Advertise Here

Monday, February 10, 2014

Mwimbaji Jimmy Gait akana shutma dhidi yake juu ya Video yake mpya.

544714_334676729923469_868042671_n
Jimmy Gait
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka Nchini Kenya jimmy Gait amekataa kuomba radhi kwa kutoa Video yake Mpya ijulikanayo kama "Makekes" aliyomshirikisha Papaa Dennis. Hatua hiyo imekuja baada ya baadhi ya Watangazaji na Madj kukataa kucheza wimbo wake kwenye Vituo mbalimbali kwa Madai kuwa hawajapendezwa na Mavazi ya Wadada kwenye video hiyo na pia Wimbo huo una ujumbe mdogo sana.

Akijibu Madai hayo Jimmy Gait amesema kuwa haoni umuhimu wa kuomba radhi kwani anaamini hakuna jambo baya katika Video hiyo na kuwa hayo ni mapinduzi katika Muziki wa Injili, kwahiyo hakuna alichokosea.

Video hiyo iliyotengenezwa Nchini Afrika Kusini chini ya kampuni kubwa ya Godfather Production, imegharimu Ksh. Million 1.

Tazama Video hiyo