Advertise Here

Friday, November 2, 2012

Semina ya "Challenges After Campus Life" na Samuel Sasali.

Samuel Sasali akizungumza kwenye Semina
 ALL the way from Dar es salaam to Mwanza, ni Samuel Sasali a.k.a Papaa katika Semina maalum ya Wanachuo wa St. Augustine University of Tanzania iliyopewa jina la "Challenges After Campus Life".
Wanachuo wakifuatilia Semina kwa Makini
Semina ikiendelea
 Ikiwa leo ndo ilikuwa Siku ya Kwanza ya Semina ambayo ilifanyika katika Kanisa la T.A.G lililopo Nyamalango Malimbe, pembezoni kabisa mwa Chuo cha SAUT.
Imeeleweka????
Daniel Liberati(M/Kiti Tafes Saut-Kushoto), Remmy Paschal(Katibu Tafes Saut-Katikati), na Samwel Madaha(M/Kiti Tafes Mkoa wa Mwanza-Kulia)
Semina hii imeandaliwa na TAFES Saut kwa kushirikiana na Mtumishi Samuel Sasali, ikiwa na lengo la kuwaandaa wanachuo hawa kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali pindi wamalizapo masomo yao chuoni.
Watumishi wa Mungu wakifuatila Semina kwa Makini
Haachwi mtu hapo
 Semina hiyo itakayodumu kwa Siku 2, itamalizika Siku ya Kesho kwa kufanyika katika Ukumbi wa M1 uliopo ndani ya Chuo Kikuu cha Mt. Augustino.
Sam Sasali akiendelea na Semina
Mtangazaji wa Alive Fm Adolph Nzwalla akijitambulisha kwa wanasemina
Sadaka ni sehemu ya Ibada, na ilipofika wakati wa kutoa Sadaka Maombi yakafanyika kwanza.
Sadaka Mkononi
Happy people
Sehemu ya wanasemina
 Semina ilimalizika mida kama ya Saa 2 Usiku hivi ili kumpa nafasi Mtumishi huyu kuandaa Materials a.k.a Nondo kwa ajili ya Semina ya Kesho.
Papaa baada ya kumaliza kutoa Ujumbe wa leo
M/Kiti Tafes Mkoa wa Mwanza Bw. Samwel Madaha akiwasalimu wanasemina
Kwa leo tumalize hiviiiiiiii..........
Blogger Sowane Emmanuel akiwa na Papaa baada ya Kumalizika kwa Semina
Kutoka Kushoto ni Yusuph Magupa, Sam Papaa, Ruth Lyanga na Adolph Nzwalla
 Tukutane Kesho Ukumbi wa M1 kwa Muendelezo wa Semina hii tukiwa na Mtumishi Samuel Sasali, ambaye pia ni Christian Blogger.

Be Blessed!