James Kalekwa |
Kisa mkasa (Scenario) #2
Mchezo wa mpira wa miguu bila
magoli
Kama wewe ni mpenzi, mshabiki au mfuatiliaji wa mchezo
wa mpira wa miguu basi uanelewa fika juu ya muundo wa viwanja vya mchezo huo…
Moja ya vitu muhimu sana kwenye ujenzi wa kiwanja ni milingoti minne mikubwa
isimamayo pande mbili tofauti (zinazokabiliana) za uwanja. Bila shaka umekwisha
baini ya kwamba ninazungumza kuhusu magoli.
Hebu fikiri, mchezo wa mpira wa miguu pasipo magoli
uwanjani… Je, inawezekana kuwa na mchezo huo? Hata ule mpira wa “mchangani”
huwa na magoli, hata kama ni ya mawe au vijiti…
Hauwezi kuwa mpira wa miguu
bila magoli. Hebu jiulize wachezaji wangekuwa wanakimbiakimbia uwanjani,
wanapiga chenga, wanapeana pasi, wanakaba/wanazuia mashambulizi… ili iweje
sasa???
Kuna umuhimu gani wa kuwa na mchezo wa mpira wa miguu pasipo magoli?
Lengo kuu la mpira wa miguu ni magoli. Ukiyatoa
malengo hayo, umeondoa maana, umeondoa thamani iambatanayo na mchezo huo.
Kabla hatujachukua hatua kubwa sana katika kujifunza
haya, ninaomba tujenge uelewa wa pamoja juu ya maswala kadhaa ambayo yana uhusiano
wa moja kwa moja na maswala mazima ya malengo.
Kusudi – ni sababu kuu ya kuwepo kwako. Hii hujibu
swali la “Kwanini ninaishi?” mfano:
Ninaishi ili kuudhihirisha utukufu wa Mungu kwenye kizazi changu.
Maono – ni taswira/picha kubwa uionayo juu ya mwisho wa
maisha yako. Ni mkusanyiko wa mwisho wa maisha yako. Hii hujibu swali la
“ninakwenda wapi?” mfano: … Kumtukuza
Mungu kwa kufanya ugunduzi, uvumbuzi na utatuzi chanya wa mahitaji ya kizazi
changu.
Dhamira – ni namna gani utafanya ili kuyafikia maono
hayo kivitendo. Hii hujibu swali la “Namna gani nitatekeleza?” Mfano: … Kufungua taasisi ya utafiti wa
uwezo wa mwanadamu na uelimishaji wa vijana.
N.B Unaweza kuwa na dhamira zaidi ya moja… Hakuna ukomo
ilimradi tu dhamira zinafanikisha ufikiaji wa maono yako.
Malengo/Mipango – ni kuweka namna/njia za kivitendo na
zinazopimika ili kufanikisha dhamira yako/zako Mfano: … Kufanya usajili wa taasisi yangu ifikapo March 28 ili
kuanza utendaji rasmi.
Mkakati – ni mchanganuo wa hatua kwa hatua na uratibu wa
rasilimali ili kufanikisha malengo yako. Hii hujibu maswali mengi “Nifanye
nini, nifanye wapi, wakati gani?...” Mfano:
…
Mkakati
wa usajili wa taasisi:
#
|
Jukumu
|
Yatakayohitajika
|
Kinachotarajiwa
|
Muhusika
|
Lini
|
Hali
ya utendaji
|
Kuandika katiba ya taasisi.
|
Katiba ya taasisi
|
Frida
|
1-23 January, 2014
|
Inaendelea
|
||
Kualika wajumbe waanzilishi na kuwashirikisha wazo
|
Kikao/mkutano wa kwanza
|
James
|
28 January, 2014
|
Bado
|
||
Kufanya shughuli za usajili wa taasisi
|
Cheti cha usajili
|
Charisa & Joshua
|
19 February, 2014
|
|||
Kutoka kwenye mkakati huu unaweza kutengeneza bajeti
(maelezo juu ya uratibu wa rasilimali fedha).
Lengo la kuainisha, walau kwa ufupi tu, tofauti ya
mambo hayo ni ili uwe na uhakika na kitu gani unakiendea na unapaswa kufanya.
Ni muhimu sana ufahamu ya kwamba kusudi ndilo huwa sababu ya maono; maono huzaa
dhamira (utume) na dhamira ndiyo huleta malengo ambayo huzaa mikakati tayari
kwa utekelezaji. Ili kurahisisha uelewa juu ya mambo haya, tazama na kujifunza
kwenye Taswira ifuatayo:
Mafundisho haya yameandaliwa na James Kalekwa
Mwanataaluma, Mwandishi wa vitabu na Mwalimu wa Neno la Mungu
+255 714 762 669
+255 754 917 764