuanzisha benki, hospitali na chuo kikuu.

“Sisi tuna uwezo wa kuanzisha chuo kikuu kupita hata kile cha Dodoma na hospitali kupita ile ya KCMC na jambo hili linawezekana kabisa kama kutakuwa na lengo na nia katika hilo,” alisema Mtokambali.

Askofu huyo alisema si vema nyumba za ibada kutumika kwa kufanya biashara na mambo ya siasa.

Mchungaji wa kanisa hilo Mashariki Kaskazini, Samson Swila, alisema jengo hilo limegharimu sh milioni 146 hadi kukamilika kwake, na kuongeza kuwa wamekabiliana na vikwazo vingi lakini Mungu aliwasimamia.

- Tanzania Daima -

Monday, October 28, 2013

TB Joshua atabiri kutekwa kwa Kiongozi Afrika Mashariki.

Nabii Tb joshua
Nabiii TB Joshua wa SCOAN Nigeria ametabiri kutekwa kwa Kiongozi wa nchi moja ya Afrika Mashariki.

Utabiri huo ameutoa kwenye Ibada ya Jana huku akiwataka wana'Afrika Mashariki kuomba sana juu ya hili ili lisitokee.

Utabiri wa TB Joshua mara nyingi umekuwa ukitimia. Je! kwa hili mambo yatakuwaje???

Hebu Tazama clip ya Video hii akitoa Utabiri huo

TD Jakes: Don't Let the Good Times Fool You - Part 1

Biashara ya Madawa ya Kulevya, Viongozi wa Dini wataja Majina 61.

Viongozi wa dini wametaja majina 61 ya vinara wanaojihusisha na dawa za kulevya nchini ambao wanatarajia kuwaburuza katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), mjini The Hague, Uholanzi kujibu tuhuma zao.

Majina hayo yametajwa na Kamati ya Maadili na Haki za Jamii kwa Viongozi wa Dini na Wananchi nchini, ambapo miongoni mwao wamo wabunge wa majimbo na viti maalum, mawaziri, viongozi wa dini na wafanyabiashara.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kipendekoste, William Mwamalanga, alisema kuwa, majina hayo yalipatikana Jumanne wiki hii kupitia mkutano wa siri wa viongozi wa dini wa madhehebu ya kiislam na kikristo 134 kutoka Tanzania Bara, Zanzibar na Pemba.

Mkutano huo ambao ulifanyika kwa siku mbili kuanzia Oktoba 21, mwaka huu hapa jijini Dar es Salaam uliwakilishwa na viongozi wawili wa dini kila mkoa isipokuwa Rukwa ambapo hapakuwa na mwakilishi.

Alisema ulifanyika kwa siri ili kutotoa mwanya wa kuingiliwa na mifumo isiyo rasmi ambayo ingevuruga adhima yao.

Kuhusu upatikanaji wa majina, mchungaji huyo alisema ulitokana na utafiti walioufanya ndani na nje ya nchi.

Pia alisema taarifa nyingine walizipata kupitia kwa wasiri wao kutoka ndani ya jeshi la polisi nchini na vyanzo mbalimbali vya habari kutoka nje ya nchi.

Akizungumzia mkutano huo, alisema lengo lake lilikuwa ni kutathmini biashara za dawa hizo ambazo alieleza ni tishio linaloangamiza kwa kasi kubwa vijana na kusababisha nchi kuingia kwenye aibu duniani.

Mchungaji Mwamalanga alisema katika mkutano huo walitoka na maazimio mawili likiwamo la kuwafikisha mahakamani wahusika na kufanya kampeni za siri kupita kwenye majimbo sita ya wabunge (majina tunayo) waliotajwa.

Alisema lengo la kampeni hiyo ni kuwaeleza wananchi tabia za wawakilishi wao ili mwaka 2015 waweze kuchagua viongozi bora wenye uchungu na nchi yao, wakereketwa wa amani na watakaochochea watu kujituma na kufanya kazi kwa bidii.

Alisema wakati wa uchaguzi mkuu wawakilishi wa mkutano huo, watapita tena majimboni kuwataja wahusika kwa majina.

Kuhusu viongozi wa dini ambao nao wametajwa kujihusisha na biashara hiyo, mwenyekiti huyo alisema, mkutano umewataka wafuate mfano wa Mchungaji Donald Mwakisambwe wa kanisa la Kiinjili la Kipentekoste nchini, ambaye aliacha kwa ridhaa yake.

Aidha, kamati hiyo imetoa siku 71 kuanzia Jumanne ya wiki hii kwa wahusika wote 61 kujisalimisha wenyewe kwa Rais Jakaya Kikwete.

“Wakati mchakato wa kuyapeleka majina haya ICC ukiendelea tunawataka wahusika wajisalimishe kwa Kikwete kwa kuwa orodha hii tuliyonayo (akitaja majina yao) ni miongoni mwa wale waliotajwa kwenye orodha aliyokabidhiwa Rais wakati ule, wakijisalimisha tutajua kupitia wasiri wetu,” alisema na kuongeza:

“Vinara hawa ambao Watanzania wamekuwa wakiwaita ‘vigogo wa dawa za kulevya’ hawapaswi kuitwa jina hili, hawa ni wahuni na wauaji, tusiwape majina mazuri ambayo yanawatukuza ndiyo maana biashara hii inakuwa kwa kasi,” alisema.

Kuhusu Watanzania 175 waliokamatwa nchini China ambao wanasubiri adhabu ya kunyongwa na wengine waliowahi kukamatwa nchi nyingine duniani alisema, utafiti waliofanya unaonyesha kuwa wengi wao hutumwa na wakubwa hapa nchini na kuahidiwa fedha nyingi.

- Nipashe -

Sunday, October 27, 2013

Yaliyojiri kwenye Usiku wa Uamsho pale CCM Kirumba.

Usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi ulikuwa ni Usiku wa Uamsho yaani Revival Night. Usiku huo wa Kusifu, Kuabudu, Maombi na Maombezi ulifanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, Usiku uliondaliwa na Tafes Mkoa wa Mwanza kwa Kushirikiana na Radio ya Kikristo ya Hhc Alive Fm(91.9Mhz) ya Jijini Mwanza.

Ulikuwa ni Usiku wa Baraka sana kwani mbali ya maombi mbalimbali pia kulikuwa na Maombi maalum Juu ya Taifa letu la Tanzania, huku watumishi wa Mungu mbalimbali wakifundisha Neno la Mungu akiwemo Askofu Eugene Murisa wa Kanisa la Highway of Holiness Cathedral la Ilemela Mwanza, huku Ma'Mc wa Event hiyo wakiwa ni Sowane Emmanuel na Albert Francis.

Vikundi Mbalimbali vya waimbaji na waimbaji binafsi walihudumu huku Jackson Benty kutoka Arusha akihudhuria pamoja na kuhudumu katika Mkesha huo wa Kipekee kufanyika chini ya Tafes Mkoa wa Mwanza.

Sasa Mambo yenyewe yalikuwa hivi
Tafes Praise Team ya Mkoa


Revival Mission Band
Kihayile group
Tafes Saut Dadaz
Askofu Eugene Murisa
Ma'Mc Sowane Emmanuel(Kushoto) na Albert Francis(Kulia)
Askofu Murisa akihubiri
Askofu Murisa akiombea watu waliofika Uwanjani hapo
Jackson Benty akihudumu
Mr. Madaha(M/Kiti Tafes Mkoa wa Mwanza)
Viongozi Kamati ya Maandalizi
- Utukufu urudi kwake yeye aliye Mkuu kupita wote -

Hatimaye Samuel Sasali afunga ndoa na Milembe John.

Jana ilikuwa ni siku ya kufunga ndoa kwa Bw. Samuel Sasali a.k.a The Blogger na Bi. Milembe John Madaha.

Sasa haya ni Matukio katika Picha jinsi tukio zima lilivyokuwa
Sam Sasali akimvisha Pete Milembe
Milembe akimvisha Pete Sam Sasali
Hapa wakionesha Vyeti vyao vya Ndoa
Wakitoka Kanisani
Kisha shughuli nzima ikahamia Ukumbini
Mr. & Mrs. Samuel Sasali
So Beautiful
Handsome Men
Ukweni
Ukweni
Prosper Mwakitalima akitoa Zawadi kwa Maharusi
Blogger Jimmy akitoa Zawadi
Tunawatakia Maisha Mema na yenye Furaha na Baraka Tele.

- Uncle Jimmy -

Friday, October 25, 2013

Facebook na Watumishi wa Mungu leo.

Askofu Mwanyika afariki Dunia.

Askofu Mstaafu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe, Raymond Mwanyika amefariki dunia jana mkoani Njombe.

Askofu Mwanyika alizaliwa mwaka 1930 huko kijiji cha Uwemba-Njombe, baada ya makuzi na majiundo yake ya kiroho na kimwili alipata daraja takatifu la Upadre 11/10/1959.

Mnamo 16/01/1971 Baba Mtakatifu Paulo VI alimteua kuwa Askofu wa Njombe, na 25/04/1971 alisimikwa kuwa Askofu rasmi wa Jimbo la Njombe.

June 8 2002 Askofu Mwanyika alipumzika na nafasi yake kuchukuliwa na Askofu Maluma. Askofu Mwanyika amekuwa Padre kwa miaka 54 na Askofu kwa miaka 42.


Atakumbukwa kwa majitoleo yake katika kuwahudumia watu wa Njombe bila kujali tofauti zao za kiimani,alikuwa mstari wa mbele katika kuendeleza huduma za jamii kama hospitali na shule, huduma za maji na umeme katika maeneo mengi ya Njombe, Makete mpaka Ludewa.

Anatarajiwa kuzikwa 29/10/2013 ndani ya Kanisa katoliki la Njombe(Njombe Cathedral).

Bwana alitoa na Bwana ametwaa,jina lake lihimindiwe
Ameeeeeen!

- Jamii Forum -

Thursday, October 24, 2013

Askofu mbadhirifu afukuzwa Kanisani Ujerumani.

Askofu mbadhirifu afukuzwa kanisani Ujerumani
Vatican imemfuta kazi Askofu mmoja mbadhirifu wa Ujerumani. Makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani yamesema kuwa Vatican imechukua hatua hiyo kutokana na kiongozi huyo wa kanisa kufanya ubadhirifu.

Askofu Franz-Peter Tebartz-van Elst amefutwa kazi kwa kufanya ubadhirifu wa mamilioni ya fedha za Kanisa. Kabla ya hapo, askofu huyo alikuwa analalamikiwa sana kwa kufanya ubadhirifu na watu walikuwa wanataka afukuzwe kwenye Kanisa Katoliki.

Katika taarifa yake, Vatican imesema kuwa, Kanisa Katoliki limemfukuza kwa muda Askofu Franz-Peter Tebartz-van Elst wa Limburg, Ujerumani. Taarifa zinasema kuwa, askofu huyo ametumia karibu Euro Milioni mbili na laki tisa kwa ajili ya kujenga makazi yake, fedha ambazo zilitoka kwenye mfuko wa kodi za masuala ya kidini wa Ujerumani.

Askofu huyo mwenye umri wa miaka 53 analaumiwa pia kwa kutumia Euro Milioni 31 kujengea eneo la Kanisa katika mji wa kale wa Limburg wakati gharama ya ujenzi wa eneo hilo ulikuwa ni Euro Milioni 5.5.

 - Iran Swahili Radio -

Tuesday, October 22, 2013

Askofu: Waliofungwa China walijitakia Kifo.

Askofu Mkuu Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi mkoani Kilimanjaro, Isack Amani
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi Mkoani Kilimanjaro Isack Amani
ASKOFU Mkuu Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi mkoani Kilimanjaro, Isack Amani amesema watanzania 175 wanaoshikiliwa nchini China, kwa tuhuma za kufanya biashara ya dawa za kulevya, serikali haiwezi kuwaombea msamaha, kutokana na kutokuwa na mamlaka na serikali ya China.

Alisema hayo mwishoni mwa wiki, wakati akizungumza kwenye sherehe za mahafali ya kwanza ya kidato cha nne ya shule ya Sekondari St. Amedeus, inayomilikiwa na Kanisa Katoliki jimbo la Moshi, pamoja na kuzindua jengo la maabara ya sayansi.

Alisema serikali hawezi kuwaombea msamaha wa kutonyongwa watanzania wanaoshikiliwa kwenye magereza ya nchini China, kwani hawezi kuingilia sheria za nchi nyingine.

Alisema hakuna wa kulaumiwa, endapo watanzania hao watanyongwa, kwani wao ndio waliojitakia. Alieleza kuwa watuhumiwa hao wanatambua sheria za nchi hiyo vizuri, kwamba endapo mtu akikamatwa na dawa za kulevya, lazima anyongwe.

“Serikali haiwezi kuwaombea msamaha watanzania 175 wanaoshikiliwa nchini China kwa dawa za kulevya, sheria za nchi hiyo walizijua hivyo walijitakia wenyewe, pia serikali yetu haina mamlaka kwenye sheria za China,” alisema Askofu Amani.

“Hakuna umuhimu wa serikali kuwaombea wasinyongwe, wamejitakia wenyewe kifo kwani wanajua vyema kule kuna sheria kali, na sisi hatuna mamlaka na huko hivyo serikali yetu haina cha kufanya,”alisema.

Alisema serikali wakati ikishererekea miaka 50 ya uhuru inapaswa kutatua tatizo la ajira kwa kuweka mazingira mazuri kwa vijana ili wasiweze kujiingiza kwenye matukio ambayo yanawagharimu uhai wao.

Akofu Amani alifafanua kwamba wakati serikali ikipigana na adui maradhi, ujinga na umaskini, pia itambua upougonjwa wa dunia wa uaminifu na kutojali amri za Mungu, maadili katika jamii, hali inayosababisha taifa kuyumba kutokana na kukosekana kwa haki.

- Habari Leo -

Monday, October 21, 2013

Harusi ya James Kalekwa na Frida Madenda.

James Kalekwa na Frida Madenda wakiwa wenye Furaha baada ya kuvishana Pete
Jumamosi ya Juzi ilikuwa ni Siku ya Harusi ya Bw. James Kalekwa na Frida Madenda iliyofanyika Mkoani Dodoma.

James Kalekwa ni Mwanataaluma, Mwandishi wa Vitabu na Mwalimu wa Neno la Mungu. Pia amekuwa akifundisha kupitia Mtandao huu kila siku za Jumatatu.

Unaweza kusoma Mafundisho ya James Kalekwa ya Jumatatu iliyopita kwa Kubofya Hapa

Hizi ni Baadhi tu ya Picha za Harusi ya Bw. James Kalekwa na Frida Madenda

Kwa tukio hili, leo hatutakuwa na Mafundisho ya James Kalekwa, Kwa Mafundisho yake mengine tembelea Mtandao huu Jumatatu Ijayo.

Mtandao huu unawatakia Maisha Mema yenye Furaha na Baraka tele.

Sunday, October 20, 2013

Kanisa Dar lachomwa Moto.

Kanisa la Baptist Vingunguti
KANISA la Baptist, lililoko Vingunguti jijini Dar es Salaam limechomwa moto usiku wa kuamkia Jana ambapo vitambaa na madhabahu vimeteketea kwa moto.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Marietha Minangi amesema kuwa, tukio hilo limetokea usiku wa saa nane, na hadi anazungumza na mwandishi, hakuna mtu aliyekuwa amekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Kamanda Minangi alisema, ilikuwa mapema mno kuhusisha tukio hilo na tofauti za imani za kidini. Alisema, polisi wanaendelea na uchunguzi.
 
Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo, Hezron Mwaisemba alimwambia mwandishi wa habari hizi kanisani hapo, kuwa wakiwa wamelala usiku kama saa nane na robo hivi, binti mwenye umri wa zaidi ya miaka ishirini aliwaamsha na kuwaambia kuwa, ameambiwa kanisa linawaka moto.

“Tuliamka na kuelekea kanisani, tukakuta kweli kanisa linaungua. Yule binti alituambia aligongewa dirisha na motto wa jirani akamwambia kuwa kanisa linawaka moto. Basi, tulipofika hapa tukakuta meza moja pamoja na ile ya madhabahuni vimeteketea kabisa.

"Tulikuta kisu na kiberiti na pembeni pale kulikuwa na moto walikusanya maboksi wakayachoma, naona lengo lilikuwa kuteketeza kabisa jengo hili. Kwa bahati nzuri tulifanikiwa kuzima moto kwa kutumia mchanga,” alisema Mchungaji Mwaisemba.

Mchungaji huyo alisema kuwa, tangu kanisa hilo lijengwe mahali pale mwaka 1992 limekuwa na uhusiano mzuri na majirani, hivyo wameshangazwa na kitendo hicho.

“Sijui huyo mtu au watu waliofanya kitendo hiki walikuwa na sababu gani. Sisi hapa tuna uhusiano mzuri sana na jamii yote hapa Vingunguti,” alisema.

Mchungaji huyo alisema kuwa, thamani ya vitu vilivyoungua moto inaweza kufika shilingi 200,000/=.

Hata hivyo, Mchungaji Mwaisemba alilalamika kuwa, ukiacha tukio hilo la kuchomwa moto kanisa lake lenye waumini wapatao 150 linakabiliwa na matukio mengi ya wizi, ambapo watu wasiojulikana wamekuwa wakifika kanisani hapo usiku na kuiba vitu mbalimbali ikiwemo viti vinavyotumiwa na watoto wa shule ya awali inayomilikiwa na kanisa.
 

The Next Level Album Launching.

Tazama walichokifanya Glorious Worship Team kwenye Campus Night - Saut.

October 18, 2013 ilikuwa ni Siku ya Usiku wa Kusifu na Kuabudu ujulikanao kama Revival Flames Campus Night ndani ya Chuo Kikuu cha Mt. Augustino, na Moja ya Vikundi vilivyohudumu ni Glorious Worship Team kutoka Dar es salaam.

Sasa tazama Video hii uone watu walivyokuwa Wakimsifu Masiha wakiongozwa na GWT toka Dar es salaam

Saturday, October 19, 2013

Yaliyojiri kwenye Revival Flames Campus Night ndani ya Saut - Mwanza.

USIKU wa kuamkia leo, ulikuwa ni Usiku wa kusifu na Kuabudu Maarufu kama Revival flames Campus Night iliyoandaliwa na Tafes Saut - Mwanza Campus na kufanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Nyamalango kuanzia Mida kama ya Saa 3:00 Usiku na Kumalizika Mida kama ya Saa 10 usiku.

Vikundi mbalimbali vya Kusifu na Kuabudu vilihudumu katika Mkesha huo kama Vile Tafes Saut Praise & Worship Team, Tafes Choir, Huima Choir, n.k huku Neno la Mungu likitolewa na Pastor elisha Msanifu kutoka Kanisa la Highway of Holiness Cathedral lililopo Ilemela Jijini Mwanza.

Mbali ya vikundi hivyo kutoka chuo cha SAUT Mwanza, pia kundi Maarufu Maarufu la Glorious Worship Team(GWT) kutoka dar es salaam pia lilipata fursa ya Kuongoza sifa katika Usiku huo.

Sasa Tazama namna mambo yalivyokuwa Viwanjani hapo
Watumishi wa Mungu wakiwa Viwanjani hapo
Tafes Praise Team On Stage




Sasa mida kama ya Saa 7 hivi wakaingia glorious Worship Team na Mambo yakawa hiviiii...
Kwenye Mic ni Paul Clement



Emma Solo wa GWT

Sifa na Utukufu zirudi kwake yeye aliye Mkuu kupita wote Mbinguni na Duniani.

- Picha zote na Elia Migongo -