Advertise Here

Sunday, November 11, 2012

Askofu Anglikana ataka wacheza kamari watoe Sadaka.

Askofu Justin Welby

ASKOFU Justin Welby, aliyeteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana, yaani Askofu wa Canterbury, amependekeza kwenye mtandao wa Twitter kwamba mtu yeyote aliyeshinda kwenye kamari kwa kubahatisha kuwa yeye ndiye atateuliwa, anafaa kutoa fedha hizo kama sadaka kwa kanisa.

Mwanzo wa juma hili makampuni ya kamari yalitangaza kuwa yamesimamisha kamari juu ya nani atakuwa kiongozi mpya wa kanisa la Anglikana, kwa sababu wengi walifikiri kuwa ni Askofu Welby, ambayo inaonesha baadhi ya maafisa wakijua kuwa jina hilo ndilo lilopendekezwa.

Askofu Welby atachukua nafasi ya Rowan Williams mwaka ujao kuwa kiongozi wa wamumini wa Kianglikana dunia nzima.

- BBC Swahili -