Advertise Here

Tuesday, September 10, 2013

Solomon Mukubwa aelezea chanzo cha kupoteza mkono wake wa kushoto.

Solomon Mukubwa
Mwimbaji wa nyimbo za Injili wa Nchini Kenya na mwenye asili ya Kongo, Solomon Mukubwa ameelezea jambo lililopelekea kupoteza mkono wake wa kushoto.

Solomon anasema akiwa na Umri wa Miaka 12, Uvimbe ulianza katika mkono wake wa kushoto, na hivyo wazazi wake walimchukua na kumpeleka katika hospitali mbalimbali na hata kwa waganga wa kienyeji ili kufahamu chanzo cha uzimbe huo lakini kote huko hawakufanikiwa kujua chanzo cha uvimbe huo.

Solomon aliishi na uvimbe huo kwa Miaka 3. Baadaye ilifunguliwa hospitali flani ya wazungu iliyokuwa karibu na nyumbani kwao hivyo wazazi wake walimpeleka hapo pia, lakini majibu yakawa ni yale yale. Madaktari wa hospitali hiyo baada ya kuona uvimbe unazidi na hawaoni chanzo cha uvimbe huo, walishauri mkono wa Solomon Mukubwa ukatwe ili kunusuru maisha yake.

Solomoni aliendelea kusema kuwa hakuna mtu aliyejua kuwa uvimbe huo umetokana na nini lakini hapo baadae ilidhihirika wazi kuwa mama yake wa kambo ndie aliyemroga na kumsababishia tatizo hilo kwani baadae alikuja kukiri na kueleza ukweli. 

Solomoni ambaye kwa sasa maskani yake yapo jiji la Nairobi nchini Kenya anasema wimbo wake wa Mfalme wa Amani aliutunga ili kumtukuza Mungu baada ya kumuepusha na kifo ambacho kingempata baada ya mama yake wa kambo kumroga na kusababisha mkono wake kuvimba na kutibiwa na madaktari bingwa bila mafanikio na hata alipoenda kwa waganga wa kienyeji pia hakupona. 

“Wimbo wangu wa Mfalme wa amani niliamua kuuimba baada kuvuka katika shida hizo na albamu yangu kuipa jina la Mungu mwenye nguvu, na kuna maneno niliweka kwenye kibao hicho kwamba, ukiwa na shida usiende kwa waganga wa dunia, mwite mfalme wa amani, yeye anajibu maombi,” alisema Solomoni Mukubwa.