Advertise Here

Tuesday, September 11, 2012

Semina ya Mwl. Christopher Mwakasege sasa kufanyika Viwanja vya jangwani na si Biafra.

Mwl. Christopher Mwakasege

MTUMISHI wa Mungu Mwl. Christopher Mwakasege anatarajia kufanya Semina ya Neno la Mungu Jijini Dar es salaam Mwezi huu wa 9 kuanzia tarehe 23 -30 katika Viwanja vya Jangwani.

Taarifa za awali zilisema kuwa Semina hiyo ingefanyika katika Viwanja vya Biafra, mahali ambapo huwa anafanyia Semina zake mara kwa mara, lakini kupitia Ukurasa wake wa Facebook Mwl. Christopher Mwakasege amethibitisha kuwa Semina hiyo sasa itafanyika katika Viwanja vya Jangwani, na si viwanja vya Biafra kama ilivyotajwa hapo awali.

Hapa Mwalimu Christopher anasema; "Bwana Yesu Asifiwe. Najua wengi mmeulizia semina ya Arusha na Dar es salaam itafanyika lini, tarehe za semina ya Arusha na Dar ni hizi; 9-16 Sept 2012- Arusha, Uwanja wa reli na tarehe 23-30 Sept 2012- Dar-es- Salaam, Uwanja wa Jangwani Mungu awabariki."

Mbali ya semina hizo pia amesema kuwa wakati Semina hizo zikiendelea, kutakuwa na Semina za Vijana walioko Vyuoni, Shule za Sekondari na Walioko Majumbani.

Mwl. Mwakasege anasema; "
Wakati wa semina ya Arusha na Dar es salaam kutakuwa na kipindi cha vijana wa chuo, sekondari na walioko nyumbani siku ya jumamosi tarahe 15/9/2012 kwa Arusha(uwanja wa reli) na 29/9/2012 kwa Dar es salaam(uwanja wa jangwani) kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa sita mchana. Mungu awabariki sana na tunashukuru kwa maombi yenu na tunaendelea kuwaombea."