Advertise Here

Tuesday, September 10, 2013

Aic Kambarage Vijana Choir wazindua DVD yao.

AIC Kambarage wakihudumu siku ya Uzinduzi
Wiki moja iliyopita, yaani Septemba 1, 2013 Vijana wa Kanisa la AIC Kambarage walizindua DVD ya album yao ijulikanayo kama "Kaa Ukijua" katika Viwanja vya Kanisa la AIC Kambarage, Mkoani Shinyanga.

Mgeni rasmi katika Uzinduzi huo alikuwa ni Mbunge wa viti maalum Shinyanga Mh. Rachel Mashishanga(Chadema). DVD ya Album hiyo iliwekwa wakfu na Mch. Masasila.

Hivi ndivyo ilivyokuwa.....
Mgeni rasmi Mh. Rechal Mashishanga(Katikati)
AIC Kambarage
Mh. Rachel Mashishanga akizindua DVD ya AIC Kambarage
Mgeni rasmi na Mgeni mwenza
Mch. Masasila akiweka wakfu album ya AIC Kambarage
DVD hii sasa ipo Madukani, Hakikisha unajipatia Nakala yako.