Advertise Here

Tuesday, September 3, 2013

Yaliyojiri katika kuuaga Mwili wa Askofu Dr. Mosses Kulola Uwanja wa CCM Kirumba.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Engeneer Evarist Ndikiro akitoa heshima za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu
Lilikuwa si jambo la kuamini kwa haraka kama kweli Askofu Dr. Mosses Kulola katutoka, lakini ilibidi kukubaliana na ukweli huo kwani wakati huu watu waliweza kuushuhudia mwili wa Marehemu Babu/Baba yetu ukiwa katika Jeneza.
Mwili wa Marehemu ukiwa Uwanja wa CCM Kirumba
Watu wengi sana walifurika Uwanja wa CCM Kirumba japokuwa leo ilikuwa ni Siku ya kazi. Kila alitamani ajionee kwa macho yake ili aamini ukweli uliopo ya kuwa hatuko tena na Askofu Dr. Mosses Kulola.
Mch. Dastan Mboya akieleza namna alivyomfahamu Askofu Mosses Kulola
Viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama mbalimbali na Viongozi mbalimbali wa Makanisa tofauti tofauti waliweza kufika Uwanja wa CCM Kirumba ili kutoa heshima zao za mwisho kwa Mwili wa Marehemu wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Engeener Evarist Ndikiro.
Ndugu wa Marehemu wakiwa Uwanjani
Maaskofu, Wachungaji na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Mwanza walifika Uwanjani hapo, pia alikuwepo Mwl. Christopher Mwakasege kutoka Mkoani Arusha akiongozana na baadhi ya wanahuduma wa MANA.
Umati wa watu
Zoezi la kutoa heshima za Mwisho lilianza mida ya Saa 2:30 Asubuh, na lilikamilika mida ya Saa 10 Jioni, huku watu wakipata fursa ya kusikiliza Wasifu wa Askofu Dr. Mosses Kulola pamoja na viongozi mbalimbali kutoa rambirambi zao pamoja maneno machache namna wanavyomfahamu Marehemu Askofu Mossas Kulola.
Bango lenye picha ya Marehemu Askofu dr. Mosses Kulola
Sikiliza hapa chini Neno la Mungu lililotolewa leo katika kuuaga mwili wa Marehemu Askofu Dr. Mosses Kulola

Na huu hapa chini ndio Wasifu wa Askofu Dr. Mosses Kulola uliotolewa na Ndugu Limbu katika Uwanja wa CCM Kirumba

Kauli ya Mwl. Christopher Mwakasege akiwa Uwanja wa CCM Kirumba wakati wa kuwasilisha Rambirambi kwa Familia ya Marehemu

Kauli ya Askofu Eugene Murisa wa Kanisa la High Way of Holliness Cathedral akitoa rambirambi kwa Familia ya Marehemu

Mwili wa Marehemu utazikwa kesho katika Kanisa la EAGT Bugando kuanzia mida ya Saa 2:00 Asubuhi. Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina lake libarikiwe.